Afisa wa FIFA apelekwa Marekani kushtakiwa

Jose Maria Marin
Maelezo ya picha, Jose Maria Marin

Mtu ambaye ndiye aliyeratibu Fainali za Kombe la Dunia mwaka 2014 huko nchini Brazil Jose Maria Marin ametolewa kutoka Uswisi kwenda nchini Marekani ili akashtakiwe kwa tuhuma za rushwa.

Bw Marin alikuwa ni miongoni mwa maafisa saba wa Shirikisho la Soka Duniani FIFA waliokamatwa nchini Uswisi mwezi Mei.

Anatuhumiwa kupokea rushwa ya mamilioni dola kutoka kampuni za masoko ya michezo kuhusiana na mashindano ya Copa Amerika na Mashindano ya Brazil ya Copa Brazil.

Watawala nchini Uswisi wamesema amesindikizwa na maafisa wa polisi wa Marekani kwenye ndege kutoka Zurich kwenda New York.

Iwapo atapatikana na hatia anaweza kuhukumiwa kifungo cha hadi miaka 20 jela.