Claudio Bravo: Kipa wa Man City apasuka mshipa wakati wa zoezi

Chanzo cha picha, Getty Images
Kipa wa Manchester City raia wa Chile Claudio Bravo amepasuka mshipa wa Achilles wakati wa mazoezi siku ya Jumatatu.
Mchezaji huyo mwenye miaka 35 alipigwa picha kuthibitisha jeraha hilo na anatarajiwa kusafiri hadi Barcelona kufanyiwa ukaguzi wa ziada Alhamisi wiki hii.
Jeraha lake Bravo linaicha City ikimtegemea Daniel Grimshaw mwenye umri wa miaka 20 anayeichukua nafasi ya naibu wa chaguo la kwanza la Ederson.
Mchezaji wa kiungo cha kati Kevin de Bruyne tayari amethibitishwa kuwa hatocheza kwa miezi mitatu baada ya kuumizwa goti pia akiwa katika mazoezi.
Claudio Bravo ameicheza ManCity mechi tatu pekee za ligi ya England msimu uliomalizika 2017-18.
Hatahivyo kipa huyo aliyesajiliwa kutoka Barcelona kwa thamani ya £15.4m mnamo 2016,aliwajibika kutoa ulinzi wa maana.
Uwepo wake ulimruhusu Guardiola kumuuza kipa wa England mwenye umri wa chini ya miaka 21 Angus Gunn kwa timu ya Southampton mnamo Julai na pia Joe Hart kwa timu ya Burnley mwezi Agosti.
Wakati Grimshaw akisubiriwa kuonekana kucheza mechi kuu , alisaini mktaba wa miaka mitatu katika klabu hiyo mnamo Juni.

Chanzo cha picha, @C1audioBravo












