Familia ya Kenya yaunganishwa na kutunzwa dola $50,000 Marekani.

Chanzo cha picha, The Ellenshow You Tube
Familia ya Kenya imeshinda tuza la $50,000 (Ksh.5,000,000) katika kipindi cha Televisheni cha mchekeshaji wa Kimarekani Ellen Degeneres' cha 'The Ellen Show.'
Zawadi hiyo ilitolewa baada ya muongozaji wa kipindi cha televisheni cha Marekani Ellen Degeneres kumkutanisha Achieng' mwakamke raia wa Kenya anayeishi Marekani na familia yake baada ya kutengana kwa miaka miwili.
Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue
Mwisho wa X ujumbe, 1
Mchekeshaji huyo alimuita kwenye jukwaa Achieng Agutu aliyeondoka kwenda Marekani kupata elimu ya juu na baadae alimshitukiza kwa kumuunganisha na familia yake kwa njia ya simu ya video.
Achieng aliishi na familia ya muongozaji wa kipindi, inayohfahamika kama the Graces lakini anafanya kazi ya kudumu lakini bado anaweza kuhudhuria masomo shuleni.
"Nilihamia hapa (Marekani ) karibu miaka mitano iliyopitakwa kupata elimu ya juu na mambo yamekuwa mazuri, lakini bado imekuw ani vigumu sana kwa familia yangu nyumbani Kenya kwasababu kusema ukweli wamefanya kila wawezalo kuanzia kuuza ardhi, kuchukua mikopo ili waweza kulipa karo yangu ya shule na kuhakikisha ninaishi vizuri ," alielezea Achieng.
Aliongeza kusema kuwa wazazi na ndugu zake wamekuwa wakisaidia zaidi ya watoto 10 wanaotoka katika familia zisizojiweza nchini Kenya kwasababu wanahisi wamebarikiwa.
Achieng' ambaye alijawa na furaha alielezea kuwa pia anafanya kazi ya udereva katika kampuni ya Uber , kuwalea watoto, mwalimu wa kiingereza na wakati mwingine husafisha nyumba za watu na kuosha magari ili kupata pesa za ziada.
Aidha alielezea jinsi kutazama kipindi cha Ellen ilivyomsaidia kuifahamu vizuri lugha ya kiingereza.
Alisema: ''Nilijifunza lugha ya kiingereza kwa kusikiliza wasanii wa muziki kwenye kipindi cha Ellen Show, na kuandika maneno na baadae kutafuta maana ya maneno hayo, na hivyo kuzungumza vizuri maneno ya kiingereza''
Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue
Mwisho wa X ujumbe, 2
Kaka yake mkubwa pia Churchill yuko nchini Afrika Kusini kutafuta maisha bora.
Baada ya hapo Ellen alijifanya anaenda kutengeneza mtambo wa mawasiliano ya video yaliyokuwa yamekatika nyuma ya jukwaa, lakini alipokaribia lango, Achieng aliiona familia yake ana kwa ana na familia kwa njia ya video. Haya yalikuwa yakiendelea huku familia ya Achieng' ikiwa nyuma ya jukwaa.
Achieng' alishituka sana kuona familia yake ikija jukwaani alipokuwa.
Baba yake alielezea kuwa kukutana tena kama familia ni jambo kubwa sana.
Baadae walicheza mchezo wa bahati nasibu ulioandaliwa na kampuni ya Walmart na kuchagua namba 2 ambayo huja na zawadi ya juu zaidi ya dola $50,000.
Baadhi ya Wakenya wamemkosoa Achieng
Licha ya kushinda kiwango kikubwa cha pesa, baadhi ya Wakenya kwenye mitandao ya kijamii wamemkosoa Bi Achieng' Agutu ambaye ni mzaliwa wa kisumu nchini Kenya kwa kudai kuwa alijifunza kiingereza kupitia kipindi cha 'The Ellen Show.' huku wakidai hakuwa mkweli kwa hili na baadhi walidai alisema hivyo ili kujipatia pesa. Baadhi wametuma picha za kukejeli madai ya Achieng' :
Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue
Mwisho wa X ujumbe, 3

Mwisho wa X ujumbe, 4

Mwisho wa X ujumbe, 5
Baadhi pia walidai familia yake inajiweza kinyume na yeye alivyojaribu kuueleza umma kupitia kipindi cha 'The Ellen Show.'
Unaweza pia kutazama: