Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Kwa nini sungura huenda wakafumbua fumbo la chanzo cha kufika kilele wakati wa tendo la ndoa
Kwa nini wanawake wanafikia kilele wakati wa tendo la ndoa , iwapo kilele hicho hakihusiki katika uzazi?
Ni mabadiliko makubwa ya kisiri.
Mwanamume anapofika kilele wakati wa tendo la ndoa, kilele hicho uhusishwa na kutoka kwa mbegu za kiume, lakini kwa mwanamke kuhisi raha na kufikia kilele kuonaonekana kana kwamba hakutimizi lengo lolote.
Kuna nadharia nyingi kuhusu chanzo cha sababu ya wanawake kufika kilele.
Sababu mojawapo , kwa mfano inasema kwamba kupanuka ama kupungua kunakosababishwa na kufika kilele kunasaidia kufyonza mbegu za kiume na kuzisafirisha ndani zaidi hatua ambayo inasaidia kuimarisha uwezekano wa ujauzito.
Sababu nyengine inasema kwamba kufika kilele wakati wa tendo la ngono kunaleta uhusiano mzuri miongoni mwa wapenzi.
Kundi moja la wanasayansi nchini Marekani limezua sababu nyengine , na inahusisha maumbile ya sungura.
Visa vya utaratibu wa mabadiliko
Mtu kufikia kilele ni swala la neva na gumu kuwa ajali katika mabadiliko ya mwanadamu, kulingana na kundi la utafiti uliochapishwa katika Jarida la Chuo cha Sayansi cha Marekani, Utaratibu wa Chuo cha kitaifa cha Sayansi.
Nadharia mpya ni kwamba kufika kilele kunatokana na matokeo ya utaratibu wa mabadiliko ya mwanadamu kwa lengo la kuchochea mwanamke kuwa tayari kushika ujauzito.
Wanawake hufikia kipindi cha kuweza kushika ujauzito wakati wa mzunguko wote wa hedhi, iwapo watashiriki ngono au la.
Lakini katika kesi ya spishi zingine, kama vile sungura na paka, ni shughuli za ngono ambazo husababisha wao kufikia kipindi cha kuwa tayari kushika ujauzito kwa jina CIO kwa lugha ya Kiingereza.
Hatua hiyo inajulikana kama utayari uliochochewa na ngono.
Wanasayansi wanasema kwamba kilele kinachofikiwa na wanawake wakati wa tendo la ngono ni kifungu cha mifumo ya kisaikolojia iliyoandaliwa ili kuchochea wanawake kuwa tayari kushika ujauzito wakati wa tendo la ndoa
''Tunajua kwamba kuna taswira miongoni mwa sungura''. Swali ni iwapo taswira kama hio ilipoteza kazi zake miongoni mwa wanadamu, alisema Mihaela Pavlicev, mwanzilishi mwenza wa utafiti huo.
Vipimo na sungura
Wagner na Pavlicev wanadai kwamba tendo la CIO miongoni mwa sungura na kufikia kielele miongoni mwa wanawake ya vyanzo sawa.
Na kuthibitisha hilo, Pavlicev na wenzake waliwafanyia sungura wa kike vipimo.
Katika mojawapo ya vipimo hivyo wanasayansi waliwapatia wanyama hao dawa za kuzuia kufikia kwa kilele miongoni mwao wanawake.
Iwapo dawa hiyo ina athari kama hiyo miongoni mwa wanadamu , itaathiri wanawake kufikia wakati wao wa kuwa tayari kushika ujauzito, wanasema watafiti.
Kwa sungura waliopatiwa dawa hiyo wakati wao wa kuwa tayari kushika mimba ulipungua kwa asilimia 30.
Kwa nini athari yao haikuwa kubwa? Utafiti unaonyesha kwamba sungura hutumia dawa hiyo vizuri ikilinganishwa na wanawake.
Wanasayansi wengine ambao hawakushiriki katika utafiti huo walisema kwamba kupungua kwa hali ya sungura kuwa tayari kushika mimba hakutoshi kuthibitisha CIO na kufika kilele miongoni mwa wanawake vina vyanzo sawa.
Hatua nyengine kulingana na Wagner, ni kurejelea vipimo na spishi nyengine ambapo tendo la ngono husababisha kuwa tayari kushika ujauzito.