Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Serena Williams aomba ushauri wa mwanawe anayeota meno
Bingwa wa mchezo wa tenisi duniani upande wa wanawake Serena Williams huenda anakabiliwa na changamoto kubwa baada ya kuwataka mashabiki wake katika mitandao ya kijamii kumshauri vile atakavyokabiliana na tatizo la mwanawe wa kike anayeanza kuota meno.
''Tatizo la mwana anayemea meno ni gumu kutatua'', aliwaambia.
Anasema kuwa ametumia kila njia ikiwemo taweli za baridi mbali na kumpatia mwanawe kidole chake akisema kuwa alimbeba mwanawe hadi aliposhikwa na usingizi.
Mwanawe wa kike Alexis Olympia Ohanian Jr alizaliwa mnamo tarehe mosi mwezi Septemba
Mashabiki wa Serena nao walikuwa na ushauri tofauti kwake.
Wengi walimtaka kung'ata wanaserere matunda baridi ama hata barafu.
Pia walimshauri kutumia biskuti za kukabiliana na tatizo hilo mbali na mafuta.
Wengine walimshauri kumwacha mwanawe kung'ata maeneo ya kandokando ya blanketi na mto wa kulalia ama kumpatia mtoto huyo dawa za kukabiliana na tatizo la kuota meno miongoni mwa watoto.
Kulikuwa na mapendekezo ya kutumia maziwa ya mama iwapo anaendelea kunyonya ama hata kumnyonyesha kama njia moja ya kupunguza tatizo hilo.
Wengine walimtaka kutumia karafuu baridi ama mafuta ya karafuu ili kupaka katika ufizi wa mtoto huyo.
Mmoja alisema kuwa bibiye alitumia mfupa wa kuku kusugua ufizi.