Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Panama yatangaza siku kuu baada ya kufuzu kwa Kombe la Dunia
Rais wa Panama ametangaza siku ya Jumatano kuwa siku kuu baada ya nchi hiyo kufuzu kwa mechi za Kombe la Dunia kwa mara ya kwanaa kabisa.
Juan Carlos Varela aliandika katika Twitter, "Sauti za watu zimesikika...Kesho ni siku ya kitaifa."
Panama ilishinda Costa Rica mabao 2-1 mjini Panama City siku ya Jumanne.
Rais alisema kuwa wafanyakazi wa umma na wale wa makampuni ya kibinafsi watapumzika na pia shule hazitafunguliwa.
Watu nchini Panama walisherekea usiku kucha baada ya ushindi huo.
Hata hivyo kumekuwa na utata ikiwa goli la kwanza la Panama lilivuka mstari wa goli.
Panama imejaribu kufuzu kwa kila kombe la dunia tangu mwaka 1978 lakini haijafanikiwa hadi sasa.
Nchi hiyo itashiriki katika mechi za mwaka 2018 ambazo zinaanza Urusi mwezi Juni mwaka ujao.
Marekani ilikuwa katika kundi moja la kufuzu kwa nchi za kaskazini na kati mwa Marekani, lakini ikashindwa baada ya kupoteza kwa Trinidad and Tobago.
Mexico na Costa Rica na walifuzu.