Tetesi za soka Ulaya Jumatano 03.04.2019: Bale, Varane, Courtois, Sancho, Pedro, Barella

Gareth Bale amesema kuwa hana mipango ya kuondoka Bernabeu

Chanzo cha picha, Getty Images

Mshambuliaji wa kati wa Real Gareth Bale amesema kuwa hana mipango ya kuondoka Bernabeu katika kipindi kijacho cha kuhama. Kumekuwa na taarifa kwamba mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 29-atahamia Tottenham na pia Manchester United. (Marca, via Inside Futbol)

Zinedine Zidane anasema haitaki Real bila Bale

Chanzo cha picha, Getty Images

Zidane hajaamua juu ya kuondoka kwa Bale na amesema kuwa hatma ya mchezaji huyo wa Wales katika Real Madrid itaamuliwa mwishoni mwa msimu. (Mirror)

Hata hivyo , Zidane amepuuzilia mbali taarifa kwamba mchezaji wa safu ya ulinzi Raphael Varane, mwenye umri wa miaka 25, anayelengwa na Manchester United, anaondoka Real Madrid, akisema : "Siitaki Madrid bila Varane," (Marca)

Manchester United wako tayari kumlipa pesa yoyote Jadon Sancho ili wamchukue

Chanzo cha picha, Getty Images

Wakati huo huo , Zidane amedokeza kuwa atamuuza golikipa wa zamani wa Chelsea Thibaut Courtois, mwenye umri wa miaka 26, msimu huu. (Mirror)

Manchester United wamemtaja winga wa Borussia Dortmund ya England Jadon Sancho kama mchezaji wanaemlenga kwa ajili ya kuijenga upya timu hiyo na wamejiandaa kulipa zaidi ya £100m kwa ajili ya kijana huyo mwenye umri wa miaka. (Independent)

Arsenal wametujma ujumbe wa lkumuangalia Cagliari Nicolo Barella

Chanzo cha picha, Getty Images

Inter Milan na AC Milan wote wanamfukuzia Winga wa Chelsea Muhispania Pedro, mwenye umri wa miaka 31. (Express)

Arsenal wametuma ujumbe wao kumuangalia mchezaji wa muda mrefu wa safu ya katikati wa Cagliari Nicolo Barella, mwenye umri wa miaka 22, katika mchezo wao dhidi ya Juventus. (Star)

Real Madrid imefichua picha za mpango wao wa ukarabati wa miaka minne wa uwanja wa Bernabeu.

Real Madrid na Juventus wamezipiku Manchester United na Manchester City wamo katika harakati za kusaini mkataba na kiungo wa kati wa Benfica Joao Felix, mwenye umri wa miaka 19. (Sun)

Sam Allardyce amethibitisha kuwa hawajafanya mawasiliano yoyote juu ya kazi ya kocha mkuu wa West Brom , licha ya kutajwa kuwa mtu anayependelewa kuchukua nafasi ya Darren Moore ambayo kwa sasa iko wazi - lakini Meneja huyo wa zamani wa England mwenye umri wa miaka 64-yuko tayari ikiwa West brom watamtaka. (Express and Star)

Sam Allardyce amethibitisha kuwa hajafanya mawasiliano yoyote juu ya kazi ya ukocha mkuu wa West Brom

Manchester United ni timu ya hivi karibuni kuonyesha kuwa wanamtaka mchezaji wa kiungo cha kati wa Leicester Mbelgiji Youri Tielmans, mwenye umri wa miaka 21, ambaye kwa sasa anacheza kwa deni kutoka Monaco. (HLN, via Leicester Mercury)

Cardiff wameomba kufany amkutano na Nantes kujaribu kutatua ugomvi mkubwa baina yao juu ya kuhama kwa Emiliano Sala. (Telegraph)

Mourinho amedokezea kuwa matatizo yake na Paul Pogba huenda yaliibuka wakati Pogba alipotaka kusafiri peke yake badala ya kusafiri katika basi pamoja na timu nzima

Chanzo cha picha, Getty Images

Mkurugenzi wa soka wa Everton Marcel Brands anasema kombe lazima lirejee katika kipindi hiki ambacho timu ina uongozi bora wa Marco Silva ambapo alipewa "muda" kuleta mafanikio kwa Goodison. (Liverpool Echo)

Meneja wa zamani wa Manchester United Jose Mourinho anaangalia timu ya tano ya nyumbani inayoweza kumchukua na ameacha mlango wazi kwa Bundesliga ikiwa watamtaka. (Daily Mail)

Mourinho amedokezea kuwa matatizo yake na Paul Pogba huenda yaliibuka wakati kulipokuwa na mzozo juu ya mchezaji huyo wa safu ya kati kutaka kusafiri peke yake badala ya kusafiri kwenye basi la timu na wachezaji wenzake. (Manchester Evening News)

Leicester imekuwa ikisemekana kuwa inataka kumchukua mchezaji wa kiungo cha kati wa Cardiff Victor Camarasa

Chanzo cha picha, Getty Images

Meneja wa Crystal Palace boss Roy Hodgson anapanga kuwa na Aaron Wan-Bissaka, mwenye umri wa miaka 21, na Wilfried Zaha, mwenye umri wa miaka 26, katika kikosi chake msimu ujao - lakini anasema kuwa kila mchezaji ana bei yake . (Evening Standard)

Leicester imekuwa ikisemekana kuwa inataka kumchukua mchezaji wa kiungo cha kati wa Cardiff Victor Camarasa, mwenye umri wa miaka 24, ambaye anacheza kwa deni kutoka Real Betis. (Leicester Mercury)

Chelsea wanaangalia uwezekano wa kumzawadiia mlinzi Reece James, mwenye umri wa miaka 19, kwa kucheza kwa deni katika Wigan kwa kumfanya kuwa sehemu ya kikosi chao kikuu msimu ujao.. (London Evening Standard)

Mshambuliaji wa zamani wa Newcastle Shola Ameobi anasema Rafa Benitez anaweza kuanza kuiga matokeo ya mafanikio katika Newcastle ya Sir Bobby Robson. (Newcastle Chronicle)

Kiungo wa kati wa Newcastle Sean Longstaff, mwenye umri wa miaka 21,ametajwa kama balozi wa klabu hiyo wa misaada kufuatia kufanya kwake vema kwenye msimu huu katika St James' Park. (Newcastle Chronicle)