Tetesi za soka Ulaya Alhamis tarehe 17.10.2019: Eriksen, Allegri, Longstaff, Mandzukic

Tottenham huenda wakamtoa kiungo wa Mdenmark Christian Eriksen, mwenye umri wa miaka 27, na badala yake wakamchukua kiungo wa kati wa Real Madrid Muhispania Isco, mwenye umri wa miaka 27, katika kipindi cha uhamisho wachezaji mwezi Januari . (El Desmarque, via Express)
Arsenal wameripotiwa kutoa ofa kwa Real Madrid kwa ajili ya winga Muhispania Lucas Vazquez, mwenye umri wa miaka 28, kabla ya kipindi cha uhamisho cha Januari (El Desmarque, via Football.London)
Unaweza pia kusoma:
Meneja wa zamani wa Juventus Massimiliano Allegri anaweza kumchukua mshambuliaji wa wa Croatia Mario Mandzukic, mwenye umri wa miaka 33, na kiundo wa kati wa Mjerumani Emre Can, mwenye umri wa miaka 25, pamoja nae katika Manchester United ikiwa atachukua nafasi ya Ole Gunnar Solskjaer kama meneja wa United. (Tuttosport, via Express)

Chanzo cha picha, Getty Images
Badala yake , Manchester United watasaini mkataba na wachezaji sita katika vipindi sita vya dirisha la uhamisho akiwemo Moussa Dembele kutoka Lyon, kiungo wa kati wa Atletico Madrid Saul Niguez na James Maddison Leicester City (Mail)
Anderlecht wamepigwa faini ya pauni ya £4,315 na shirikisho la soka la Ubelgiji kwa kumteua mlinzi wa zamani wa Manchester City Vincent Kompany, mwenye umri wa miaka 33, kama kocha mkuu wakati hana vigezo vya kufuzu . (Sun)

Chanzo cha picha, Getty Images
Mshambuliaji wa kati wa Manchester City Muargentina Aguero, mwenye umri wa miaka 31, amegongesha gari lake la Range Rover lenye thamani ya pauni £150,000 alipokuwa akielekea kwenye mazoezi lakini hakuumia . (Mail) Newcastle watatoa ofa ya miaka mitano zaidi ya mkataba na mchezaji wa safu ya mashambulizi Muingereza Matty Longstaff. Kijana huyo mwenye umri wa miaka 19-anakamilisha mkataba wake msimu ujao. (mail)

Chanzo cha picha, Getty Images
Leicester, West Ham na Valencia kwa pamoja wanajaribu kusaini mkataba na kiungo wa kati wa Arsenal Mohamed Elneny katika msimu ujao kabla kijana huyo mwenye umri wa miaka 27 kutoka Misri kwenda katika kikosi cha Besiktas nchini Uturuki. (Leicester Mercury)
Nahodha wa zamani Manchester United Paul Ince anasema kuwa "hajui wanafanya nini katika klabu "na kwamba United wanaweza kumaliza wakiwa miongoni mwa timu sita za mwisho katika Primia Ligi mwaka huu . (Talksport)

Chanzo cha picha, Getty Images
Kocha wa zamani wa Tottenham Clive Allen amefichua kuwa alizuiwa kumpiga meneja wa zamani wa Arsena -Arsene Wenger na mlindalango Carlo Cudicini. (Mail)
Chelsea imefichua rasmi kwamba ndiyo timu iliyo chafu zaidi katika Primia Ligi , huku kukiwa hakuna klabu iliyopokea kadi zaidi kuwaliko tangu mwaka 1992. (Star)
Leeds United wanamfuatilia kwa karibu mlinzi wa Chelsea Reece James, mwenye umri wa miaka 19, na wanatumai kuweza kumchukua kwa mkopo mwezia Januari. (Football Insider)

Chanzo cha picha, Getty Images
Timu ya ligi ya Uturuki Galatasaray inajiandaa kumaliza msimu mrefu wa mkopo wa kiungo wa kati wa Southampton Gabon Mario Lemina, mwenye umri wa miaka 26, mwezi Januari. (Fotomac, via Sport Witness)
Kiungo wa kati wa Chelsea Mskochi Billy Gilmour,mwenye umri wa miaka 18, aliomba kutoka nje ya klabu kwa mkopo lakini ombi lake lilikataliwa na meneja wake Frank Lampard. (Sun)
Mshambuliaji wa safu ya kati Eddie Nketiah, mwenye umri wa miaka 20, anasema mbinu za mchezaji wa England wa kikosi cha vijana wenye chini ya umri wa miaka 21 alizoziona Jumanne zinaonyesha kuwa anastahili kuanza kuichezea Leeds wakati mkataba wake wa mkopo utakapomalizika Arsenal.(Independent)

Chanzo cha picha, Reuters
Everton wanamsaka kiungo wa kati wa Bolton Muingereza Ronan Darcy, mwenye umri wa miaka 18, na Mromania anayecheza katika safu ya kati ya Romania Dennis Politic, ambaye sasa ana umri wa miaka 19. (Football Insider)
Kiungo wa kati wa Chelsea Christian Pulisic, mwenye umri wa miaka 21, aliangua kilio baada ya kuondolewa uwanjani na kuingizwa kwa mchezaji mwingine katika mechi nchini Marekani wakati waliposhindwa na Canada 2-0 . (Mirror)

Chanzo cha picha, Getty Images
Mlinzi wa Watford Mcolombia Jorge Segura, mwenye umri wa miaka 22, atarejea katika klabu hiyo mwezi wa Januari kama klabu ya Atlas ya ligi ya Mexico kama hawatataka kuufanya mkataba wake wa mkopo kuwa wa kudumu (Futbol Total, via Sport Witness)
Kocha wa Arsenal Unai Emery hatazamii kupanua kikosi chake mweizi Januari wakati wa kipindi cha uhamisho wa wachezaji. (The Athletic, via Mirror)

Chanzo cha picha, AFP
Tottenham wameimarisha haja yao ya kumtaka Jose Mourinho huku kukiwa na hali ya sintofahamu kuhusu msimamo wa Manchester United wa kumtaka Mauricio Pochettino. (Daily Express)
Mshambuliaji wa Chelsea Mfaransa Olivier Giroud,mwenye umri wa miaka 33, anajiandaa kuondoka katika klabu hiyo mwezi wa Januari ikiwa hatacheza tena. Inter Milan na timu ya Ligi kuu ya Canada Vancouver Whitecaps ni miongoni mwa timu zinazomtaka. (Sun)













