Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Tetesi za Soka Jumatatu 30.07.18 Crouch, Maguire, Pickford, Darmian, Courtois, Willian
Burnley inatayarisha £500,000 kumnunua mshambuliaji wa Stoke Peter Crouch, mwenye umri wa miaka 37. (Sun)
Mlinzi wa England Harry Maguire, mwenye umri wa miaka 25, ana hamu ya kuhama kwa thamani ya £65m kwenda Manchester Unitedlakini hatolazimisha uhamisho , na Leicester inaona uzito kumuuza. (Mirror)
Jordan Pickford anatarajiwa kupewa mktaba mpya Everton wakati wanapotazamia kutathmini mustakabali wa kipa huyo wa England mwenye umri wa miaka 24- aliyehusishwa na uhamisho kwenda Chelsea. (The Times)
Real Madrid imewasilisha ombi la kwanza kwa Chelsea la thamani ya £100m kwa kipa Thibaut Courtois, mwenye umri wa miaka 26, na mchezaji wa kiungo cha kati Willian, aliye na miaka 29. (Mail)
Huenda Chelsea ikamuwania mlinzi wa Juventus Mattia Caldara, mwenye umri wa miaka 24, badala ya mshambuliaji Gonzalo Higuain, aliye na miaka 30, ambaye aliwahi kuhusishwa na uhamisho kwenda the Blues. (Corriere della Sera)
Meneja wa Tottenham Mauricio Pochettino ametupilia mbali shutuma za timu hiyo kumsajili upya Gareth Bale, kutoka Real Madrid, lakini amesema anatambua umuhimu wa kusajili wachezaji wapya. (Sky Sports)
Aston Villa wamewasilisha ombi la kumsajili mchezaji wa Liverpool Ben Woodburn kwa mkopo, huku mchezaji huyo wa miaka 18 kutoka Wales akitarajiwa kuondolewa kutoka kambi ya mazoezi ya kikosi cha Jurgen Klopp nchini Ufaransa (Telegraph)
Mshambuliaji wa Chelsea Olivier Giroud anapanga kuipigania nafasi yake Stamford Bridge, licha ya kufanya mazungumzo na Marseille. (Mail)
Meneja wa Manchester United Jose Mourinho anasema hangenunua tiketi ya kutazama mechi ambapo timu yake ilifungwa 4-1 Liverpool katika ziara yao Marekani kabla ya kuanza kwa msimu. (Star)
Newcastle inafanya mazungumzo na West Brom kumsajili mshambuliaji wa Venezuela Salomon Rondon, mwenye miaka 28. (Sky Sports)
Aliyekuwa mshambuliaji wa Chelsea kutoka Middlesbrough Patrick Bamford, atafanyiwa ukaguzi wa afya kuelekea kujiunga na Leeds leoJumatatu kabla ya uhamisho huo unaokisiwa kuwana thamani ya £10. (Mail)
Mchezaji wa kiungo cha kati wa Liverpool Pedro Chirivella, mwenye umri wa miaka 21, anatarajiwa kufikia makubaliano ya mkataba wa tahamani ya £3.5m kuelekea timu ya Norway - Rosenborg baada ya makubaliano kati ya klabu hizo mbili.(Liverpool Echo)
Fulham inakaribia kumsajili mlinzi Alfie Mawson, mwenye umri wa miaka 24, kutoka Swansea, huku mazungumzo kati ya klabu hizo mbili yakiwa yamefikia kiwango kikuu. (Sky Sports)
Aston Villa inataka kumsajili winga wa West Ham mwenye umri wa miaka 30 Robert Snodgrass kwa mkataba mwingine wa mkopo , baada ya ya Mskotchi huyo kutoa huduma kwa timu hiyo msimu uliopita. (Birmingham Mail)
Derby wanakaribia kukamilisha usajili wa thamani ya £1m kwa mchezaji wa miaka 23 Reading - George Evans. (Sky Sports)
Winga wa Nottingham Forest Barrie McKay,anatarajiwa kujiunga na Swansea katika mkataba wa thamani ya £500,000. (Mail)