Tetesi za Soka Ulaya Jumanne 31.12.12: Abraham, Pogba, Fernandes, Henry, Drinkwater, Nketiah

Tammy Abraham

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Mshambuliaji wa Chelsea, Tammy Abraham anataka kulilipwa - £180,000 kwa wiki - sawa na winga Callum Hudson-Odoi

Mazungumzo ya Chelsea kuhusu mkataba mpya wa mshambuliaji wa England Tammy Abraham yamekwama kwa sababu kiungo huyo wa miaka 22-anataka kulilipwa - £180,000 kwa wiki - sawa na winga Callum Hudson-Odoi, 19. (Goal)

Mkufunzi wa Liverpool Jurgen Klopp amekubali kumpoteza kiungo wa kati wa England Adam Lallana, 31, mwisho wa msimu huu. (Telegraph)

Kiungo wa kati wa Ufaransa Paul Pogba, 26, amekiri kuwa Manchester United haitamuuza mwezi Januari. (Sky Sports, via Metro)

Paul Pogba

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha, Paul Pogba, 26, amethibitisha kuwa Manchester United haitamuuza mwezi Januari

Beki wa Argentina Marcos Rojo, 29, anajiandaa kuondoka Manchester United mwezi Januari wakati wa dirisha la uhamisho wa wachezaji litakapofunguliwa. (Manchester Evening News)

Thierry Henry atakuwa mmoja wa watakaowania nafasi ya ukufunzi wa Barcelona ikiwa mkufunzi wa sasa Ernesto Valverde ataondoka klabu hiyo mwaka 2020. (Sport - in Spanish)

Mkufunzi mpya wa Arsenal Mikel Arteta anakabiliwa na kibarua kigumu kumshawishi mshambuliaji wa Gabon Pierre-Emerick Aubameyang, 30, kusalia katika klabu hiyo badaa ya msimu huu utakapokamilia. (Telegraph)

Pierre-Emerick Aubameyang

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Arsenal inakabiliwa na kibarua kigumu kumshawishi mshambuliaji wa Gabon Pierre-Emerick Aubameyang asiondoke katika klabu hiyo

Everton wanaongoza kinyang'anyiro cha usajili wa winga wa Colombia James Rodriguez, 28, kutoka Real Madrid. (El Desmarque - in Spanish)

Fiorentina inataka kumsaini mshambuliaji wa Wolverhampton na Italia Patrick Cutrone, 21, kwa mkopo hadi mwisho wa msimu. (Gazzetta dello Sport - in Italian)

Aston Villa inataka kumsajili kiungo wakati wa Chelsea Danny Drinkwater, 29, kwa mkopo mwezi Januari January. Mchezaji huyo wa England kwa sasa yuko Burnley kwa mkopo. (Sky Sports)

Danny Drinkwater

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Aston Villa inataka kumsajili kiungo wakati wa Chelsea Danny Drinkwater (kushoto) ambaye yuko Burnley kwa mkopo

Liverpool inamfutilia winga wa Vitesse Arnhem, Max Clark. Kiungo huyo wa miaka 23-ameiwakilisha England katika soka ya wachezaji wa chini ya miaka 16 na 17. (Mirror)

Arsenal itamrudisha nyumbani mshambuliaji wa England wa chini ya miaka-21 Eddie Nketiah, 20, kutoka Leeds ambako amekuwa akicheza kwa mkopo mwezi Januari. (Yorkshire Evening Post)

Eddie Nketiah

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Eddie Nketiah aliichezea Arsenal katika mechi ya kirafiki ya hivi karibuni dhidi Barcelona uwanjani Nou Camp

Inter Miami ambayo inamilikiwa na David Beckham na ambayo itaungana na MLS mwaka 2020 imemteua Diego Alonso kama mkufunzi wa kwanza wa klabu hiyo. (Inter Miami)

Real Madrid inapania kumrudisha nyumbani beki wa Uhispania Jesus Vallejo, 22, kutoka Wolves mwezi Januari kwa sababu ya kukosa muda wa kucheza. (AS - in Spanish)