Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Wachezaji 3 wa Arsenal waongeza kandarasi zao
Wachezaji wa Arsenal Olivier Giroud, Laurent Koscielny na Francis Coquelin wameongeza kandarasi zao na klabu hiyo.
Arsenal haijatangaza kuhusu kiwango cha kandarasi hizo ,lakini Koscielny amesema katika mtandao wa Twitter kwamba ataongeza kandarasi yake hadi mwaka 2020.
''Tunafurahi kwamba wachezaji watatu muhimu wameamua kusalia nasi kwa kipindi cha muda mrefu'', Mkufunzi wa Arsenal Arsene Wenger amenukuliwa akisema.
Wachezaji hao wa Ufaransa wamekuwa wakishiriki kila mechi huku Giroud akiweka kandarasi hiyo baada ya kufunga mabao manne katika mechi nne likiwemo bao lake la 'nge' dhidi ya Crystal palace.
''Francis ameimarika pakubwa katika kipindi cha miaka michache iliopita kwa sababu ana maono kila siku'', alisema Wenger.
''Olivier ana uzoefu katika mechi kubwa na ameimarika zaidi tangu ujio wake hapa. Koscielny ni kiungo muhimu wa kikosi chetu na ninaamini ni mmojawapo wa mabeki wazuri duniani''.