Serikali ya Kenya yapoteza mabilioni ya fedha kuwalipa polisi bandia

polisi wa Kenya

Chanzo cha picha, AFP/GETTY

Muda wa kusoma: Dakika 2

Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta amesema kuwa usajili wa kidijitali wa maafisa wa polisi nchini humo umewafichua zaidi maafisa 5000 bandia.

Alisema hayo wakati wa uizunduzi wa mpango wa usajili wa watu kupitia mfumo wa kidijitali unaofahamika kama 'Huduma Namba'.

Bwana Kenyatta ameongeza kuwa serikali yake imekuwa ikipoteza zaidi ya dola 148,000 kila mwaka kuwalipa maafisa hao bandia.

"Baada ya kukamilisha usajili wa maafisa wa polisi tutaelekea katika idara ya magereza hadi tuwasajili wafanyikazi wote wa umma," alisema bwana Kenyatta.

Ruka X ujumbe, 1
Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)

Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue

Onyo: Imetoka kwingine na inaweza kuwa na matangazo

Mwisho wa X ujumbe, 1

Hatua hiyo ni sehemu ya mageuzi katika idara ya polisi iliyotangazwa na serikali yake mwaka jana.

Data ya mtu binafisi iliyo faraghani.

Rais Kenyatta pia aliwahakikishia wakenya kwamba serikali yake italinda data za watu binafsi iliyo faraghani.

Ameongeza kuwa hatua madhubuti zimechukuliwa kushughulikia hoja zilizoibuliwa kuhusiana na usalama wa mfumo huo mpya wa kuwasajili watu kidijitali.

"Sote tunafahamu changamoto ambazo wakenya wanapitia kupata huduma za serikali kutokana na ukosefu wa stakabadhi muhimu. Lakini ukiwa na Huduma Namba, hakuna afisa wa serikali atakunyima haki kupata huduma za msingino," alisema.

Ruka X ujumbe, 2
Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)

Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue

Onyo: Imetoka kwingine na inaweza kuwa na matangazo

Mwisho wa X ujumbe, 2

Aliwakemea viongozi wa kidini kwa kupotosha umma kuhusiana na mpango huo ambao uinatarajiwa kukamilishwa katika siku 45 zijazo.

"Naomba tusitumie nyadhifa tulizo nazo katika jamii kueneza taarifa za uwongo. Kuna wengin wanasema kuwa usajili huo utajumuisha mahusiano yao ya pembeni. Huo ni uwongo'' Alisema bwana Kenyatta.

Hata hivyo makundi matatu ya kutetea haki za binadamu yamepinga mfumo huo yakidai kuwa huduma namba haifai kutumika kumnyima Mkenya haki ya kupata huduma muhimu kulingana na katiba.

''Makundi mengine katika jamii yatatengwa'', yalisema kupitia taarifa ya pamoja kwa vyombo vya habari.

Mpango huo tayari umeufanyiwa majaribio katika majimbo kumi na tano ikiwa ni pamoja na jimbo la Nairobi miongoni mwa nyingine.

Mahakama kuu nchini Kenya imeamua kuwa hakuna mtu anayestahili kushurutishwa kujisajili.

Shirika la Nubian Rights Forum ambalo ni moja ya makundi yanayopinga mpango huo limeandika hivi katika mtandao wake wa Twitter.

Ruka X ujumbe, 3
Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)

Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue

Onyo: Imetoka kwingine na inaweza kuwa na matangazo

Mwisho wa X ujumbe, 3

Usajili huo unalenga kupata sajili moja, ambapo kila mtu atapewa nambari maalumu kwa jina Huduma Namba na hakuna atakayehudumiwa na serikali bila kuwa na nambari hiyo maalumu.

Baadhi ya data zitakazochukuliwa ni picha ya kila anayesajiliwa, jina, jinsia, tarehe ya kuzaliwa, umri, eneo la kuzaliwa, uraia, maelezo kuwahusu wazazi, nambari za simu, anwani ya baruapepe, anwani ya mahali anakoishi na hali ya ndoa.

Shughuli hiyo itagharimu kati ya shilingi bilioni 5 na shilingi bilioni 6 za Kenya.