Fahamu jinsi wanafunzi waliotekwa nyara Nigeria walivyoachiliwa

Chanzo cha picha, Getty Images
Baadhi ya wanafunzi waliokuwa wametekwa nyara kutoka katika shule ya kaskazini mwa Nigeria ya Kaduna wameokolewa.
Watu wenye silaha waliwateka nyara wanafunzi 121 kutoka shule ya malazi inayofahamika kama Bethel Baptist High School mwezi uliopita.
Mmoja wa waasisi wa shule, mchungaji John Joseph Hayab ameiambia BBC kuwa 28 kati yao sasa wameachiliwa kufuatia mazungumzo baina ya watekaji nyara na wazazi wa wanafunzi waliokamatwa.
Hakusema ni kiasi gani cha kikombozi kilichotolewa lakini alisema '' ni jambo lililowezekana .'' Mchungaji Hayab alisema watoto walioachiliwa Jumamosi walionekana 'wenye hofu kubwa, wenye mkanganiko na dhaifu .'' Walikutana na wazazi wao katika amasaa ya mapema ya Jumapili baada ya kufanyiwa uchunguzi wa kimatibabu.

Chanzo cha picha, Getty Images
Kuachiliwa kwa wanafunzi waliotekwa nyara kutoka Shule ya Bethel kumekuja wakati genge lingine likiripotiwa kumteka nyara mzee ambaye alizungumza kutoka katika shule kwao miezi mwili iliyopita katika jimbo la kati mwa Nigeria.
Watu wenye silaha walisema kiwango cha pesa kilikuwa chini ya zile walizokuwa wamekubaliana. Wazazi walisema kuwa sasa wamepoteza matumaini baada ya kuuza mali zao ikiwemo sehemu ya ardhi ya shule kuchangisha zaidi ya dola elfu sabini kwa ajili ya kuachiliwa lakini watekaji waliendelea kuwashikilia.
Zaidi ya wanafunzi elfu moja walikamatwa kutoka kwenye shule mbali mbali kote nchini Nigeria tangu mwezi Disemba mwaka jana.
Mamia yao bado wameendelea kushikiliwa huku mzozo wa kikombozi ukiendelea kuongezeka. Maafisa nchini Nigeria wanakosolewa vikali kwa kushindwa kukabiliana na kusambaa kwa usalama mvovu.












