Tetesi za Soka Ijumaa 05.07.2019: Maguire, Fernandes, Niguez, Marcelo, Lukaku, Gomez

Mchezaji Bruno Fernandes ameanza mchakato wa kuhamia Old Trafford. Nyota huyo wa miaka 24 anayecheza safu ya kati ya Sporting Lisbon na Ureno anatarajiwa kwenda Manchester kufanya vipimo vya afya. (Sport Witness)

Red Devils wanamlenga mlinzi wa Atletico Madrid na Uhispania Saul Niguez, 24, kuchukua nafasi ya Paul Pogba, endapo nyota huyo wa miaka 26 raia wa Ufaransa ataondoka Old Trafford. (Express)

Manchester City hawako tayari kulipa pesa zinazoitishwa na Leicester kumnunua Harry Maguire,26, hatua ambayo imeipatia Manchester United nafasi ya kumsajili mchezaji huyo wa Kimataifa wa England. (90Min)

Arsenal watamkosa kipa wa Ujerumani wa miaka 21 Markus Schubert, ambaye ameamua kujiunga na Schalke kutoka Dynamo Dresden. (Sport1)

Arsenal pia wako mbioni kumsajili Marcelo baada ya beki huyo Mbrazil kuomba kuondoka Real Madrid. (Sport - via Metro)

Inter Milan wanachelewa kutoa ombi rasmi la kumnunua mshambuliaji wa Manchester United na Ubelgiji Romelu Lukaku, 26. (Sun)

Mchezaji nyota wa zamani wa Tottenham Ossie Ardiles anasema ni "kazi bure" kwa klabu hiyo kujaribu kumzuia Christian Eriksen, 27 asiondoke. (Talksport - via Goal)

West Ham United wanajaribu kunyakua uhamisho wa mshambuliaji wa Celta Vigo na Uruguay Maxi Gomez, 22, kutoka kwa Valencia. (Sky Italia - via Inside Futbol)

Leicester wataelekeza nguvu zao zote kumsaini beki wa Burnley James Tarkowski endapo Harry Maguire ataenda klabu ya Man United. Hata hivyo, Leicester wataminyana na Wolves katika harakati za kutaka kumsajili Tarkowski. (Birmingham City)

Man United inajiandaa kumpatia mkataba mpya wenye thamani ya pauni milioni 85 kipa wao Mhispania David de Gea ambapo atapokea kitita cha pauni 350,000 kwa wiki. (Star)

Tetesi Bora Alhamisi

Frank Lampard amepigwa picha katika uwanja wa Stamford Bridge alipokaribia kuwa kocha mpya wa Chelsea. (Mail)

Kuidhinishwa kwa Lampard kuwa kocha mpya wa Chelsea kulicheleweshwa Jumatano jioni baada ya mitandao ya kijamii ya Facebook na Instagram kukumbwa na changamoto za kiufundi hali ambayo ilifanya kuwa vigumu kuchapisha picha au kuweka video mtandaoni. (Mirror)

Chelsea pia imeanza mazungumzo ya kandarasi mpya ya na kiungo wa kati wa miaka 20 Mason Mount, ambaye aliichezea Derby msimu uliopita chini ya ukufunzi wa Lampard. (Evening Standard)

Arsenal wamepewa nafasi ya kumsaini mshambuliaji wa Barcelona Mbrazil Malcom, 22, lakini azma yao kubwa ni kumnasa mshambuliaji wa Ivory Cost wa miaka 26, Wilfred Zaha kutoka Crystal Palace. (Mirror)

Gunners wana pauni milioni 70 wanapojianda kuweka dau la pili la kumnunua Zaha, japo kuwa Palace wanamini thamani ya mshambuliji huyo ni pauni milioni 80(Sky Sports)

Agenti wa Romelu Lukaku amaefanya mazungumza mapya na Inter Milan lakini klabu hiyo ya Italia bado inashauriana na Manchester United kuhusu ada ya kiungo huyo wa Ubelgiji aliye na miaka 26. (Sky Sport Italia - in Italian)

Manchester United wanataka kumsajili mchezaji wa safu ya kati wa Ureno Bruno Fernandes, 24 kutoka Sporting Lisbon. (Sky Sports)

Tottenham imesitisha mazungumzo yake na Real Betis kumhusu kiungo ya kati wa Argentina Giovani Lo Celso, 24, baada ya vilabu kushindwa kuafikiana malipo. (Sky Sports)