Huddersfield 1-1 Man Utd: Timu ya Solskjaer kucheza ligi ya Europa League baada ya sare ya Huddersfield

Mchezaji wa Huddersfield, Isaac Mbenza akishangilia bao la kusawazisha dhidi ya Manchester United

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Mchezaji wa Huddersfield, Isaac Mbenza akishangilia bao la kusawazisha dhidi ya Manchester United
Muda wa kusoma: Dakika 2

Manchester United hawana budi kucheza ligi ya Europa League msimu ujao baada ya Huddersfield kudidimiza nafasi yao ya kumaliza Ligi ya Premia katika nafasi ya nne.

Matokeo ya mechi ya leo ni muendelezo wa matokeo mabaya kwa United baada ya kushindwa katika mechi tano mfululizo.

Mara ya mwisho United walijipata katika hali hiyo ilikuwa kati ya mwezi Novemba na Disemba mwaka 2015 ambapo walicheza mechi nane bila kuandikisha ushindi chini ya mkufunzi Louis van Gaal.

Alexis Sanchez amefunga bao moja katika ligi ya Premier msimu huu

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha, Alexis Sanchez amefunga bao moja katika ligi ya Premier msimu huu

Matokea ya hivi punde ya mechi yao ya ligi kuu ya Uingereza inaamanisha vijana wa Ole Gunnar Solskjaer hawananafasi ya kufikia Chelsea au Tottenham na wana nafasi finyu ya kuiondoa Arsenal katika nafasi ya tano.

Ruka X ujumbe
Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)

Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue

Onyo: Imetoka kwingine na inaweza kuwa na matangazo

Mwisho wa X ujumbe

Alexis Sanchez pia huenda asiheze katika mechi ya mwisho ya Man U dhidi ya Cardiff katika uwanja wa Old Trafford, baada ya kujeruhiwa katika kipindi cha pili cha mechi ya Huddersfield.

Huddersfield amba wako chini kabisa katika jedwali la msimamo wa ligi wana alama 11 wanatarajiwa kuchuana na Southampton Jumapili ijayo.

Sanchez apewa nafasi adimu

Sanchez alipewa nafasi ya kuanza mechi kwa mara ya kwanza tangu tarehe mbili mwezi Machi baada washambuliaji wenzake Romelu Lukaku na Anthony Martial kuumia.

Mchezaji wa Machester United Scott McTominaya akishangialia bao lake dhidi ya Huddersfield

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Mchezaji wa Machester United Scott McTominaya akishangialia bao lake dhidi ya Huddersfield

Macho yote sasa yanamuangazia kiungo huyo raia wa Chile kabla ya mwisho wa msimu huu baada ya Solskjaer kuahidi kufanyia marekebisho makubwa kikosi chake.

Inasadikiwa kuwa mshahara wa Sanchez hausaidii United kushauriana kuhusu mkataba wa wachezaji kama David de Gea, Juan Mata na Ander Herrera.

De Gea, pia amekuwa akikosolewa vikali kutokana na utenda kazi wake katika mechi kadhaa zilizopita.