Tetesi za Soka Ulaya Jumapili 02.12.2018: Pickford, De Gea, Ramsey, Clyne, Pulisic

Chanzo cha picha, Getty Images
Manchester United wako tayari kutumia pauni milioni 70 kwa mchezaji wa Everton raia wa England Jordan Pickford, 24, ikiwa watampoteza mhispania David de Gea, 28, kwenda Paris St-Germain. (Sunday Mirror)
De Gea atapinga jitihada zozote za Manchester United za kumuuza kabla ya mkataba wake kumalizika mwaka 2020, lakini anaweza kusalia Old Trafford ikiwa watamfanya kuwa mchezaji mwenye mshaharaja wa juu zaidi. (Times - subscription required)

Chanzo cha picha, Getty Images
Napoli wamekataa ofa ya Manchester United ya pauni milioni 91 ya mchezaji wa kimtaiafa raia wa Senegal Kalidou Koulibaly, 27. (Corriere dello Sport, via Mail on Sunday)
Mchezaji wa Arsenal Mesut Ozil, 30, atafikiria hatua zake msimu ujao ambapo huenda akaamua kutua huko Inter Milan. (Sun on Sunday)
Real Madrid watamwendea ghafla kiungo wa kati wa Arsenal Aaron Ramsey, 27, in January. (Sunday Mirror)

Chanzo cha picha, Getty Images
Meneja wa Fulham Claudio Ranieri ameomba Liverpool kumruhusu achukue mlinzi raia wa Uingereza Nathaniel Clyne, 27, kwa mkopo kwa msimu wote. (Sun on Sunday)
Chelsea wana mpango ya kumsaini kiungo wa kati wa Borussia Dortmund Christian Pulisic, lakini wanataka kupunguza thamani ya pauni milioni 70 iliyowekwa na wakuu wa Bundesliga kwa mchezaji huyo wa kimataifa wa Marekani mwennye miaka 20. (Goal.com)

Chanzo cha picha, Getty Images
Chelsea wamejiunga na vilabu kadhaa, ikiwemo Everton, Juventus na Manchester United, kumfuatilia mlinzi raia wa Brazil Eder Militao, anayeichezea Porto. (Mail on Sunday)
Beki wa Liverpool, Joel Matip, 27, ameshuka ngazi kwenye kikosi lakini na moyo wa kusalia na kupigania nafasi yake badala ya kuondoka. (Star on Sunday)
AC Milan wamejiunga na Arsenal na Chelsea kumwinda kiungo wa kati wa Barcelona Denis Suarez, 24. (Sunday Express, via Calciomercato)

Chanzo cha picha, Getty Images
Meneja wa Newcastle United Rafael Benitez anataka kuwasaini wachezaji wawili wiki mbili za kwanza za Januari. (Newcastle Chronicle)
Watford, Cardiff na West Brom ni kati ya vilabu vinavyommemzea mate wing'a wa Nottingham Forest Joe Lolley, 26. (Mail on Sunday)

Chanzo cha picha, Getty Images
Meneja wa Liverpool Jurgen Klopp anasema timu zingine zinaiogopa sana Manchester City na hazionyeshi kikosi chake heshima jinsi zinaonyesha kwa mabingwa hao wa Premier League. (Sunday Express)
Claudio Ranieri anasema kukutana na Chelsea na Leicester kama meneja wa Fulham itakuwa yenye hisia lakini lengo lake kuu ni kuzuia kushushwa. (London Evening Standard, via Gazzetta dello Sport)












