Afcon 2021: Mendy na Koulibaly nje ya kikosi cha ufunguzi cha Senegal dhidi ya Zimbabwe

Senegal itawakosa kipa Edouard Mendy na beki Kalidou Koulibaly katika mechi yao wa ufunguzi kwenye michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika baada ya wachezaji wote wawili kukutwa na virusi vya corona.

Teranga Lions, namba mbili wa michuano hiyo mwaka 2019, watamenyana na Zimbabwe katika mechi yao wa ufunguzi katika Kundi B leo Jumatatu.

Kipa wa Chelsea Mendy, beki wa kati Koulibaly na mshambuliaji Famara Diedhiou wametengwa.

"Ni hali ngumu na ngumu." Alisema kocha Alious Cisse.

Cisse anaonekana kuwa na wachezaji 17 pekee wanaopatikana kwa mechi hiyo huko Bafoussam kwa sababu ya visa kadhaa vya Covid-19 na majeraha.

"Tunaenda kuwa washindani na wale wa huko watacheza kwa wale ambao hawapo. Bado tunaenda kwenye mchezo dhidi ya Zimbabwe tukiwa na imani." Aliongeza Cisse.

Wapinzani wa Senegal katika Kundi B, Guinea na Malawi, ambao wanakutana leo Jumatatu, pia wamepoteza wachezaji katika vipimo vya afya huku wachezaji wawili wa Morocco Aymen Barkok na Auyoub El Kaabi wakiwa nje ya mechi yao ya ufunguzi ya Kundi C dhidi ya Ghana mjini Yaounde leo Jumatatu.

Sheria za Kombe la Mataifa ya Afrika zinasema nchi lazima zicheze ikiwa zina wachezaji 11 - hata kama hazina kipa anayetambulika.

Dieng wa QPR huenda akaanza golini

Koulibaly, ambaye ni nahodha wa nchi yake, alisema hana dalili na klabu ya Napoli ilisema alikuwa amechanjwa. Beki huyo wa kati mwenye umri wa miaka 30 hajacheza tangu Desemba 1 kwa sababu ya jeraha.

Senegal ilisafiri hadi Cameroon siku ya Jumatano bila wachezaji wengine sita ambao walikutwa kuwa na virusi kabla ya kuondoka.

Kipa chaguo la pili Alfred Gomis, Saliou Ciss, Bamba Dieng, Mame Baba Thiam, Pape Matar Sarr na Nampalys Mendy wote walibaki huko Dakar.

Kipa wa Queens Park Rangers, Seny Dieng, ambaye amecheza mechi moja ya kimataifa, yuko tayari kuanza dhidi ya Zimbabwe.

Mshambulizi wa Watford Ismaila Sarr na Abdoulaye Seck hawako sawa kabisa.

Maambukizi zaidi kwenye mashindano

Burkina Faso hawakuwa na kocha Kamou Malo na wachezaji sita kwnye mechi ya ufunguzi dhidi ya Cameroon siku ya Jumapili kwa sababu walikutwa na virusi.

Wakati huohuo, mkuu wa ufundi katika kikosi cha Malawi Mario Marinica na wachezaji sita wameondolewa kwenye mchuano dhidi ya Guinea, kufuatia kuripoti kesi nne zaidi wikendi.

Kikosi hicho kutoka Afrika Magharibi, ambacho walilazimika kuwaacha wachezaji watatu nyuma kwenye kambi yao ya mazoezi nchini Rwanda, baada ya mabeki Fode Camara na Ibrahima Sory Conte, kiungo wa kati Mory Konate na mshambuliaji Morgan Guilavogui wote kukutwa na virusi.

Nahodha wa Gabon Pierre-Emerick Aubameyang aliondolewa kwenye mchuono wao dhidi ya Comoro baada ya kukutwa na virusi alipowasili Cameroon siku ya Alhamisi.

Cape Verde, Misri, Gambia na Tunisia pia wachezaji wao walikutwa na virusi wakati wa maandalizi ya mechi za Kombe la Mataifa ya Afrika.