Afcon 2021: Cameroon yaishinda Burkina Faso 2-1 kabla ya Cape Verde kuizidi nguvu Ethiopia

Cameroon walitoka nyuma na kuwalaza Burkina Faso 2-1 katika mechi ya ufunguzi iliyojaa matukio mengi kwenye Kombe la Mataifa ya Afrika.

Pasi ya kistadi kutoka kwa Gustavo Sangare iliweka Burkina Faso mbele katikati ya kipindi cha kwanza huko Yaounde.

Lakini penalti mbili kutoka kwa nahodha Vincent Aboubakar ziligeuza mchezo kuwafaidi wenyeji kabla ya muda wa mapumziko.

Kipa wa Indomitable Lions Andre Onana aliokoa mabao mawili muhimu kipindi cha pili huku vijana wa Toni Conceicao wakifungua kampeni ya Kundi A kwa ushindi.

Timu ya Cape Verde iliyokumbwa na visa vya Covid-19 iliilaza Ethiopia yenye wachezaji 10 ,1-0 katika mchezo wa pili wa siku hiyo kwenye Uwanja wa Olembe, huku mshambuliaji Julio Tavares akifunga bao la kichwa dakika za lala salama.

Kuna michezo minne siku ya Jumatatu, huku washindi wa pili wa 2019 Senegal wakiwa uwanjani na mabingwa mara nne Ghana wakimenyana na Morocco saa 16:00 GMT.

Mechi ya ufunguzi ya kuvutia

Kombe la Mataifa limecheleweshwa kwa mwaka mmoja na janga la coronavirus lakini, baada ya sherehe ya kupendeza ya ufunguzi, mchezo wa kwanza ulileta shindano la kuvutia.

Beki wa Burkina Faso, Steeve Yago, alibahatika kupewa tu kadi ya manjano kwa dakika ya kwanza tu baada ya kumkabili Collins Fai, ambayo ilikuwa changamoto ya kwanza kati ya changamoto nyingi zilizoigharimu timu hiyo ya the Stallions

Burkina Faso walichukua uongozi kufuatia kipindi chao cha kwanza cha shinikizo baada ya Bertrand Traore kuona mpira wake wa kichwa ukitoka nje ya mstari na Nouhou Tolo naye Sangare akagonga mwamba wa goli kwa krosi.

Fowadi wa Aston Villa, Traore aliuchukua mpira uliolegea kwenye wingi ya kulia na kuvuka kwa wavu wa nyuma kwa Sangare, ambaye alionyesha ustadi mzuri wa kutuma pasi ya mara ya kwanza ndani ya wima wa mkono wa kushoto.

Cameroon hawakuogopa na walipewa nafasi ya kusawazisha dakika tano kabla ya mapumziko Traore alipomwangusha Andre-Frank Zambo Anguissa.

Penati hiyo ilitolewa kufuatia uhakiki wa VAR na Aboubakar alimtuma kipa Herve Koffi mkondo wa pili kutoka eneo hilo na kuurindima mpira upande wa kulia wa wavu.

Wenyeji walipata penalti ya pili katika muda wa majeruhi wa kipindi cha kwanza wakati Issoufou Dayo alipomkabili visivyo Tolo baada ya beki wa Cameroon kuucheza mpira.

Aboubakar, ambaye alifunga bao la ushindi wakati Cameroon iliponyanyua Kombe la Mataifa ya Afrika kwa mara ya mwisho mwaka wa 2017, hakufanya makosa mara ya pili alipoenda upoande wa pili na penalti yake.

Baada ya kuanza tena, Onana alizuia mpira wa adhabu wa masafa marefu kutoka kwa Traore na kumnyima Cyrille Bayala kufunga akiwa karibu.

Aboubakar alinyimwa mabao matatu kwa ilani kali ya kuotea ya VAR, wakati Zambo Anguissa alipiga shuti nje kidogo huku Indomitable Lions wakijaribu kuuweka mchezo tamati.

Wenyeji, ambao wanatazamia kunyanyua taji la bara kwa mara ya sita, wanarejea uwanjani Alhamisi, dhidi ya Ethiopia.

Ethiopia yalipia gharama kubwa kuondolewa mapema kwa mchezaji wao

Kocha Bubista na wachezaji tisa wa Cape Verde hawakuwepo kwa sababu ya Covid na Blue Sharks waliweza kutaja wachezaji sita pekee wa mechi yao dhidi ya Ethiopia.

Wachezaji hao wa Afrika mashariki walishuka hadi watu 10 mapema baada ya Yared Bayeh kushindwa kudhibiti mpira wa kichwa uliotoka nyuma na kumwangusha Julio Tavares nje kidogo ya eneo la hatari dakika ya nane.

Awali alionyeshwa kadi ya njano na mwamuzi wa Angola, Helder Martins de Carvalho, beki huyo wa kati hata hivyo alipewa kadi nyekundu baada ya ukaguzi wa muda mrefu wa VAR.

Mchezaji wa akiba Mignot Debebe nusura afunge bao la kujifunga, lakini hilo likazimwa likazimwa na kipa wa Ethiopia Teklemariam Shanko kwenye mstari, na kisha Shanko akaokoa vyema kutoka kwa kiungo Dylan Tavares.