Wafahamu wachezaji wa soka waliocheka na wavu mara nyingi zaidi msimu huu duniani

Chanzo cha picha, Reuters
Klabu kuu tano za Ulaya ziinajivunia kuwa na washambuliaji hodari zaidi duniani.
Washambuliaji hawa wameendelea kuonesha mchezo wa hali ya juu katika ligi kuu za nyumbani na kuwa viungo muhimu katika klabu zao.
Lakini je washambuliaji 10 bora duniani kufikia sasa ni kina nani?
Orodha ofuatayo inajumuisha wafungaji mabao pekee na wala sio washambulizi.
Wachezaji kama Lionel Messi na Marcus Rashford hawakujumuishwa katika orodha ya washambulizi 10 bora .
Washambuiaji waliorodheshwa kwa vigezo vifuatavyo vilivyotumiwa kuwalinganisha
- -Mabao yaliyofungwa
- -Mabao katika kila mchezo
- -Mabao ndani ya dakika 90
- -Mchango wao kwa ujumla (usaidizi wa magoli)
Umuhimu wa mchezaji kwa klabu
10. Andre Silva (Eintracht Frankfurt)

- Msimu wa 2020/21:
- Alicheza mechi 34
- Alifunga magoli 30
- Alisaidia katika ufungajiwa mabao 5
- Alifunga mabao 0.88 katika kila mechi
- Alifunga magoli 0.94 ndani ya dakika 90
Baada ya msimu mbaya akiichezea AC Milan, Kiungo huyo wa Ureno amekuwa makini sana msimu huu.
Mshambuliaji huyo ameifungia Frankfurt
mabao 28 na kusaidia ufungaji wa mabao 5 katika mechi 32 za ligi msimu huu
9. Ciro Immobile (Lazio)
Msimu 2020/21:
Amecheza mechi 47
Alifanikiwa kufunga magoli 27
Alitoa usaidizi wa magoli 8
Alifunga mabao 0.57 katika kila mchezo
Alifunga mabao 0.66 ndani ya dakika 90
UEFA Champions League.
8. Karim Benzema (Real Madrid)
- Msimu 2020/21:
- Ameshiriki katika mechi 45
- Akafanikiwa kucheka na wav umara 30
- Alitoa usaidizi wa magoli 9
- Alifunga magoli 0.66 katika kila mchezo
- Alifunga mabao 0.72 ndani ya dakika 90
Karim Benzema amekuwa kiungo muhimu katika safu ya mashambulizi ya Real Madrid tangu Cristiano Ronaldo alipoondoka
Mshambuliaji huyo wa Ufaransa aliiongoza Real Madrid kushika nafasi ya pili katika La Liga.
7. Kylian Mbappe (Paris Saint-Germain)

Chanzo cha picha, Getty Images
Msimu 2020/21:
- Alicheza mechi 58
- Alicheka na wavu mara 48
- Alitoa usaidizi wa magoli 11
- Alifunga mabao 0.83 katika kila mechi
- Alifunga mabao 1.15 ndani ya dakika 90
Kasi na uwezo wake kuchenga umempatia Kylian Mbappe aliye na umri wa miaka 22 sifa na kuwatia imetia kiwewe walinzi wa timu zote duniani.
6. Cristiano Ronaldo (Juventus)

Chanzo cha picha, Reuters
- Msimu wa 2020/21
- Ameshiriki katika mechi 55
- Alifunga magoli 41
- Alitoa usaidizi wa mabao 5
- Alifunga magoli 0.75 kwa kila mechi
- Alifunga magoli 1.15 kwa kila dakika 90
Cristiano Ronaldo ni mmoja ya washambuliaji hodari zaidi duniani. Gumzo limeibuka kuhusu kushuka kwa kiwango cha mchezo wake lakini hata hivyo amefunga mabao 41 katika mechi 55 za msimu wa 2020/21.
5. Luis Suarez (Atletico Madrid)
- Msimu 2020/21:
- Ameshiriki mechi 38
- Alifunga magoli 21
- Alitoa usaidizi wa magoli 3
- Alifunga magoli 0.55 kwa kila mechi
- Alifunga magoli kwa kila dakika 90
Barcelona ilimuuza Luis Suarez kwa Atletico Madrid
kwasababu ilihisi kiwango cha uchezaji wake kimeshuka lakini nyota huyo anasalia kuwa kiungo muhimu kwa Atletico Madrid kushinda taji la La Liga
4. Romelu Lukaku (Inter Milan)

Chanzo cha picha, BBC/Twitter
- Msimu 2020/21:
- Ameshiriki mechi 53
- Alifunga magoli 39
- Ametoa usaidizi wa magoli 12
- Alifunga magoli 0.71 kwa mechi
- Alifunga magoli 0.87 kwa kila dakika 90
Inter Milan kwa mara ya kwanza wameshinda taji la Serie A ndani ya miaka 11.
Mshambuliaji huyo wa Ubelgiji alifunga mabao 23 katika msimu wake wa kwanza nchini Italia. Ushirikiano wake na Lautaro Martinez, umeisaidia sana klabu yake kupata ufanisi.
3. Erling Haaland (Borussia Dortmund)
- Msimu 2020/21:
- Ameshirika Mechi 52 msimu huu
- Amefanikiwa kufunga mabao 49
- Alitoa usaidizi wa magoli 9
- Alifunga magoli 0.94 kwa kila mechi
- Alifunga magoli 1.2 kwa kila dakika 90
Erling Haaland ambaye ni mchezaji nyota na raia wa Norway amekuwa akisakwa na karibu klabu zote kubwa.
Haaland, akiendelea kujiimarisha anapigiwa upatu kuwa mmoja wa washambuliaji mahahiri duniani.
2. Harry Kane (Tottenham Hotspur)
- Msimu 2020/21:
- Ameshiriki mechi 54
- Amefunga magoli 30
- Ametoa usaidizi wa magoli 18
- Amefunga magoli 0.55 kwa kila mechi
- Amefunga magoli 0.67 kwa kila dakika 90
Mshambuliaji huyu wa Tottenham ameshikilia nafasi hii kwa muda mrefu katika historia ya kandanda. Ameisaidia klabu yake kumaliza Ligi Kuu ya Premia katika nafasi ya kuheshimika baada ya kufunga mabao 30 na kusaidia ufungaji wa mabao 18.
1. Robert Lewandowski (Bayern Munich)

- Msimu 2020/21
- Ameshiriki mechi 47
- Amefunga magoli 53
- Ametoa usaidizi wa magoli 9
- Amefunga magoli 1.28 kwa kila mechi
- Amefunga magoli 1.35 kwa kila dakika 90
Robert Lewandowski ambaye ni mshambuliaji wa Poland ameiongoza Bayern Munich kunyakua taji la Bundesliga baada ya kufunga mabao 53 katika mechi 47.
Kwa sasa ndiye mshambuliaji bora zaidi duniani na ndio sababu anaongoza orodha hii ya washambuliaji 10 bora duniani.












