Tetesi za Soka Ulaya Jumatatu 06.05.2019: Eriksen, Van de Beek, Higuain, Welbeck, Modric

Tottenham inajiandaa kucheza msimu ujao bila ya kiungo wa kimataifa wa Denmark kiungo Christian Eriksen, 27, na wanaelekea kumsajili kiungo wa Ajax Donny Van de Beek 22, ambaye pia anatakiwa na Real Madrid na Bayern Munich.(Mirror )
Meneja wa Chelsea Maurizio Sarri ameitaka klabu yake kumsajili moja kwa moja mshambuliaji Gonzalo Higuain ambaye anaichezea Chelsea kwa mkopo akitokea Juventus ili kuimarisha kikosi chake. (Goal.com)

Chanzo cha picha, Getty Images
Mchezaji wa kimataifa wa England Danny Welbeck, 28 hatopewa mkataba mpya na klabu yake ya Arsenal na ataondoka akiwa mchezaji huru katika dirisha lijalo. (Sky Sports)
Meneja wa Real Madrid Zinedine Zidane atamruhusu kiungo Luka Madric kuondoka. (AS)
Mchezaji wa kimataifa wa Venezuela Salomon Rondon, 29 ambaye anachezea Newcastle kwa mkopo amewaambia Magpies kutoangalia umri wake na kumnunua kwa sababu anafanana na mvinyo.(Mirror)
Winga wa Nice, Allan Saint-Maximin, 22, anayewaniwa na Arsenal na amefungua njia ya kujiunga na AC milan baada ya nafasi ya kujiunga na klabu hiyo mwezi januari kushindikana.

Meneja wa Blackburn Tony Mowbray amejiweka mbali na ripoti zinazozungumzwa kuhusu klabu yake kutaka kumsajili goli kipa wa zamani wa England Joe Hart, 32.
Mlinzi wa Chelsea Kurt Zouma ambaye anacheza kwa mkopo katika timu y a Everton anatarajiwa kurejea Stamford Bridge kuanza maandalizi ya msimu mpya ingawa The toffees wanataka kumsajili kwa mkataba wa kudumu .

Chanzo cha picha, Reuters
Nahodha wa Chelsea Gary Cahill, 33 na mchezaji wa zamani wa timu ya taifa ya England amemshambulia meneja wake Maurizio Sarri kwa kusema ameshindwa kumuonyesha heshima mchezaji huyo mkongwe wa Chelsea.
Klabu wa Celtic imetoa ofa kwa meneja wa zamani wa Manchester United Jose Mourinho, 56 kwa kumpa nafasi ya kuwa meneja wa klabu hiyo msimu ujao. (Sky Sports Italia, via Express)












