Tetesi za Soka Ulaya Jumatano 03.10.2018: Pogba, Scholes, Mourinho, Luiz, Welbeck, Rabiot

Paul Pogba

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Paul Pogba

Mabingwa wa Ufaransa Paris St-Germain wanataka kumsaini kiungo wa kati wa Manchester United Mfaransa Paul Pogba, 25. (The Sun)

Kiungo wa kati zamani wa Manchester United Paul Scholes, 43, anasema ameshangazwa kuwa meneja Jose Mourinho hakufutwa baada ya kushindwa kwa mabo 3-1 na West Ham siku ya Jumamosi. (BT Sport)

Mshambuliaji Mfaransa Christophe Dugarry anasema kocha wa zamani wa Real Madrid Zinedine Zidane, 46, mchezaji mwenzake wa zamani wa kimataifa hawezi kuchukua mahala pake Mourinho huko Old Trafford. (RMC Sport - kwa Kifaransa)

Christophe Dugarry

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Christophe Dugarry

Mshambuliajia wa Arsenal Danny Welbeck anatarajiwa kumfuata kiungo wa kati Aaron Ramsey kuondoka Arsenal msimu ujao.

Mchezaji huyo mwenye miaka 27 wa kimataifa wa England yuko katika mwaka wake wa mwisho na hakuna makubaliano kuhusu mkataba wake mpya. (Mirror)

Danny Welbeck

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Danny Welbeck

Manchester City wamekuwa wakimtazama kiungo wa wkati wa timu ya vijana ya Hoffenheim, Ilay Elmkies. MuIsrael huyo, 18, alifunga dhidi ya timu ya vijana wa Man City wikendi iliyopita. (Bild - in German)

Tottenham wako tayari kutoa ofa kwa mchezaji wa Paris St-Germain Adrien Rabiot mwezi Januari. Kiungo huyo wa kati mwenye miaka 23 raia wa Ufaransa hana mkataba msimu ujao na hivyo anaweza kuongea na klabu nyingine mwezi Januari. (Mirror)

Adrien Rabiot

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Adrien Rabiot

Kocha wa muda wa Argentina Lionel Scaloni anasema hajazungumza na mshambuliaji wa Manchester City Sergio Aguero kuhusu kurudi kwenye timu ya taifa. Aguero, 30, hakucheza katika mechi za kirafiki za kufuzu kwa kombe la dunia. (ESPN)

Chelsea watampa kiungo wa kati Mbrazil David Luiz mkataba wa mwaka mmoja zaidi. Mkata wa mchezaji huyo mwenye miaka 31 unakamilika mwisho wa msimu. (Evening Standard)

Jadon Sancho

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Jadon Sancho

Wing'a wa Borussia Dortmund Jadon Sancho, 18, yuko katika orodha ya wachezaji wa England walio chini ya miaka 21 kuitwa wiki hii, huku Aidy Boothroyd akitarajiwa kumjumuisha kwenye kikosi chake cha kufuzu dhidi ya Andorra na Scotland wiki ijayo. (The Times)

Leeds United wanatarajiwa kuanza mazungumzo na kiungo wa kati wa England Kemar Roofe. Mchezaji huyo mwenye miaka 25 ana miaka miwii iliyobaki kwenye mkataba wake wa miaka minne. (Yorkshire Evening Post)

Andreas Granqvist

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Andreas Granqvist

Nahodha wa Sweden na beki Andreas Granqvist, 33, anasema nia ya Manchester United kumleta klabuni ni kitu anachokisifia sana. (FotbollDireckt - in Swedish)

Kipa wa Liverpool Alisson anasema anatathmini kubaki huko Roma kabla ya kujiunga na klabu ya Ligi ya Premier. Mchezaji huyo mwenye miaka 26 raia wa Barzil ambaye alijiunga na Liverpool mwezi Julai alisema alilia wakati aliondoka Rome ambapo binti yake alizaliwa. (La Gazzetta dello Sport - kwa Kitaliano)

Hakuna uwezekano wa Barcelona kumsaini mchezaji yeyote mwezi Januari. (Mundo Deportivo)

Bora zaidi Kutoka Jumanne

Meneja wa Manchester City Pep Guardiola ameka nushataarifa kwamba anataka kumnunua mshambuliaji wa Paris St-Germain Kylian Mbappe, 19. (Independent)

Kylian Mbappe

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Kylian Mbappe

Bodi ya Barcelona imagawanyika kuhusu ikiwa itamwendea kiungo wa kati wa Manchester United Paul Pogba, 25 mwezi Januari lakini mabingwa hao wa Uhispania wanaamini wana uwezo wa kifedha wa kutosha kuweza kumsaini Mfaransa huyo mshindi wa Kombe la Dunia. (ESPN)

Real Madrid wamejiunga katika kundi la klabu zinazomzea mate mchezaji wa kimataifa wa Wales Aaron Ramsey, 27, ambaye atondoka Arsenal mwezi January. (Teamtalk)

Aaron Ramsey

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Aaron Ramsey

Arsenal ni kati ya vilabu vinavyommezea mate mchezaji wa Lille, Nicolas Pepe, 23.

Mchezaji huyo wa kimataifa wa Ivory Coast mwenye thamani ya pauni milioni 30 amepokelewa vizuri chini Ufaransa kwa mchezo wake mzuri msimu huu baada ya kufunga mabao matano katika mechi nane.

Nicolas Pepe

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Nicolas Pepe

Chelsea wako katika nafasi nzuri ya kumsaini mchezaji mwenye miaka 15 wa Volendam Mholanzi Sam Lautenschutz. (The Sun)

Wolves wanamwinda mlinzi wa Aberdeen raia wa Scotland Scott McKenna. Ofa za Celtic na Aston Villa zimekataliwa kwa mchezaji huyo mwemye miaka 21. (Scottish Sun)