Golden Boy: Kylian Mbappe, Boubacar Kamara, Phil Foden & Trent Alexander-Arnold kushindania tuzo ya kinda bora duniani

Kylian Mbappe akichezea Monaco

Chanzo cha picha, PA

Maelezo ya picha, Mbappe alishinda tuzo hiyo mwaka jana

Mchezaji nyota wa Ufaransa Kylian Mbappe na raia mwenzake Boubacar Kamara wameorodheshwa kushindania tuzo ya mchezaji bora wa umri mdogo barani Ulaya.

Tuzo hiyo ambayo hufahamika kama 'Golden Boy' kwa maana ya Kinda wa Dhahabu imekuwa ikitolewa na gazeti la Italia la Tuttosport mwaka 2003.

Tuzo hiyo hutolewa kwa mchezaji bora zaidi wa chini ya miaka 21 barani Ulaya.

Mshambuliaji wa Paris Saint German Kylian Mbappe ambaye alishinda Kombe la Dunia akiwa na Ufaransa mwezi Julai anapigania kushinda tuzo hiyo kwa mwaka wa pili baada ya kushinda mwaka jana.

Kwa jumla wachezaji 40 wameorodheshwa.

Kwenye orodha hiyo kuwa mchezaji wa Liverpool Trent Alexander-Arnold na nyota wa Manchester City Phil Foden na pia Tom Davies wa Everton na mchezaji aliyenunuliwa na Manchester United mwezi Agosti Diogo Dalot.

Trent Alexander-Arnold

Chanzo cha picha, Andrew Powell

Mkabaji kamili Alexander-Arnold, 19, alicheza katika fainali ya Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya dhidi ya real Madrid mwezi Mei ambao Liverpool walishindwa, na pia alikuwa kwenye kikosi cha England cha Kombe la Dunia kilichotumiwa na meneja Gareth Soutgate.

Foden, 18, bado hajachezeshwa timu ya taifa lakini alikuwa mfungaji mabao bora katika Kombe la Dunia la wachezaji wa chini ya miaka 17 mwaka jana.

Alifunga bao lake la kwanza akichezea Manchester City mechi yao waliyowashinda Oxford katika Kombe la Carabao Jumatano.

Washindi wa awali ni pamoja na Neymar, Edinson Cavani, Lionel Messi, Wayne Rooney na Paul Pogba.

Orodha kamili ya wachezaji wanaoshindania tuzo

1) Trent John ALEXANDER-ARNOLD, LIVERPOOL, West Derby (Liverpool, England), 7 Oktoba 1998, England, Beki

2) Kelvin Adou AMIAN, TOLOSA, Toulouse (Fra), 8 Februari 1998, France-Ivory Coast Beki

3) Houssem AOUAR, OLYMPIQUE LIONE, Lyon (Fra), 30 Juni 1998, France-Algeria, Kiungo wa kati

4) Musa BARROW, ATALANTA, Banjul (Gam), 14 Novemba 1998, Gambia, Mshambuliaji

5) Justin BIJLOW, FEYENOORD, Rotterdam (Ola), 22 Januari 1998, Dutch, Mlinda lango

6) Josip BREKALO, WOLFSBURG, Zagreb (Cro), 23 Juni 1998, Croatia, Mshambuliaji

7) Patrick CUTRONE, MILAN, Como (Italy), 2 Januari 1998, Italia, Mshambuliaji

8) Daniel Carvajal DANI OLMO, DINAMO ZAGABRIA, Terrassa (Spa), 7 Mei 1998, Uhispania, Mshambuliaji

9) Thomas DAVIES, EVERTON, Liverpool (Eng), Juni 30, 1998, England, Kiungo wa kati

10) Matthijs DE LIGT, AJAX, Leiderdorp (Ola), 12 Agosti 1999, Uholanzi, Beki

11) Moussa DIABY, PARIS SAINT-GERMAIN, Paris (Fra), 7 Julai 1999, France-Ivory Coast, Mshambuliaji

12) José Teixeira DIOGO DALOT, MANCHESTER UNITED, Braga (Por), 18 Machi 1999, Ureno Kiungo wa kati

Boubacar Kamara wa Olympique Marseille akicheza mechi ya Europa League dhidi ya RB Leipzig 5 Aprili, 2018

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Boubacar Kamara

13) Moussa DJENEPO, STANDARD LIEGI, Bamako (Mli), 15 Juni 1998, Mali, Kiungo wa kati

14) Ritsu DOAN, GRONINGEN, Amagasaki (Gia), 16 Juni 1998, Japan, Mshambuliaji

15) Gabriel ÉDER MILITÃO, PORTO, Sertãozinho (SP, Bra), 18 Januari 1998, Brazil, Beki

16) Odsonne ÉDOUARD, CELTIC GLASGOW, Kourou (Guyana, Fra), 16 Januari 1998, France-Guyana, Mshambuliaji

17) Ferreira da Silva EVANDER, MIDTJYLLAND, Rio de Janeiro (Bra), 9 Juni 1998, Brazil, Mshambuliaji

18) Philip Walter FODEN, MANCHESTER CITY, Stockport (Eng), 28 Mei 2000, England, Kiungo wa kati

19) Achraf Mouh HAKIMI, BORUSSIA DORTMUND, Madrid (Spa), 4 Novemba 1998, Uhispania-Morocco, Beki

20) Amadou HAIDARA, RED BULL SALZBURG, Bamako (Mli), 31 Januari 1998, Mali, Kiungo wa kati

21) Siqueira JOÃO FÉLIX, BENFICA, Viseu (Por), 10 Novemba 1999, Ureno, Kiungo wa kati

22) João Pedro Neves Filipe JOTA, BENFICA, Lisbon (Por), Machi 30, 1999, Ureno, Mshambuliaji

23) Eduardo Borges JOVANE CABRAL, SPORTING LISBON, Assomada (CPV), 14 June 1998, Cape Verde, Mshambuliaji

24) Dejan JOVELJIC, STELLA ROSSA, Bijeljina (Bos), 7 Agosti 1999, Bosnia- Serbia, Mshambuliaji

25) Boubacar KAMARA, OLYMPIQUE MARSEILLE, Marseille (Fra), 23 Novemba 1999, France-Mauritania, Beki

26) Moise Bioty KEAN, JUVENTUS, Vercelli (Ita), 28 Februari 2000, Italia-Ivory Coast, striker

27) Abdoulaye Jules KEITA, DIGIONE, Conakry (Gui), 20 Julai 1998, Guinea, Mshambuliaji

28) Justin KLUIVERT, ROME, Zaandam (Ola), Mei 5, 1999, Uholanzi-Suriname, Mshambuliaji

29) Alban LAFONT, FIORENTINA, Ouagadougou (Buf), 23 Januari 1999, France-Burkina Faso, portierte

30) Manuel Alonso MANU GARCIA, TOLOSA, Oviedo (Spa), 2 Januari 1998, Uhispania, Kiungo wa kati

31) Kylian Sanmi Lottin MBAPPÉ, PARIS SAINT-GERMAIN, Bondy (Fra), 20 Desemba 1998, France-Cameroon, Mshambuliaji

mbappe anfield

Chanzo cha picha, Michael Regan

Maelezo ya picha, Kylian Mbappe alifunga bao katika mechi ambayo PSG walishindwa 3-2 na Liverpool uwanjani Anfield katika Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya mwezi Septemba

32) Pietro PELLEGRI, AS MONACO, Genoa (Ita), Machi 17, 2001, Italia, Mshambuliaji

33) Christian Mate PULISIC, BORUSSIA DORTMUND, Hershey (PA, Usa), Septemba 18, 1998, Marekani-Croatia, Kiungo wa kati

34) Marcelo Josemir Pintos SARACCHI, RB LIPSIA, Paysandú (Uru), 23 Aprili 1998, Italia-Uruguay, Beki

35) Ismaila SARR, RENNES, Saint-Louis (Sen), 25 Februari 1998, Senegal, Mshambuliaji

36) Dayotchanculle Oswald UPAMECANO, RB LIPSIA, Évreux (Fra), 27 Oktoba 1998, France-Guinea, Beki

37) José Paixão de Oliveira VINICIUS JUNIOR, REAL MADRID, San Gonçalo (Bra), 12 Julai 2000, Brazilian, Mshambuliaji

38) Moussa WAGUÉ, BARCELONA, Bignona (Senegal), 4 Oktoba 1998, Senegal, Beki

39) Timothy Tarpeh WEAH, PARIS SAINT-GERMAIN, New York (USA), 22 Februari 2000, France-Marekani, Mshambuliaji

40) Nicolò ZANIOLO, ROMA, Massa (Italia), 2 Julai 1999, Italia, Kiungo wa kati