Demba Ba, Arshavin, Michu na Adel Taarabt: ''Wachezaji wa kandanda ambao hawatasahaulika mitaani''

Chanzo cha picha, Gualter Fatia
- Author, Sam Harris
- Nafasi, BBC Sport
Je unamkumbuka mchezaji wa zamani wa Queens Park Rangers {QPR} Adel Taarabt?
Baada ya siku 1,387 ,mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 29 hatimaye alianza kuichezea klabu ya Benfica siku ya Jumamosi , takriban miaka minne baada ya kutia kandarasi ya kuichezea klabu hiyo ya Rs kutoka Ureno.
Taarabt alikuwa mchezaji mahiri kumtazama akiichezea QPR katika msimu wa 2010-11 katika ligi ya mabingwa.
Alitangazwa kuwa mchezaji bora wa ligi hiyo kabla ya QPR kupandishwa hadi katika ligi ya Premia, lakini maisha katika ligi hiyo hayakuisha vizuri kwa mchezaji huyo wa Morocco.
Baada ya kudaiwa kuwa mnene kupitia kiasi na mkufunzi Harry Rednapp 2012 na kuuzwa kwa mkopo , Taarabt alielekea Benfica 2015 baada ya kandarasi yake kufutiliwa mbali kupitia makubaliano.
Miaka minne baadaye , raia huyo wa Morrocco alipata umaarufu mkubwa mjini Lisbon baada ya watumiaji wa mtandao wa Twitter kuandika kwamba mitaa haitamsahau mchezaji huyo.

Chanzo cha picha, @james_monteithh
Ni chapisho ambalo lilisambazwa sana katika mtandao wa twitter.
Unampata mchezaji ambaye alionesha mchezo mzuri katika uchezaji wake, walichapisha baadhi ya picha na kusema kwamba mitaa haitasahau.
Kumekuwa na wachezaji tajika kama vile mchezaji wa Portsmouth Benjani na yule wa Blackburn Roque Santa Cruz waliopendwa.
Lakini hawa hapa baadhi ya wachezaji ambao wanahitaji kuona kwamba majina yao hayatasahauliki mitaani.
Demba Ba na Papiss Cisse

Chanzo cha picha, Getty Images
Mashabiki wa Newcastle United walifurahishwa na ushirikiano wa washambuliaji maarufu katika miaka iliopita: Andy Cole na Peter Beardsley, Alan Shearer na Les Ferdinand, na hata Obafemi Martins pamoja na Michael Owen .
Lakini kulikuwa na kitu tofauti kuhusu mshambuliaji wa Senegal Demba Ba na Papiss Cisse.
Wawili hao waliingia katika klabu hiyo ya Tyneside bila umaarufu mkubwa, hakuna mtu aliyejua walichokitarajia.
Ba alikuwa ameichezea West Ham na kujiunga na Newcastle kwa uhamisho wa bila malipo mnamo mwezi Juni 2011 baada ya kufeli vipimo vya matibabu katika klabu ya Stoke, huku Cisse akijiunga kutoka Freiburg mnamo mwezi Januari 2012, baada ya kufunga mabao machache katika ligi ya Bundesliga.
Wachezaji hao hawakuwa na umaarufu mkubwa.
Hatahivyo msimu wa 2011-12 ulikuwa mzuri sana kwa klabu hiyo.
Huku Alan Pardew akiwa uongozini, Ba na Cisse waliisaidia Newcastle kupanda hadi nafasi ya tano, huku wakikaribia kufuzu katika kombe la vilabu bingwa Ulaya , wakifunga magoli 29 kati yao.
Na sote tunakumbuka kwamba Cisse alifunga bao la ndizi , mumesahau? akiwa katika mstari katika uwanja wa Stamford Bridge , mbele ya mashabiki wa ugenini akimfunga kipa Petr Cech- boom.
Ahsante Papis Cisse.
Mchezo mzuri wa wawili hao ulisaidia kuwalaza wapinzani wao na kumfanya Ba kuitwa Chelsea 2013 na kuvunja ushirikiano uliokuwepo kati ya wawili hao.
Michu

Chanzo cha picha, Getty Images
Magoli 19, katika mechi 35 na kupanda hadi nafasi ya tisa katika jedwali la ligi ya Uingereza.
Michu aliung'arisha uwanja wa Liberty Stadium baada ya uhamisho wake kuelekea Swansea msimu wa 2012-13.
Mshambuliaji huyo alikuwa muhimu sana sio tu kwa klabu ya Swansea bali kwa kila timu iliopenda soka.
Alifunga magoli mawili dhidi ya Arsenal na kuisaidia klabu hiyo kuishinda Arsenal nyumbani mbali na mechi zote mbili dhidi ya Manchester United.
Ni msimu ambao kila kitu alichoshika kiligeuka na kuwa dhahabu. Vichwa, mguu wa kulia, mguu wa kushoto ulikuwa ulimwengu wa Michu na tulikuwa tukiishi ndani yake.
Aliisaidia klabu hiyo ya Swansea kushinda kombe la ligi.
Hatahivyo Michu hakusalia kwa muda mrefu -huku majeraha yakimzuia.
Mchezaji huyo wa Uhispania hakuweza kuendelea na mchezo wake mzuri hata baada ya kupona jeraha lake 2012-13, akifunga magoli mawili dhidi ya Wales na kushiriki mechi tatu akiichezea Napoli wakati alipouzwa kwa mkopo 2013.
Alistaafu 2017 kutokana na jeraha , lakini hatosahau kumbukumbu za msimu wake wa kwanza katika ligi ya Uingereza.
Hatem Ben Arfa

Chanzo cha picha, Getty Images
Tukirudi katika uwanja wa Tyneside na kumuangazia mshambuliaji wa Ufaransa, Hatem Ben Arfa.
Alikua amejiunga na klabu hiyo kwa mkopo kutoka Marseille 201, Ben Arfa alikuwa mmojawapo wa wachezaji wazuri katika soka na alionyesha mchezo mzuri.
Goli moja ambalo 2012 alichukua mpira katika upande mmoja wa uwanja akawchenga mabeki wa Bolton Wandarers na kucheka na wavu.
Ben Argfa alikuwa mchezaji kamili wa Newcastle mnamo mwezi Januari 2011, akisaini mkataba wa miaka minne, lakini akashindwa kuonyesha umahiri wake.
Ni kitu ambacho kiliwaudhi mashabiki wa klabu ya Newcastle kwa kuwa walikuwa wakijua kile anachoweza kufanya.
Aliondoka Newcastle 2015 na kurudi nchini Ufraansa kuichezea klabu ya Ligue 1.
Andrey Arshavin

Chanzo cha picha, Getty Images
Ni rahisi kumsahau raia huyu wa Urusi Andrey Arshavin ambaye alikuwa mmojawapo wa wachezaji wazuri kwa muda mfupi kati ya 2008 na 2009.
Alijiunga na Arsenal mwaka 2009 mwezi Januari baada ya kuisaidia klabu ya Zenit St Petersburg kushinda kombe la Uefa Cup 2008 na kuwa mmoja wa nyota Ulaya msimu huo , akiisaidia Urusi kufika nusu fainali.
Miezi mitatu baada ya kuandikisha mkataba na Arsenal, klabu ya The Gunners ilikabiliana na Liverpool katika uwanja wa Anfield katika mechi kali, huku Arshavin akifunga magoli manne pekee katika droo ya 4-4 hatua iliokatiza matumaini ya liverpool kushinda kombe la ligi ya Uingereza.
Arshavin pia alifunga goli dhidi ya Man United mnamo mwezi Agosti 2009 na kuisaidia Arsenal kushinda mechi ya awamu ya kwanza dhidi ya Barcelona katikja mechi ya vilabu bingwa Ulaya 2011.
Lakini huo ndio uliokuwa mwisho wake. Alirudi nchini Urusi akiichezea Zenit 2013 na baadaye kuhamia katika ligi ya Kazakhstan na kustaafu katika soka 2018.
Huenda hawakung'aa sana katika soka kama vile wachezaji wengi tajika lakini iwapo wachezaji hawa hawakutoa mchango wao, soka haingekuwa ilivyo sasa.
Mitaa kamwe haitosahau na sisi pia hatufai kuwasahau.













