Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Tetesi za Soka Ulaya Jumatano 18.09.2019: Sancho, Lloris, Guardiola, Wilson, Isco
Manchester United inajitayarisha kumnyatia mshambuliaji wa Bournemouth mwenye umri wa miaka 27 Callum Wilson, aliyefunga mabao matatu katika mechi mbili zilizopita. (Sun)
Real Madrid, Barcelona na Liverpool wanataka kumsajili mchezaji wa kiungo cha kati wa Napoli Fabian Ruiz, mwenye umri wa miaka 23. (Mail)
Manchester United imeulizia kuhusu kumsajili winga wa Borussia Dortmund mwenye umri wa miaka 19 mchezaji wa timu ya taifa ya England Jadon Sancho wakati wa majira ya joto (Kupitia sport Football - kupitia Manchester Evening News)
Aliyekuwa mlinzi wa Manchester United na timu ya taifa ya Ufaransa Patrice Evra, mwenye umri wa miaka 38, anasema wachezaji waliopo sasa wa juu Old Trafford wanahitaji kujitolea pakubwa kwa klabu hiyo kabla ya kukubalika na mashabiki. (Sky Sports)
Mchezaji wa Real Madrid mwenye umri wa miaka 27 anayeichezea timu ya taifa ya Uhispania Isco, na anayezivutia Manchester City na Liverpool, anasakwa na Juventus, ambayo inatayarisha kitita cha £66m kuwasilisha ombi la mshambuliaji huyo wa zamani wa Malaga. (Sun)
Kipa wa Tottenham na timu ya tifa ya Ufaransa Hugo Lloris, mwenye umri wa miaka 32, anasema huenda akastaafu katika klabu hiyo na ana hamu ya kucheza katika soka ya ligi kuu kabla ya kustaafu. (France Football)
Meneja wa Manchester City Pep Guardiola anakosa kuwasajili wachezaji wakubwa aliowalenga kwasbabu anakataa kulipa kiwango ambacho hudhaniwa huenda kikwavutia wanunuzi. (Guardian)
Winga wa Manchester United na timu ya taifa ya Wales Daniel James, aliye na miaka 21, anasema nusra aachane na soka kabisa wakati akiwa na miaka 12. (Inside United, kupitia Mirror)
Mzozo kuhusu uhamisho wa mshambuliaji wa timu ya taifa ya Ufaransa mwenye miaka 28 - Antoine Griezmann wenye thamani ya £107 kutoka Atletico Madrid kwenda Barcelona huenda ukachangia klabu hiyo ya Catalan kuishia kucheza mechi kwa faragha pasi kuwa na mashabiki. (Goal.com)
Winga wa Barcelona mwenye umri wa miaka 16 wa timu ya taifa ya Guinea-Bissau, Ansu Fati anakaribia kukamilisha makubaliano ya mkataba mpya wa miaka mitano baad aya kufunga mabao mawili katika mechi tatu alizoshiriki kwenye ligi ya Uhispania La Liga. (AS)
Mchezaji wa kiungo cha kati wa timu ya taifa ya Brazil Philippe Coutinho, mwenye umri wa miaka 27, anasema Bayern Munich - ambako anacheza kwa mkopo kutoka Barcelona - ni 'kama familia' kuliko Barca nailiyokuwa klabu yake Liverpool. (Liverpool Echo)
Aliyekuwa mshambuliaji wa Manchester United na timu ya taifa ya England Wayne Rooney, aliye na miaka 33 - na sasa anayeichezea timu ya DC United - anasema wachezaji wa MLS wanastahili kulipwa zaidi. (ESPN)
Mkurugenzi wa michezo wa Norwich City Stuart Webber amekubali mkataba mpya wa miaka mitatu. (Telegraph)
Tetesi za soka Jumanne
Klabu ya Celtic ya Uskochi inaweza kujaribu kumsajili kiungo wa klabu ya Tottenham na Kenya Victor Wanyama, 28, mwezi Januari, kwa mujibu wa kocha wa klabu hiyo Neil Lennon. Wanyama aliwika na Celtic kabla ya kutimkia England, na sasa kocha wa Tottenham ameshaeleza kuwa hana haja naye. (Team Talk)
Winga wa Chelsea na Brazil Willian anataka kusalia kwenye uga wa Stamford Bridge, lakini klabu hiyo hata hivyo bado haijampatia nyota huyo mwenye miaka 32 mkataba mpya. (Express)
Beki wa Ajax na Uholanzi Joel Veltman, 27, amebainisha kuwa alitaka kujiunga na klabu ya West Ham United ya England katika dirisha la usajili lililopita lakini mabingwa hao wa Uholanzi hawakumruhusu kuindoka. (NOS)
Meneja wa Manchester United Ole Gunnar Solskjaer ataendelea na mipango ya kusajili wachezaji kutoka Uingereza msimu ujao wa dirisha la usajili la majira ya joto.
Wachezaji ambao wapo kwenye rada ya Solskjaer ni mshambuliaji kinda wa England na klabu ya Borussia Dortmund Sancho, 19, na kiungo wa Leicester City na England James Maddison 22. (ESPN)
Miamba ya soka ya Italia, vilabu vya AC Milan, Inter Milan, Juventus na Borussia Dortmund zote zipo kwenye mipango ya kutaka kumsajili kiungo wa Manchester United Nemanja Matic, 31, pale mkataba wa mchezaji huyo wa kimataiifa wa Serbia utakapofikia tamati mwishoni mwa msimu huu. (Calcio Mercato)
Liverpool walipanga kumsajili mlinzi wa kati wa Napoli na Senegal Kalidou Koulibaly iwapo mipango yao ya kumsajili beki kisiki wa Uholanzi Virgil van Dijk, ingegonga mwamba mwezi Januari 2018. (Goal)
Bournemouth wanajiandaa kumpatia Ryan Fraser,25, mkataba mpya wa mshahara wa thamani ya pauni 100,000 kwa wiki. Tayari vilabu vya Arsenal, Everton, Chelsea NA Wolves vyote vinamnyemelea winga huyo raia wa Uskochi. (90min.com)
Bournemouth pia wanaweza kumpoteza mshambuliaji wao Callum Wilson, 27, anayenyemelewa na Manchester United.(ESPN)
Beki wa klabu ya Watford na Ubelgiji Christian Kabasele, 28, amebainisha kuwa anakaribia kusaini mkatabampa na klabu yake. (Sport Witness)
Everton, Southampton, Bournemouth, Sheffield United, Bristol City, Barnsley na Sunderland wote wanamfuatilia kwa makini winga kinda wa klabu ya Motherwell ya Uskochi James Scott, 19. (Team Talk)