Je, waweza kufanya ukarimu kwa watu usiowafahamu?

Ukarimu

Chanzo cha picha, Getty Images

Liberia imetajwa kuwa namba moja duniani kwa kuwa wakarimu na kusaidia watu wasio wafahamu.

Kwa mujibu wa ripoti ya hali ya ukarimu duniani (world giving index) Liberia ndio ya nchi kwanza kwa ukarimu.

Ripoti ya hali ya ukarimu duniani hutolewa kila mwaka na kuchapishwa na shirika la msaada la Uingereza la 'Charity Aid Foundation' na kutumia takwimu zinazokusanywa kisha kupanga kwa idadi ya nchi zaidi ya 140 duniani kwa jinsi walivyo na ukarimu.

Lengo la ripoti hii ni kuonesha hali ya ukarimu duniani.

Kusaidia watu usiowafahamu ni miongoni mwa vigezo vya kuongoza katika ripoti hiyo.

Ripoti hiyo pia imeangalia ni kiasi gani cha fedha watu huchangia katika misaada na kiasi gani watu kuhijihusisha na shughuli za kujitolea.

Tafiti hii imefanywa kwa muda wa miaka 10 na kuangazia watu milioni 1.3 duniani kote.

Katika orodha hiyo ya pamoja, Kenya imeorodhozeshwa kuwa nchi yenye ukarimu zaidi Afrika na ya 11 kwa dunia.

Liberia ilikua ya 13 na, Sierra Leone ya 20 na Nigeria ya 22.

Lakini kwa upande wa kuwa karibu na watu usiowajua Afrika ndio imeongoza.

Katika kipengele hicho cha kuwasaidia usiowafahamu, Sierra Leone (ya pili), Kenya (ya nne), Zambia (ya tano), Uganda (sita), Nigeria (saba) and Malawi (ya 10).