Tetesi za soka Ulaya Jumapii tarehe 07.02.2022 : Carvalho, Rudiger, Logbo, Gnabry, Wijnaldum

Chanzo cha picha, Getty Images
Manchester United "wanafuatilia kwa karibu mambo yanavyokwenda" huku mlinzi wa Chelsea Antonio Rudiger akiripotiwa kukataa ofa ya hivi karibuni ya mkataba wa klabu hiyo, mlataba wa thamani ya karibu pauni laki 200 kwa wiki . (Football 365)
Liverpool wanamfuatilia kwa karibu mchechajiwa klabu ya Le Havre mwenye umri wa miaka 17 Andy Elysee Logbo ambaye alikuwa analinganishwa na mshambuliaji wa Chelsea Romelu Lukaku. (Mirror)

Chanzo cha picha, Getty Images
Liverpool itafanya mazungumzo na Fulham mwezi huu kuhusu mkataba kwa ajili ya mshambuliaji mwenye umri wa miaka 19 Fabio Carvalho, huku wakitaka kufikia makubaliano kabla ya msimu ujao. (Football Insider)
Hatahivyo, AC Milan wana matumaini ya kuwahi dau la Liverpool na kusaini mkataba na Carvalho huku klabu hiyo ya Italia ikiwasiliana na wawakilishi wa Carvalho. (Calciomercato - in Italian)

Chanzo cha picha, Getty Images
Manchester United na Liverpool kwa Pamoja zinamfuatilia kwa karibu winga wa Bayern Munich Serge Gnabry huku kukiwa na mzozo wa mkataba baina ya klabu hiyo ya Ujerumani na mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 26, wakati Barcelona na Real Madrid pia wakimtaka. (Mirror via Sky Germany)
Mshambuliaji wa West Ham Michail Antonio ameitaka klabu hiyo kuboresha kikosi chake cha mashambulizi na kusaini mkataba na mshambuliaji mwingine msimu huu. (Teamtalk via The Footballer's Football Podcast)

Chanzo cha picha, Getty Images
Kiungo wa kati Jack Wilshere, 30, ameelezea ni kwanini ameendelea kuwa wakala huru kwa kufichua kuwa meneja wa Arsenal Mikel Arteta " hamtaki " yeye asaini mkataba katika klabu hiyo . Wilshire amekuwa akifanya mazoezi na klabu yake ya zamani. (Mirror)
Mkurugezi wa AC Milan Paolo Maldini anasema mshambuliaji Zlatan Ibrahimovic, 40, atasaini mkataba mpya katika klabu. (Goal)

Chanzo cha picha, Getty Images
Uvumi unaozingira hatua ya Arsenal kumtaka mchezaji wa Paris Saint-Germain Georginio Wijnaldum, 31, imejitokeza baada ya kiungo huyo wa kati kuachwa nje ya kikosi cha wanaume 25 kwa ajili ya mechi yao ijayo ya Championi Ligi dhidi ya Real Madrid. (The Sun)
Watford wamejaribu kusiani nmkataba na mlinzi Phil Jones mwenye umri wa miaka 29- kutoka Manchester United lakini hawakuweza kusaini mkataba kabla ya kufungwa kwa dirisha la uhamisho katika mwezi wa Januari. (Football Insider)

Chanzo cha picha, Getty Images
Iwapo Barcelona itashindwa kusiani mkataba na Erling Braut Haaland, 21, msimu huu wamemlenga Alexander Isak, 22, kutoka klabu ya Real Sociedad, na Antony, 21, wa Ajax , Pamoja na Lisandro Martinez, 24. (Sport - in Spanish)
Dakika chache baadaye, Mahrez alifunga bao la nne alipokimbilia pasi ya uhakika ya De Bruyne na kuona shuti lake likipanguliwa na Paulo Gazzaniga.
Manchester United pia wanajiandaa kutuma ofa ya kumnunua Araujo, ambaye mkataba wake wa Barcelona unamalizika 2023. (Marca - in Spanish)

Chanzo cha picha, Getty Images
United iko tayari kumenyana na Bayern Munich na Barcelona katika kinyanganyiro cha kumsajili Matthijs de Ligt mwenye umri wa miaka 22, beki wa zamani wa Uholanzi kutoka Juventus. (Calciomercato - in Italian)
Manchester City wana nia ya kumsajili beki wa kati wa Uruguay Ronald Araujo, 22, ambaye amesitisha mazungumzo ya kuongeza mkataba na Barcelona. (Sport - in Spanish)

Chanzo cha picha, Getty Images
The Red Devils wanapanga kurekebisha safu yao ya kiungo wa kati katika msimu ujao na Declan Rice wa West Ham, 23, Mwingereza mwenzake Kalvin Phillips mwenye umri wa miaka 26 kutoka Leeds na mchezaji wa kimataifa wa Mali wa RB Leipzig Amadou Haidara, 24, wote wakiwa katika orodha ya wanaolengwa na klabu hiyo. (ESPN)
Chelsea ilishindwa katika jaribio lao la hivi punde la kumsainisha mlinzi wa Ujerumani Antonio Rudiger kwenye mkataba mpya licha ya kutoa ofa kwa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 28 karibu pauni 200,000 kwa wiki huku Real Madrid na Paris St-Germain zikiwa na nia ya kutaka kumsajili.(Mail)












