Tetesi za Soka Ulaya Ijumaa 04.02.2022; Ronaldo, Osimhen, Neves, Calvert-Lewin, Botman, Raphinha, Zaniolo

Victor Osimhen

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Mshambuliaji wa Napoli na Nigeria Victor Osimhen

Tottenham inapania kumsajili mshambuliaji wa Napoli Victor Osimhen katika msimu wa joto baada ya kumkosa Mnigeria huyo mwenye umri wa miaka 23 ambaye alitemwa na klabu hiyo ya Italia katika dirisha la uhamisho wa Januari. (Football Insider)

Arsenal wanapanga kutumia hadi pauni milioni 180 msimu huu wa joto kumsajili kiungo wa kati wa Wolves na Ureno Ruben Neves,24, na mshambuliaji wa Everton na Uingereza Dominic Calvert-Lewin, 24, pamoja na Alexander Isak, 22, kutoka Real Sociedad. (Sun)

Mshambulizi wa Ureno Cristiano Ronaldo, 36, atasubiri hadi Manchester United itakapotangaza utambulisho wa kocha wao mpya kabla ya kuamua ikiwa atasalia Old Trafford. (ESPN)

Cristiano Ronaldo

Chanzo cha picha, Rex Features

Maelezo ya picha, Cristiano Ronaldo akishangilia kufunga bao United

Roma wako tayari kupokea ofa za euro milioni 40 (£33.6m) kwa ajili ya mshambulizi wa Italia Nicolo Zaniolo, huku Juventus na Tottenham zikiwa miongoni mwa klabu zinazomtaka kiungo huyo wa miaka 22. (Calciomercato - in Italian)

Kiungo wa kati wa Ufaransa Tanguy Ndombele amesema kazi yake Tottenham "haijaisha" baada ya mchezaji huyo wa miaka 25-kurejea Lyon kwa mkopo siku ya mwisho ya makataa. (RMC Sport via Mirror)

West Ham msimu wa joto inapanga kumtafuta beki wa kati wa Arsenal na Ufaransa William Saliba, 20, ambaye yuko Marseille kwa mkopo. Saliba pia amaehusishwa na Inter Milan, AC Milan na Real Madrid. (Jeunes Footeux via Sport Witness)

William Saliba (right)

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, William Saliba (kulia) alijiunga na Saint-Etienne mwaka 2016

Liverpool huenda ikafufua azma ya kumsaka Fabio Carvalho msimu wa joto baada ya kukaribia kumsajili mshambuliaji huyo wa Fulham mwezi uliopita. Lakini klabu za ugenini zitalipa fidia kidogo kumpata kiungo huyo wa kimataifa wa Uingereza mwenye umri wa miaka 19, katika hatua ambayo imewapa matumaini Real Madrid, Barcelona, Sevilla, Borussia Dortmund na AC Milan. (AS - in Spanish)

Mkufunzi wa zamani wa Real Madrid Zinedine Zidane, 49, bado hajakubali kuwa mrithi wa Mauricio Pochettino kama kocha wa Paris St-Germain kwa sababu anasubiri kuona ikiwa Didier Deschamps ataachia jukumu lake kama kocha wa Ufaransa. (RMC Sport - kwa Kifaransa)

Zinedine Zidane

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Zinedine Zidane, 49, bado hajakubali kuwa mrithi wa Mauricio Pochettino PSG

Winga wa Brazil Douglas Costa, 31, amepuuzilia mbali ombi la Flamengo na kukubali kujiunga na klabu ya MLS LA Galaxy kwa mkopo wa miezi sita kutoka Juventus, ikifuatiwa na mkataba wa kudumu wa miaka miwili. (Fabrizio Romano)

Newcastle itafufua azma yake ya kumsajili mlinzi wa Lille Sven Botman, 22, ikiwa itaponea kushushwa daraja kutoka kwa Ligi ya Primia baada ya kumkosa Mholanzi huyo mwezi Januari. (Athletic - usajili unahitajika)

Hata hivyo, Botman inanyatiwa na Tottenham, ambayo pia inamfuatilia mlinzi wa Inter Milan na Italia Alessandro Bastoni, 22, na Mcroatia Josko Gvardiol, 20, kutoka RB Leipzig. (Telegraph - usajili unahitajika)

Egypt celebrate

Chanzo cha picha, Getty Images