Tetesi za Soka Ulaya Jumatatu 27.08.2018: David Luiz, Mesut Ozil, Juan Mata, Anthony Martial, Theo Walcott, Mario Mandzukic

David Luiz

Chanzo cha picha, Getty Images

Meneja wa Arsenal Unai Emery anatarajia mchango zaidi kutoka kwa kiungo wa kati wa Ujerumani Mesut Ozil, 29, aliyekosa mechi ya Jumamosi dhidi ya Westham kutokana na kuugua. Arsenal walishinda 3-1. (Mirror)

Beki wa Brazil David Luiz, 31, anasema huenda angelazimika kuihama Chelsea iwapo Antonio Conte angesalia kama meneja wa klabu hiyo. (Sky Sports)

Mlindalango wa Liverpool Simon Mignolet, 30, anasema inashangaza kwamba klabu hiyo ya Anfield ilimruhusu kipaLoris Karius kujiunga na Besiktas ya Uturuki kwa mkopo. Mbelgiji huyo anasema hajui mustakabali wake katika klabu hiyo ya England. (Liverpool Echo)

Beki wa Tottenham Danny Rose, 28, huenda akahamia Marseille - kwa mkopo au kwa mkataba wa kudumu - katika juhudi zake za kutaka kujiimarishia nafasi ya kucheza katika timu ya taifa ya England. (Star)

Mario Mandžukić

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha, Mario Mandžukić alikataa kujiunga na Man Utd

Meneja wa Spurs Mauricio Pochettino amewaambia wachezaji wake kwamba wote ni lazima wamridhishe tena baada yake kulazimika kuwatumia wachezaji mbadala kutokana na baadhi yao kushiriki Kombe la Dunia. (Telegraph)

Meneja wa Newcastle Rafael Benitez amesema anaridhishwa na uamuzi wa kuchelewesha mazungumzo kuhusu mkataba wake mpya hadi mwaka ujao. Mhispania huyo alitarajiwa kutia saini mkataba mpya kabla ya msimu lakini sasa anasema anafikiria tu kuhusu mechi. (Goal)

Danny Rose

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Danny Rose

Benitez alimwacha nje nahodha wa klabu hiyo ambaye pia ni beki Jamaal Lascelles kutoka kwa mechi ya Jumapili ambayo walishindwa 2-1 na Chelsea baada yao kuzozana mazoezini kuhusu mbinu za kutumiwa kwenye mechi hiyo. (Mail)

Mshambuliaji wa Juventus Mario Mandzukic, 32, alikataa ofa ya kujiunga na Manchester United. (Calciomercato kupitia Sun)

Winga wa Everton Theo Walcott, ambaye hajachezeshwa timu ya taifa ya England kwa miaka miwili anasema bado hajapoteza matumani kwamba anaweza kuchezeshwa. (Independent)

West Ham wamepokea ofa kutoka kwa klabu ya Uholanzi AZ Alkmaar na klabu ya Uhispania Eibar wote wakimtaka beki wa England mwenye miaka 19 Reece Oxford. (Mail)

Juan Mata

Chanzo cha picha, Getty Images

Mlinzi wa Manchester United kutoka England Demetri Mitchell anakaribia kujiunga na Hearts kwa mkopo. Mchezaji huyo wa miaka 21 alicheza mechi 11 katika klabu hiyo ya Scotland akiwa kwa mkopo mwaka jana. (ESPN)

Tottenham walikuwa wanamtaka mshambuliaji Anthony Martial, 22, na pia kiungo wa kati Juan Mata, 30, kutoka kwa Manchester United, lakini maombi yao yakakataliwa. (Manchester Evening News)

Meneja wa AC Milan Gennaro Gattuso amesema kiungo wa kati Mfaransa Tiemoue Bakayoko - aliye nao kwa mkopo kutoka Chelsea - ni lazima ajifunze "mambo kadha ya msingi" baada ya klabu hiyo kushindwa 3-2 Napoli. (Eurosport)

Tiemoue Bakayoko

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Tiemoue Bakayoko

Atletico Madrid wanataka walipwe zaidi ya euro 30m (£27m) ndipo wakubali kumwachilia beki wa kushoto wa Brazil Filipe Luis ahamie Paris St-Germain. (AS kupitia Sport)

Liverpool wamemteua mkufunzi wa kurusha mipira ndani ya uwanja, wakitaka kuimarisha jinsi wanavyoshughulikia mipira ya kurushwa ndani ya uwanja, kona na frikiki. (Telegraph)

Bora kutoka Jumapili

Paris St-Germain wako tayari kuipa Tottenham ofa ya pauni milioni 100 kwa kiungo wa kati wa Denmark mwenye miaka 26 Christian Eriksen. (Sunday Express)

Christian Eriksen

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Christian Eriksen

Anthony Martial, 22, yuko tayari kusalia Manchester United baada ya kuvunjwa moyo kufuatia klabu yake kukataa kumuuza kuambatana na matakwa ya meneja Jose Mourinho. (Sunday Telegraph)

Na mshambuliaji Mfaransa Martial amasema atakuwa huko Old Trafford msimu mwingine baada ya kusaini mkataba wa miezi 12. (Sunday Mirror)

Kiungo wa kati wa Arsenal wa Wales Aaron Ramsey, 27, anajiandaa kufuata mfano wa mcheaji mwenzake Mesut Ozil wa kusubiri hadi mwezi Januari kuwezesha klabu kushughulikia mkataba wake. (Mail on Sunday)

Roman Abramovich

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Roman Abramovich

Chelsea wamekanusha ripoti kuwa mmiliki wake Roman Abramovich yuko tayari kuuza klabu hiyo. (Standard)

Eden Hazard

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Eden Hazard

Mshambuliaji Mbelgiji Eden Hazard, 27, angeweza kuondoka Chelsea kuelekea Real Madrid iwapo Zinedine Zidane angebaki kuisimamia klabu hiyo ya Uhispania. (Hiet Niewuwsblad - kupitia Talksport)