Waziri ataka uchaguzi mpya ufanywe mapema Kenya

Wizara wa elimu Kenya yatao ratiba na mitihani ya kitaifa

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Wizara wa elimu Kenya yatao ratiba na mitihani ya kitaifa

Waziri wa elimu nchini Kenya Dkt Fred Matiang'i ametoa wito kwa Tume ya Uchaguzi nchini humo kuandaa uchaguzi kufikia tarehe 17 Oktoba ili kuhakikisha mitihani ya kitaifa haiathiri na uchaguzi huo.

Tume ya uchaguzi ina hadi Oktoba 31 kuandaa uchaguzi mpya baada ya matokeo ya uchaguzi wa urais wa awali kubatilishwa na Mahakama ya Juu Ijumaa wiki iliyopita.

Wizara ya elimu nchini Kenya imesema kuwa maandalizi ya mitihani ya mwisho ya kidato cha nne KCSE na darasa la nane KCPE yamekamilika.

Wizara hiyo imetoa ratiba ambayo tayari imetumwa kwa shule ambapo mtihani wa darasa la nane KCPE utaanza tarehe 31 mwezi Oktoba mwaka 2017 na kukamilika tarehe 2 Novemba mwaka 2017.

Matayarisho ya mtihani huo wa KCPE yatafanyika Jumatatu tarehe 30 Oktoba mwaka 2017.

Wanafunzi wa kidato cha nne nao wataanza kufanya mtihani wao wa KCSE tareha 6 Novemba mwaka 2017 na mtihani huo uatamalizika tarehe 29 Novemba mwaka 2017.

Wizara wa elimu Kenya yatao ratiba na mitihani ya kitaifa

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Wizara wa elimu Kenya yatao ratiba na mitihani ya kitaifa

Matayarisho ya mtihani wa KCSE yatafanytika tarehe 3 Novemba mwaka 2017.

Huku zoezi la uchaguzi mkuu wa urais nalo likiwa niiani, waziri wa elimu Fred Matiang'i, ameandika barua kwa tume huru ya uchaguzi na mipaka kuomba zoezi la upigaji kura likamike ifikapo tarehe 17 Oktoba mwaka 2017 kuzuia kuvurugwa shughuli za mitihani.

Jumla ya wanafunzi 1,003,556 walijiandikisha kufanya mtihani wa darasa la nane wa KCPE huku wanafunzi 615,773 wakijiandikisha kufanya mtihadi wa kidato cha nne wa KCSE.

Kutakuwa na jumla ya vituo 28,566 vya kufanyia mtihani wa KCPE na vituo 6,037 vya kufanyia mtihani wa KCSE.