Je simu yako ya Androdi itaathiriwa na mfumo mpya wa Huawei?

Baada ya miezi kadhaa ya kutoa kauli zinazokinzana sasa wakurugenzi wa kampuni ya bidhaa nyingine za kielektoniki Huawei ya uchina wamefichua mfumo mpya uliotengenezwa na kampuni hiyo kwa ajili ya kuboresha simu za mkononi za Samartphones, vipakatalishi na vifaa vingine vya nyumbani.

Mfumo huo wa Huawei -HarmonyOS unalenga kupunguza utegemezi wake kwa kampuni za Marekani.

HarmonyOS utakuwa tayari kuwekwa katika skrini za samart kwenye bidhaa kama vile Televisheni, saa za smart , na magari baadae mwaka huu, amesema Richard Yu, Mkurugenzi mkuu wa wa kitengo cha walaji cha Huawei katika mkutano wa ubunifu.

Katika kipindi cha miaka mitatu ijayo Huawei,kampuni ambayo ni ya pili kwa ukubwa duniani ya mauzo ya smartphone , itaangalia jinsi ya kuuweka mfumo wa HarmonyOS kwenye vifaa zaidi zikiwemo siku zake za mkononi aina ya smartphones, amesema.

Yu alidai kuwa , bila kutoa ushahidi halisi ,kwamba HarmonyOS ni "yenye nguvu zaidi na bora zaidi ya mfumo Android." "Inaweza kuwekwa katika smartphones? Bila shaka."

" HarmonyOS unaweza kuwekwa katika hali ya kuwa na maingiliano na kifaa kingine chochote kile . Ukitengenezwa kwa njia ya kifaa chenye uwezo wa kusambaza data , HarmonyOS inaweza kujenga mwanzao wa uhusiano shirikishi wa mfumo wa ikolojia," ilieleza taarifa ya kampuni hiyo.

Kampuni ya Huawei inasema kuwa imeazimia kuendelea kutumia Android , lakini HarmonyOS utatumika kama mbango mbadala kama mambo yataenda kombo . "tutaupa kipaumbele mfumo wa Android kwa smartphones, lakini kama hatutatumia Android, tutaweza kuweka mfumo wa HarmonyOS haraka," Yu amesema.

Kuwepo kwa mfumo wa simu za mkononi ,ambao ni chanzo cha wazi utakuwa ni kwa ajili ya Uchina pekee kwa sasa, ingawa kampuni ina mipango ya kuuleta katika masoko ya kimataifa baadae , amesema.

Tangazo hilo la Huawei limekuja miezi kadhaa baada ya serikali ya Marekani kuweka masharti ya kibiashara nchini Marekani yanayoilenga kampuni hiyo pamoja na kampuni nyingine washirika .

Serikali ya Marekani imeishutumu Huawei kwa kuiba siri za kibiashara , na ikasema inaleta hatari kwa usalama wa taifa.

Huawei inapinga shutuma zote hizi na imeamua kuchukua mbinu za kisheria kukabiliana na shutuma za Marekani.

Baada ya shutuma hizo , Google, Intel,na makumpuni mengine yanayochngia katika kwa kiasi kikubwa katika teknolojia na utatuzi wa matatizo ya smartphone walisitisha biashara na Huawei, huku wakihoji juu ya hali ya baaadae ya kampuni hiyo.

Vita vinavyoendelea vya kibiashara baina ya Marekani na China tayari vimeanza kuiathiri Huawei. Utendaji wa kampuni umeripotiwa kuwa ni dhaifu kufikia hadi mwezi Juni.

Ambalo haliko wazi ni ukubwa wa athari za shutuma za Marekani dhidi ya Huawei juu ya jina i lake duniani.

Kwa mujibu wa kampuni ya utafiti ya Counterpoint, karibu nusu ya simu za martphones za Huawei huuzwa nje ya Uchina.

Huawei ilikuwa imejipanga kuwa muuzaji mkubwa zaidi wa bidhaa nje ya nchi duniani, jambo ambalo ingelifanikisha "kama ingekuwa si vita vya kibiashara ," amesema Yu.