Akaunti rasmi za Facebook na Twitter za rais Uhuru Kenyatta zimefutwa

Chanzo cha picha, REUTERS
Akaunti zote rasmi za mitandao ya kijamiii ya rais wa Kenya Uhuru zimefungwa baada ya kutumiwa na watu ambao ''hawajaidhinishwa", amesema mkuu wa wafanyakazi wake kwenye ujumbe wa Twitter.
Nzioka Waita hakutoa taafa kuhusu namna uingiliwaji wa mitandao hiyo ulivyotokea, lakini akaongeza kuwa itarejeshwa tena mtandaoni baada ya kuchukuliwa kwa "hatua za suluhu ya tatizo hilo ".
Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue
Mwisho wa X ujumbe
Akaunti za Twitter na Facebook za Bwana Kenyatta zina mamilioni ya wafuasi.
Gazeti la kibinafsi la The Star nchini humo limeripoti kuwa ujumbe uliotumwa kwenye Twitter unaoangaliwa kama kuwa nwenye utata wa kisiasa, uliotumwa leo asubuhi, ulikuwa ndio sababu ya kufungwa kwa akaunti hizo.
Gazeti la The Star lilishirikisha umma picha ya ujumbe huo wa Twitter:

Chanzo cha picha, The Star/ Twitter
Gazeti hilo limeripoti kuwa maneno yaliyoandikwa kwenye ujumbe huo tata yaliyosema "mshirika wangu wa karibu wa kisiasa" katika twittee hiyo huenda ulimaanisha Naibu rais wa Kenyatta, William Ruto.
Wafuasi wa Bwana Ruto wamekuwa wakikosoa vikali vita vya rais Kenyatta vya hivi karibuni dhidi ya ufisadi ambavyo vimesababisha kukamatwa na kuhojiwa kwa maafisa wa serikali, wakisema kuwa vimekuwa na njama dhidi ya naibu wake.
Wanasema kuwa watu walio karibu na Bwana William Ruto wamekuwa wakilengwa.

Chanzo cha picha, Reuters
Uhusiano baina ya viongozi hao wawili , ambao waligombea nafasi zao chini ya Muuungao wa Jubelee, katika uchaguzi wa mwaka 2013 na 2017, unasemekana kuingia dosari hivi karibuni, husasn baada ya Bwana Kenyatta kusaini makubaliano na kiongozi wa upinzani Raila Odinga.
Bwana Odinga na Bwana Kenyatta - walikuwa na uhasama mkubwa wa kisiasa wakati wa uchaguzi wa mwaka 2017 - walikubaliana kufanya kazi pamoja mwaka 2018 kwa ajili ya "kuteta amani nchini ".
Uhusiano wa karibu wa Bwana Kenyatta na Bwana Odinga na pia kuongezeka wa umaarufu wa Bwana Odinga tangu walipofanya makubaliano kunaangaliwa na baadhi ya watu kama njama za kisiasa za kumaliza mpango wa Bwana Ruto wa kumrithi Bwana Kenyatta kama rais.












