'Walazimishwa kujenga' uwanja wa kombe la dunia Qatar

Wajenzi wa viwanja vya kombe la dunia Qatar

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha, Wajenzi wa viwanja vya kombe la dunia Qatar

Kundi la haki za kibinadamu Amnesty International limeishtumu Qatar kwa kuwafanyisha watu kazi kwa lazima katika uwanja utakaochezewa mechi ya ufunguzi wa michuano ya Kombe la Dunia 2022.

Amnesty linasema kuwa wafanyikazi katika uwanja wa Khalifa wanalazimishwa kuishi katika mazingira machafu, wanalipa fedha nyingi ili kuajiriwa huku baadhi ya mishahara yao ikizuiliwa na kupokonywa pasipoti zao.

Uwanja wa Kombe la dunia nchini Qatar

Chanzo cha picha, AP

Maelezo ya picha, Uwanja wa Kombe la dunia nchini Qatar

Pia imelishtumu shirikisho la soka duniani Fifa kwa kushindwa kuzuia dimba hilo linaloandaliwa chini ya unyanyasaji wa haki za kibinadamu.

Qatar imesema kuwa ina wasiwasi kuhusu madai hayo na kwamba itayachunguza.

Serikali ilisema kuwa maslahi ya wafanyikazi wahamiaji yanapewa kipaumbele na kusisitiza kuhusu marekebisho ya sheria za kazi nchini humo.

Uwanja wakombe la dunia Qatar

Chanzo cha picha, Getty

Maelezo ya picha, Uwanja wakombe la dunia Qatar

Mwaka uliopita taifa hilo liliahidi kufanyia marekebisho mfumo wa ''Kafala'' ambao huwazuia wafanyikazi wahamiaji kubadilisha kazi ama hata kuwacha kazi bila idhini ya mwajiri wao.

Lakini Amnesti imeonya kwamba marekebisho hayo hayataleta tofauti yoyote na kusema kwamba baadhi ya wafanyikazi ''wanakabiliwa na wakati mgumu''.