Europa League: Arsenal yailaza Valencia nayo Chelsea yapata sare ugenini dhidi ya Frankfurt

Chanzo cha picha, Reuters
Mshambuliaji wa Arsenal Alexandre Lacazette alofunga magoli mawili huku Sarsenal ikitoka nyuma katika uwanja wa Emirates na kuilaza valencia katika mechi ya mkodo wa kwanza ya nusu fainali ya Europa League.
Mouctar Diakhaby aliiweka mbele valencia kupitia kichwa kilichomuwacha bila Jibu Petr Cech kabla ya Lacazette kusawazisha kutoka kwa pasi iliotolewa na Pierre-Emerick Aubameyang.
Baadaye mshambuliaji huyo wa Ufaransa alifunga goli la pili kutoka kwa krosi iiliopigwa na Granit Xhaka dakika saba baadaye na kufanya mambo kuwa 7-1 kabla ya kipindi cha kwanza kukamilika.

Chanzo cha picha, Getty Images

Chanzo cha picha, Getty Images
Na goli la mwisho la Aubameyang katika dakika za lala salama ziliihakikishia ushindi Arsenal wa mabao mawili kabla ya mkondo wa pili wa mchuano huo utakaochezwa Uhispania.
Wakati huo huo Chelsea ilitoka sare ya 1-1 katika mechi nyengine ya nusu fainali ya Europa baada ya kiungo wa kati wa Chelsea Pedro kuipatia timu yake bao la Ugenini.

Chanzo cha picha, Getty Images
Eintracht Franfurt ilichukua uongozi kupitia mshambuliaji Luka Jovic ambaye alipata pasi nzuri kutoka kwa Filip Kostic.
The Blues ambao walianza na Eden hazard akiwa mchezaji wa ziada walisawazisha wakati Pedro alifunga goli zuri kabla ya kipindi cha kwanza kukamilika.
Beki David Luiz pia alikosa bao pale mkwaju wake wa adhabu uligonga mwamba wa goli.

Chanzo cha picha, Getty Images
Sare hiyo inamaanisha kwamba Chelsea itakuwa timu ya kwanza kucheza mechi 16 za Europa League bila kushindwa , ikivunja rekodi iliowekwa na Atletico Madrid kutoka 2011 hadi 2012.
Watakuwa na fursa ya kuimarisha rekodi hiyo hadi mechi 17 Alhamisi ijayo katika mkondo wa pili nchini Uingereza.
Katika mechi ya Arsenal Lacazette angejipatia hat-trick yake ya kwanza baaa ya kukosa bao la wazi kutoka maguu sita ya goli katika kipindi cha pili na baadaye akazuiliwa na kipa Neto katika visa viwili.
Arsenal sasa itaelekea Valencia kwa awamu ya pili siku ya Alhamisi wakitumai kuzuia kushindwa kwa nusu fainali yao ya pili baada ya kuondolewa na Ateltico madrid mwaka uliopita.












