Christian Eriksen: "Alishapoteza uhai kabla ya kufufuka": Maneno ya daktari aliyemtibu Nyota huyo wa Denmark

Eriksen

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Eriksen alikimbizwa Hospitali mara baada ya kuanguka na kupoteza fahamu uwanjani

"Alishapoteza maisha. Alishakufa kabla ya kufufuliwa."

Kwa maneno haya, Daktari wa timu ya taifa ya Denmark, Morten Boesen, anarejea tukio la jumamosi hii, lililomkumba nyota wa Denmark, Christian Eriksen.

Katika dakika ya 43 katika mechi ya kwanza ya kundi B ya michuano ya Euro 2021 kati ya Finland na Denmark, kiugo huyo anayecheza Inter Milan alikua anaelekea upande wa kulia wa uwanja kupokea mpira wa kurushwa.

Akiwa anakaribia alipepesuka mara kadhaa kabla ya kudondoka na kupigiza uso chini.

Kwa dakika kadhaa, akizungukwa na wachezaji wenzake, walioonyesha utu kwa kumzunguka kulinda faragha wakati akipatiwa matibabu ya awali.

Eriksen lipoteza fahamu katika uwanja wa Telia Parken uliopo katika jiji la Copenhagen.

Kufuatia hali hiyo, mchezo ulilazimika kusimama kwa muda mpaka alipozinduka baadae, ambapo uliendelea na Denmark ikachapwa bao 1-0.

Karibu kila nyota mkubwa wa soka duniani, alituma salama za kumtakia heri Eriksen, ili arejee katika hali yake ya kawaida.

Eriksen azungumza

Christian Eriksen anasema kwamba yuko salama kwa sasa na kuchapisha picha akiwa katika kitanda chake hospitalini akonesha kidole gumba ishara kwamba yuko katika hali nzuri.

Eriksen

Hii ilikuwa mara yake ya kwanza kuzngumza tangu alipozirai uwanjani na kukimbizwa hospitali akiichezea Denmark.

Erksen amewashukuru mashabiki kutoka kote duniani kwa risala zao za kumtakia heri.

''aSasa nitawashabiki vijana wa timu ya Denmark katika mechi yao ijayo'' , aliandika.

''Chezena kwa niaba ya raia wote wa Denmark''.

Kiungo huyo mchezeshaji yupo katika hali thabiti katika hopsitali ya Copenghagen.

''Shukran kwa risala zenu nzuri na jumbe kutoka kote duniani, aliongezea. Ina maana kubwa sana kwangu na familia''