Tetesi za Soka Ulaya Jumapili: Spurs inamfukuzia Robertson Liverpool

Muda wa kusoma: Dakika 2

Klabu za Tottenham na Liverpool zinajadili kifurushi cha pauni milioni 5 katika dili la nahodha wa Uskoti Andy Robertson, 31. (Mail)

Wakati huohuo, The Reds wamefufua nia ya kumsajili mchezaji wa Fulham mwenye umri wa miaka 28 na beki wa Marekani Antonee Robinson. (Teamtalk)

Bournemouth inakaribia kukamilisha usajili wa mkopo wa mlinda mlango wa Lazio na Ugiriki Christos Mandas, 24, kwa £2.6m. (Fabrizio Romano)

Arsenal italazimika kutumia pauni milioni 80 kumsajili mshambuliaji wa Atletico Madrid na Argentina Julian Alvarez, 25, msimu huu. (Football Insider)

Sunderland wamewasiliana na Borussia Monchengladbach kuhusu uwezekano wa kumsajili mlinda lango wa Uswizi Jonas Omlin, 32. (Florian Plettenberg, Sky Germany).

Beki wa Ukraine Oleksandr Zinchenko, 29, bado anajadiliana na Arsenal kuhusu masharti ya kuondoka kwake kwenda Ajax kwa mkataba wa kudumu. (Sky Sports)

Crystal Palace inalenga kumsajili mchezaji atakayeshikilia kwa muda nafasi ya Marc Guehi, 25, aliyejiunga na Ma City kabla ya dirisha la uhamisho kufungwa. (Givemesport)

Lazio ina nia ya kupata mkataba wa Januari kumsajili kiungo wa kati wa Everton Muingereza Tim Iroegbunam, 22. (Gianluca Di Marzio - kwa Kiitaliano), nje

Chelsea na Aston Villa zinamfuatilia kwa karibu winga wa Paris St-Germain mwenye umri wa miaka 18 na Senegal Ibrahim Mbaye. (Florian Plettenberg, Sky Germany)