Tetesi za Soka Ulaya Jumatatu 07.06.2021: Phil Foden, Marcus Rashford , Mason Greenwood,Mbappe, Haaland

Chanzo cha picha, EPA
Wachezaji Watatu wa Uingereza Phil Foden, Marcus Rashford na Mason Greenwood ndio wachezaji wenye thamani zaidi katika ligi tano bora za Uropa, kulingana na kundi la utafiti la CIES Soccer Observatory.
Foden wa Manchester City anaongoza orodha hiyo kwa euro 190.2m (Pauni 163.4m), mbele ya wachezaji wawili wa Manchester United Greenwood (Pauni 152.8m) na Rashford (Pauni 136.6m).
Mchezaji wa United Bruno Fernandes (£ 132.4m) ni wa tano kwenye orodha hiyo.
Mason Mount, mwenye umri wa miaka 22, ndiye mchezaji wa 10 aliye na bei ya juu kwa Pauni 106.1m.
CIES hutumia vigezo mbali mbali pamoja na umri wa mchezaji, maonyesho, thamani ya kiuchumi ya kilabu yao na mfumko wa bei kufanya makadirio ya thamani ya uhamisho

Chanzo cha picha, Getty Images
Afisa Mkuu mtendaji wa Paris St-Germain Nasser Al-Khelaifi anasema mabingwa hao wa Ufaransa hawatamuuza mshambuliaji wao Kylian Mbappe, 22. (AS - in Spanish)
Aston Villa wako tayari kumnunua kiungo wa kati wa Southampton na England James Ward-Prowse, 26, siku moja baada ya kukubali kuvunja rekodi ya usajili wa klabu hiyo kumsaini kiungo wa kati mwenzake Emiliano Buendia kutoka Norwich. (Guardian)
Itagharimu euro milioni 200 sawa na (paundi milioni 171.8) kumnunua mshambuliaji wa Norway Erling Braut Haaland, 20, kutoka Borussia Dortmund msimu huu. (AS - in Spanish)

Chanzo cha picha, Getty Images
Wolves wnajiandaa kupokea ofa ya Arsenal wiki hii kuhusiana na kiungo wa kati wa Ureno Ruben Neves, 24. (Mail)
Barcelona wamefufua tena mpango wa kumsaka mlinzi wa Manchester City Mhispani Aymeric Laporte, 27, na huenda wakamtoa Sergi Roberto, 29, kama sehemu ya kufanikisha mkataba. (Sport - in Spanish)
Mshambuliaji wa Ufaransa Olivier Giroud, 34, bado huenda akajiunga na AC Milan, licha ya Chelsea kutangaza mpango wa kumuongezea mkataba wa mwaka mmoja wiki iliopita. (Goal)

Chanzo cha picha, Getty Images
Barcelona wameamua kutoongeza ofa ya Georginio Wijnaldum, 30, baada ya Paris St-Germain kuongeza mara mbili marupurupu ya ofa iliyotolewa na Barca. Kiungo huyo wa kati wa Uholanzi, ambaye yuko huru kuondoka Liverpool,anajiandaa kusaini mkataba wa miaka mitatu na PSG. (Fabrizio Romano, Twitter)
Juventus huenda wakajaribu hatua sawa na hiyo na mchezaji mwingine wa anayelengwa na Barcelona, mshambuliaji wa Uholanzi Memphis Depay, 27, ambaye anajiandaa kuondoka Lyon kwa uhamisho wa bure. (Mundo Deportivo)

Chanzo cha picha, Getty Images
Real Betis wamepiga hatua katika mazungumzo yao na mlinzi wa Paraguay Fabian Balbuena, 29, ambaye mkataba wake katika klabu ya West Ham inaelekea kumalizika. (Mundo Deportivo - in Spanish)
Tottenham itathibitisha uteuzi wa mkufunzi wa zamani wa Juventus Fabio Paratici msimu huu, baada ya juhudi zao za kumpata mkufunzi wa zamani wa-Juve na Inter Milan Antonio Conte kugonga mwamba. (Mirror)

Chanzo cha picha, Getty Images
Lazio huenda wakamsajili meneja wa zamani wa Juventus na Chelsea Maurizio Sarri, 62, kama mkufunzi wao mpya wiki hii. (Corriere dello Sport - in Italian)














