Tetesi za Soka Ulaya Jumatatu 04.04.2022: Phillips, Haaland, Akanji, Rudiger, Araujo, Martinez, Fabianski

th

Chanzo cha picha, Getty Images

Barcelona hawako tayari kutimiza matakwa ya awali ya kifedha ya Antonio Rudiger lakini watakuwa na mkutano mwingine na beki huyo wa kati wa Ujerumani, 29, kuhusu uhamisho wa bure kutoka Chelsea msimu huu wa joto. (Sport - in Spanish)

Aston Villa itashinikiza kutaka kumnunua kiungo wa kati wa Leeds United na Uingereza Kalvin Phillips, 26, kwa pauni milioni 60 msimu huu. (Telegraph - subscription required)

Nyota anayelengwa na Manchester United Manuel Akanji, 26, anataka kuondoka Borussia Dortmund na beki huyo wa Uswizi anafikiria kuhamia Ligi ya Premia. (Sport1)

Mshambulizi wa Borussia Dortmund na Norway Erling Braut Haaland, 21, ataamua kufikia mwisho wa Aprili ikiwa atajiunga na Real Madrid, Barcelona au Manchester City msimu huu wa joto. (Sport - in Spanish)

th

Chanzo cha picha, Getty Images

Barcelona wanataka kuafiki kuongeza mkataba kwa Ronald Araujo, ambaye amepokea ofa kutoka kwa Manchester United, lakini mlinzi huyo wa kati wa Uruguay, 23, hajachukulia kwa uzuri Barca kuwania Rudiger na mlinzi wa Chelsea Mdenmark Andreas Christensen, 25. (Sport - in Spanish)

Arsenal na Tottenham wanavutiwa na Lautaro Martinez lakini Inter Milan itamuuza tu mshambuliaji huyo wa Argentina, 24, ikiwa watapokea ofa ya zaidi ya euro 80m (£67.3m). (Calciomercato - in Italian)

th

Chanzo cha picha, Reuters

West Ham itamtuza kipa wa Poland Lukasz Fabianski, 36, kwa kandarasi mpya ya msimu ujao. (Mail)

Aston Villa itajaribu kupata uhamisho wa kudumu kwa Anwar El Ghazi msimu huu wa joto, lakini Everton hawana mpango wa kumsajili winga huyo wa Uholanzi, 26, wakati muda wake wa mkopo na Toffees utakapomalizika. (Football Insider)

Derby County huenda ikatoza ada kubwa kwa mlinda mlango Jack Thompson, 15, huku Manchester City, Tottenham na Chelsea zikiwa na nia ya kumnunua mchezaji huyo wa kimataifa wa Uingereza. (Sun)

Birmingham City wanajizatiti kutaka kuwindwa na vilabu vya Ligi ya Premia na Uropa kumnunua kiungo wao wa kati wa England chini ya umri wa miaka 18 George Hall, 17. (Mail)

th

Chanzo cha picha, Getty Images

Newcastle wanapanga kutoa ofa ya pauni milioni 20 kwa Brighton kwa mlinda mlango wa Uhispania Robert Sanchez, 24, msimu wa joto na pia wanalenga winga wa Watford wa Senegal Ismaila Sarr, 24. (Sun)

Everton itamruhusu Allan aondoke msimu wa joto, licha ya kiungo huyo wa kati wa Brazil, 31, kusalia na mwaka mwingine kwenye mkataba wake. (Sun)

Kiungo wa kati wa zamani wa kimataifa wa Armenia Henrikh Mkhitaryan amemaliza mkataba wake mwishoni mwa msimu huu, lakini baada ya kuboreka kwa kiwango chake cha mchezo, Roma wanajiandaa kuanzisha mazungumzo juu ya mkataba mpya wa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 33 wiki hii.

(Fabrizio Romano on Twitter)