Tetesi za soka Alhamisi:Man Utd yammezea mate Murillo

Murillo

Chanzo cha picha, Getty Images

Muda wa kusoma: Dakika 3

Beki wa Nottingham Forest na Brazil, Murillo, mwenye umri wa miaka 23, ni mmoja wa mabeki kadhaa walio kwenye orodha fupi ya Manchester United ya wachezaji wanaoweza kusajiliwa msimu huu wa joto. (i paper)

Arsenal itafikiria ofa ya kumnunua beki wa Newcastle na Uingereza, Tino Livramento msimu huu wa joto, huku mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 23 bado hajaonesha nia ya kuongeza mkataba wake zaidi ya 2028. (Telegraph)

Tottenham Hotspur itamruhusu mlinda lango Antonin Kinsky, mwenye umri wa miaka 22, kuondoka klabuni hapo kwa mkopo msimu huu wa joto ili kujenga upya kujiamini kwake baada ya mchezaji huyo wa kimataifa wa Jamhuri ya Czech kuondolewa baada ya dakika 17 pekee dhidi ya Atletico Madrid siku ya Jumanne. (Telegraph)

Antonin Kinsky

Chanzo cha picha, Getty Images

Winga wa Manchester City na Ubelgiji, Jeremy Doku, mwenye umri wa miaka 23, atatafuta uhakikisho kuhusu mustakabali wake wa muda mrefu katika klabu ya Ligi Kuu huku Atletico Madrid ikimfuatilia. (Teamtalk)

West Ham ingependa kufanya usajili wa mkopo wa mlinzi wa Chelsea na Ufaransa Axel Disasi, 28, kuwa wa kudumu ikiwa watapata nafasi ya kusalia Ligi Kuu, lakini hawako tayari kufikia ada ya pauni milioni 38.8 ambayo Chelsea ililipa kwa ajili yake mwaka wa 2023. (Mail)

Aston Villa itachuana na Arsenal kupata saini ya kiungo wa Borussia Dortmund na Ujerumani Julian Brandt, 29, ambaye atakuwa mchezaji huru msimu huu wa joto. (Football Insider)

Julian Brandt

Chanzo cha picha, Getty Images

Juventus wako tayari kuongeza juhudi zao za kumtafuta mlinzi wa Bournemouth na Argentina Marcos Senesi, 28, ambaye mkataba wake unaisha mwishoni mwa msimu. (Gazzetta dello Sport)

Mshambuliaji wa Uholanzi Joshua Zirkzee, 24, anataka kuondoka Manchester United msimu huu wa joto baada ya klabu hiyo kumzuia kuondoka Januari. (Sun)

Liverpool na Arsenal wanaongoza mbio za kumsajili mlinzi wa Stuttgart na Ujerumani chini ya umri wa miaka 21 Finn Jeltsch, 19, huku Bayern Munich pia ikimtaka. (Teamtalk)

Kiungo wa kati wa Borussia Dortmund na Ujerumani Felix Nmecha, 25, atasaini mkataba mpya na klabu hiyo ya Bundesliga hadi 2030 licha ya kuvutiwa na Manchester United. (Florian Plettenberg)