Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Rwanda yazindua magari yanayotumia umeme rafiki kwa mazingira
Rwanda ikishirikiana Kampuni ya Volkswagen na Siemens imezindua magari ya kwanza ya umeme nchini humo yatakayokuwa rafiki kwa mazingira .
Mradi huo ulioanza na magari 50 ambayo yametengenezwa kwa ajili ya majaribio yatakuwa yakitumiwa kama magari ya uchukuzi wa abiria jijini Kigali na kwingineko nchini.
Mkurugenzi mkuu wa Volkswagen Group ya Afrika kusini, Thomas Schäfer amebainisha kuwa magari haya yamo bado katika majaribio na kwamba yametengenezwa 40 aina ya e.Golf. na kwamba malengo kwanza si kuuzwa na kwamba ni ghali ingawa bei bado kutangazwa.
''Magari haya hayana mpango kuuzwa kwa wateja kwa sasa.Tunalenga kwanza kuyafanyia majaribio na kujua yanafanya kazi vipi na ndipo tutakapowajulisha iwapo zitauzwa au la.Magari haya ni ghali ikilinganishwa na yale ya kawaida,kutokana na betri yake kwani betri peke yake ina gharimu kiasi cha dola 8000 za Kimarekani,lakini umeme ukilinganishwa na mafuta ni bei nafuu. Lakini iwapo serikali ikiwasaidia kwa kuweka sera mfano kwa kupata faida nafuu ,yamkini hali ikawa nzuri zaidi.Angalia Uchina serikali iliazimia kwamba asilimia magari 25 ya magari yanayouzwa yawe yanayotumia umeme.''
Serge Iyakoze ni kiongozi wa madereva wa kampuni ya Valkswagen akihusika pia kutoa warsha kwa madereva wenza katika matumizi ta teknolojia ya magari hayo ambaye ameiambia BBC kuhusu wasi wasi ama hofu kuhusu mwendo kimya wa magari hayo na iwapo hawatarajii kusababisha ajali za barabarani kwa watu waliozoea milio na honi za magari kuwashtua wanaotembea kwa miguu.
''Unapoelekea kupata ajali kawaida huna budi kupiga honi kwani dereva ana uwezo kuangalia kwa upana mkubwa mbele yake,kwa muda mfupi.Dereva anaangalia huwa na hisia za kujua kinachoelekea kutokea kwa wakati mfupi.Unapomuona mtu akizubaa unaweza kumpigia honi.Lakini huwezi kwenda ukipiga honi ovyo ovyo,kwani hata mpita njia anao uwezo kuona gari,na unawezas pia kumwashia mataa.''
Kampuni imeeleza kuwa inalenga kupanua wigo wa kazi zake katika mataifa mengi ya Afrika .Baada ya Rwanda Ghana ndiyo inatarajia kufuata na hatimae kwingineko.
Wakati mataifa ya Ulaya yanalenga kufikia mwaka 2030 kuwa yamekwisha achana na magari yanayotumia mafuta, Afrika ndiyo imeanza safari ambayo hatima yake haijawa wazi ila waliozungumza na BBC wameelezea kuwa hatimae wao pia watafika.