Manchester City 1-0 Leicester: Vincent Kompany afunga bao la 'kipekee'

Vincent Kompany

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha, Nahodha Vincent Kompany alifunga goli lake la kwanza la msimu dhidi ya Leicester
    • Author, Chris Bevan
    • Nafasi, BBC Sport at Etihad Stadium

Manchester City wanajua watalihifadhi taji la ligi kuu nchini Uingereza iwapo watashinda mechi ya siku ya mwisho baada ya Vincent Kompany kupiga mkwaju kutoka mbali ambao kipa wa Leicester City hakuuona.

Huku zikiwa zimesalia dakika 20 , timu zote zilikua hazijaona lango la mwengine katika uwanja wa Etihad huku mabingwa hao watetezi wakihitaji msukumo katika mechi ambayo ushindi pekee utawahakikishia wanapanda juu ya Liverpool katika kilele cha jedwali la ligi.

Hatahivyo walipata bao lao la pekee kutoka kwa mtu ambaye hawakumtarajia ambaye alipiga mkwaju kutoka maguu 25-kipa wa Leicester City hakuutarajia.

Ushindi huu wa City unamaanisha kwamba wanapanda hadi juu ya jedwali na kuipiku Liverpool kwa uongozi wa pointi moja huku wakijiandaa kucheza mechi yao ya mwisho siku ya Jumapili , wakati Pep Guardiola ataelekea Brighton huku Liverpool ikicheza dhidi ya Wolveharmpton.

Baada ya kujikwamua kupata ushindi mwembamba nyumbani , sio rahisi kwamba City watalegeza kamba huku shindano hilo la kutafuta mshindi wa ligi likifikia kilele chake.

Gundogan akikabiliana na Magwire

Chanzo cha picha, Getty Images

Uongozi wa jedwali la ligi sasa umebadilika mara 32 msimu huu.

Lakini kwa kipindi cha mda mrefu ilionekana wazi kwamba Liverpool itasalia katika kilele hadi wikendi.

Ikifunzwa na aliyekuwa mkufunzi wa Liverpool Brendan Rodgers , ambaye alikaribia kushinda taji hilo katika uwnaja wa Anfield 2014, safu ya ulinzi ya Leicester ilikuwa ngumu kupasuka huku wakitishia katika safu ya mashambulizi.

Walikizuia kikosi cha Guardiola ambacho kimezoea kucheza mchezo wa kumwagika nafasi nyingi , huku kichwa cha Sergio Aguero kikipina mwamba wa goli.

Kuchanganyikiwa kwa City nje na ndani ya uwanja kuliendelea baada ya kipindi cha kwanza , hadi pale nahodha Vincent Compaby akipofunga goli lake la kwanza msimu huu na la 158 la City.

Mkufunzi wa Man City Pep Guardiola alivyoona mambo magumu katika mechi hiyo

Leicester ilitishia kuharibu sherehe hiyo katika dakika za mwisho wakati mshambuliaji wa zamani wa City Kelechi Iheanacho alipopiga nje huku afueni ikionekana katika nyuso za madhabiki wa City na wachezaji wao.

ManCity inaendelea kufunga magoli nyumbani

Hakuna upungufu wowote wa mchezo mzuri ambao mashabikji wa Man City wamekuwa wakikosa.

Lakini hawajazoea hali ya wasiwasi kama ile walioiona siku ya Jumatatu , huku Leicester ikiwazuia kutofunga goli kwa muda mrefu ikilinagnishwa na timu nyangine yoyote ambayo imecheza katika uwanja wa Etihad .

Klabu nyengine iliowazuia kwa kipindi kirefu cha dakika 59 ni West Ham.

City ilikuwa ikitengeneza nafasi , wakikaribia kufunga kabla ya kipindi cha kwanza wakati kichwa cha Aguero kilipogonga mwamba kabla ya kupanguliwa na kipa Kasper Schmeichel, na baadye kipa huyo kumnyima bao la wazi mshambuliaji huyo wa Argentina.

Mchezaji bora wa mechi - Vincent Kompany (Man City)

Vincent Kompany

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Pep Guardiala amekiri kwamba hakudhania kwamba Vincent anaweza kuachilia kombora kama lile

Lipi la kusubiriwa?

Manchester City italihifadhi taji lake iwapo itaifunga Brighton katika uwanja wa Amex Stadium katika siku ya mwisho msimu , Jumapili 12, Mei huku Leicester ikiwaalika Chelsea