Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Federer amshinda Nadal Shangai Masters
Bingwa mtetezi wa Wimbledon Roger Federer amemshinda mchezaji namba moja kwa ubora duniani Rafael Nadal kwa seti 6-4 6-3 katika michuano ya Shanghai na kuwa kikombe chake cha sita kwa mwaka huu.
Federer ambaye amepoteza michezo minne tu kwa mwka 2017, alikuwa katika kiwango cha juu na kushinda ndani ya dakika 72.
Ulikuwa ushindi wake wa nne kwa mwaka huu dhidi ya Nadal na wa sita mfululizo.
Federer ameshinda mataji 94 katika maisha yake ya uchezaji tenisi huku 19 ikiwa ni grand slam.
Inamfanya kufikia rekodi ya Ivan Lendl wakipitwa na Jimmy Connors wa Marekani mwenye vikombe 109.