Arsène Wenger apewa makaribisho makubwa Liberia

Baadhi ya mashabiki walifika kumkaribisha Wenger

Chanzo cha picha, EPA

Maelezo ya picha, Baadhi ya mashabiki walifika kumkaribisha Wenger

Aliyekuwa meneja wa Asenal Arsène Wenger amwwasilia nchini Liberia kabla a kutuzwa siku ya Ijumaa ambapo atapewa tuzo la juu nchini humo.

Wenger alikuwa kocha wa kwanza wa Rais George Weah kwenye klabu ya Ulaya baada ya Wenger kumleta Monaco 1988.

Weah ndiye mwafrika wa kwanza kushinda tuzo la Fifa la mchezaji wa mwaka.

Alistaafu kutoka soka mwaka 2003 na kuingia siasa.

Watu nchini Liberia wamekuwa wakisambaza picha za Wenger akikaribishwa nchini humo.

Wenger atapewa tuzo la hadhi ya juu zadi nchini Liberia katika hatua ambayo imezua maoni tofauti nchini humo.

Wenger alikuwa kocha wa kwanza wa Rais George Weah kwenye klabu ya Ulaya baada ya Wenger kumleta Monaco 1988.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Wenger alikuwa kocha wa kwanza wa Rais George Weah kwenye klabu ya Ulaya baada ya Wenger kumleta Monaco 1988.

Baadhi wanasema kuwa tuzo hiyo haistahili kupewa mtu binafsi kwa kile amemfanyia rais pekee.

Lakini tuzo hiyo si tuzo kuhusu uhusiano wa Rais na Wenger bali inatambua kile Wenger amechangia kwa michezo barani Afrika na kuwapa waafrika wengi fursa kwa mujibu wa waziri wa habari.

Rais Weah amesema kuwa Wenger "alinitunza kama mtoto wake" wakati alijiunga na Monaco, akisema kuwa "kando na Mungu, anafikiri kuwa bila ya Wenger hakuna vile nigefanikiwa Ulaya".