Uganda yazindua gari la kivita lililoundwa nchini humo

Gari hilo lililopewa jina la Chui - lilizinduliwa na baba yake, Rais Yoweri Museveni.

Moja kwa moja

Ambia Hirsi

  1. Na hapo tunafikia tamati ya habari zetu za leo

  2. Ole Gunnar Solskjaer: Sijali kukosolewa

    Solskjaer

    Chanzo cha picha, Getty Images

    Maelezo ya picha, Solskjaer

    Ole Gunnar Solskjaer anasema kwamba haathiriki na mapendekezo ya kwamba klabu hiyo inafaa kumbadilisha mkufunzi wake ili kuweza kushinda mataji.

    Solskjaer mwenye umri wa miaka 48 , alikuwa akimjibu aliyekuwa beki wa Liverpool Jamie Carragher katika chombo cha habari cha Sky Sports kwamba United inahitaji meneja mpya ili kuweza kupigania mataji.

    ‘’Hainiathiri’’ , alisema Solskjaer.

    ‘’Najiamini mwenyewe , na bora klabu inaniamini. Ninaamini wazo la Jamie Carragher halitabadili hilo’’.

    Solskjaer amekabiliwa na shikinikizo chungu nzima huku timu yake ikiwa katika nafasi ya tano katika ligi ya Premiabaada ya kulazwa 4-2na Leicester City Jumamosi iliopita.

  3. Mtu aanguka kutoka katika puto na kufariki Israel

    AFP

    Chanzo cha picha, AFP

    Maelezo ya picha, Puto

    Mtu mmoja amefariki kaskazini mwa taifa la Israel baada ya kuponyoka kutoka kwa puto au kibofu na kuanguka juu ya gari lililokuwa likiendeshwa.

    Vyombo vya habari vya Israel viliripoti kwamba , mtu huyo ambaye yuko katika mwenye umri wa miaka 20alikuwa mfanyakazi wa ardhini ambaye alikuwa akibembea katika kapu la puto hilobaada ya kupaa.

    Abiria wa puto hilo walijaribu kumvuta ndani , lakini aliponyoka na kuanguka yapata mita 100 hadi katika gari lililokuwa likiendeshwakatika barabara kuu karibu na mji wa Afula.

    Maafisa wa afya walisema kwamba mtu huyo alifariki papo hapo baada ya kuanguka. Watu waliokuwa ndani ya gari hilo hawakuhitaji matibabuhuku abiria waliokuwa katika puto hilo wakitua salama salmin.

    Tukio hilo litachunguzwa na maafisa wa polisina maafisa wa mamlaka ya angani nchini humo.

  4. Afrika Kusini: Chanjo ya Sputnik V huenda inaongeza hatari ya maambukizi ya HIV

    Sputnik V

    Chanzo cha picha, Reuters

    Maelezo ya picha, Sputnik V

    Idara ya udhibiti wa bidhaa za afya nchini Afrika Kusini Sahpra , imezuia matumizi ya chanjo ya Urusi ya Sputnik V kwa hofu kwamba huenda ikaongeza hatari ya maambukizi ya virusi vya HIV miongoni mwa wanaume.

    Uamuzi huo unatokana na tafiti mbili za awali ambazo zilipima usalama wa dawa aina ya adenovirusiliopo katika chanjo hiyo ya Urusi.

    Taasisi ya Gamaleya , iliotengeneza chanjo ya Sputnik V , ilisema kwamba itatoa ushahidi kuonesha kwamba wasiwasi wa Sahpra sio wa kutiliwa maanani.

    Taifa hilo lina idadi kubwa ya watu wanaoishi na maradhi ya HIV barani Afrika . Lina takriban watu milioni 7.8 wenye virusi hivyo katika idadi ya taifa hilo ya watu milioni 60, kulingana na UNAIDS.

    Takriban asilimia 13.5 ya wanaume walio kati ya umri wa miaka 15 na 49 wameambukizwa.

    Shirika la afya Duniani halijaidhinisha chanjo ya Sputnik V kwa matumizi ya dharura. Chanjo hiyo hatahivyo imekuwa ikitumika katika mataifa 45 ikiwemo Zimbabwe na Namibia.

  5. Afrika yahitaji $50bn kwa mwaka kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa

    Afrika imechangia 4% tu ya uzalishaji wa hewa chafu duniani

    Chanzo cha picha, AFP

    Maelezo ya picha, Afrika imechangia 4% tu ya uzalishaji wa hewa chafu duniani

    Ripoti mpya inasema kuwa Afrika inahitaji hadi dola bilioni 50 kwa mwaka ili kukabiliana natisho linaloongezeka la mabadiliko ya hali ya hewa climate change.

    Jumuiya ya Afrika na Shirika la Hali ya Hewa Duniani zinaonya kuwa karibu watu milioni 120 maskini wanakabiliwa na tishio la mafuriko, ukame, makazi yao, na joto kali ifikapo mwishoni mwa muongo huu ikiwa hatua madhubuti hazitachukuliwa.

    Pia inaonya kuwa barafu zilizosalia za barani Afrika ziko zinaelekea kutoweka ifikapo miaka ya 2040.

    Afrika imeathiriwa na mabadiliko ya tabia nchi ijapokuwa inawajibikia asilimia nne tu uzalishaji wa chafu duniani.

  6. Vikosi vya DR Congo vyakabiliana na wanajeshi wa Rwanda

    Jeshi la Rwanda halijajibu madai ya tukio hilo

    Chanzo cha picha, AFP

    Maelezo ya picha, Jeshi la Rwanda halijajibu madai ya tukio hilo

    Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo inasema kuwa vikosi vyake vimekabiliana na wenzao wa Rwanda karibu na mpaka wa mashariki siku ya Jumatatu.

    Msemaji wa jeshi katika Mkoa wa Kivu Kaskazini alisema vikosi vya Rwanda vilivuka mpaka na kuingia Congo katika hatua ambayo ilisababisha makabiliano.

    “Kitengo cha wanajeshi wa Rwanda kiliingia kilomita tano ndani ya Congo…Hauwezi kuelezea jinsi wanajeshi waliojihami walivuka mpaka na kuanza kupiga risasi," Brigedia Jeneral Sylvain Ekenge taliambia BBC Idhaa ya Maziwa Makuu.

    Majeshi ya Rwanda hayajatoa tamko lolote kuhusu madai hayo au kujibu ombi la BBC.

    Ramani

    Video zinazoshirikishwa mitandaoni zinawaonesha wenyeji waliokuwa na hofu wakikimbia huku vikosi hivyo viwili vikikabiliana kwa rasasi. Wanajeshi wa Rwanda baadaye walirudi nyuma na kwenda nyumbani.

    “Kwa bahati nzuri hakuna mtu aliyefariki katika tukio hilo”, Jenerali Ekenge alisema.

    Viongozi na wakazi wa eneo hilo walirejea majumbani mwao baada ya hali ya utulivu kudumishwa.

    Mvutano wa mipaka kati ya majirani hao wawili wa Afrika Mashariki ni jambo la kawaida kwa sababu ya biashara haramu, ukosefu wa mipaka wazi na mashambulio ya waasi.

  7. Uganda yazindua gari la kivita lililoundwa nchini humo

    Ruka X ujumbe
    Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)

    Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue

    Onyo: BBC haihusiki na maudhui ya nje

    Mwisho wa X ujumbe

    Kamanda wa vikosi vya ardhi nchini Uganda, Jenerali Muhoozi Kainerugaba, ameweka kwenye Twitter picha ya kile anachosema kuwa gari la kwanza la kivita kutengenezwa nchini humo.

    Anasema "liliundwa na kutengenezwa ncini Uganda", lakini hakutoa maelezo kuhusu muundo na gharama yake.

    Gari hilo lililopewa jina la Chui - lilizinduliwa na baba yake, Rais Yoweri Museveni.

    Jeshi la Uganda mwaka jana lilihusika katika msako mkali dhidi ya maandamano yaliyotikisa mji mkuu, Kampala, kufuatia kukamatwa kwa mgombea urais Bobi Wine.

    Maafisa walitete utumizi wa silaha za moto, wakisema polisi na jeshi walikua wakikabiliana na waandamanaji.

  8. Khardashian apata mchumba mpya

    Instagram

    Chanzo cha picha, Instagram

    Nyota wa zamani wa kipindi cha televisheni cha maisha halisi, Kourtney Kardashian hatimaye amekubali ombi la uchumba.

    Mpenzi wake ambaye amekuwa naye kwa chini yam waka mmoja Travis Barker alimtaka uchumba na Bi Kourtney hakukataa na kukubali ombi hilo katika hafla iliyofanyika Jumapili ufukweli mwa bahari Jumapili.

    Vyombo vya habari vinasema sherehe hiyo ya uchumba ilihudhuriwa na ndugu wa karibu wa familia pekee.

    Instagram

    Chanzo cha picha, Istagram

    Watu wengi walimpongeza mwanamitindo huyo mwenye umri wa miaka 42 baada ya taarifa ya kuchubiwa kwake kutangazwa na watu wa famialia yake.

    Mwezi Februari 2021, wawili hao waliueleza umma kuwa uchumba kwa , baada ya miezi kadhaa ya tetesi juu ya uhusiano wao.

    Kourtney tayari ana watoto watatu ambao alizaa na mpenzi wake wa awali wa kiume, Scott Disick - Mason, Penelope na Reign katika mahusiano yao yaliyoanza mwaka 2006.

    Instagram

    Chanzo cha picha, Instagram

    Mume ajaye wa Kourtney Kardashian ni nani?

    Travis Barker mwenye umri wa miaka 45 ni nyota wa muziki wa rock ambaye ana miliki bendi inayofahamika kama Blink-182.

    Amewahi kuoa mara mbili awali, ndoa yake ya kwanza alimuoa muigizajiMelissa Kennedy na ya pili alioana na mwanamitindo Shanna Moakler.

    Ana watoto wawili aliowapata katika kipindi cha ndoa yake ya mwisho na Shanna – wenye majina ya Alabamana Lander.

  9. Kanye West abadilisha jina lake kuwa Ye

    Jina lake la awali- Kanye Omari West - halitatumika tena.

    Chanzo cha picha, Getty Images

    Maelezo ya picha, Jina lake la awali- Kanye Omari West - halitatumika tena.

    Msanii wa Marekani aliyekua akijulikana kama Kanye West sasa itajulikana rasmi kama wewe tu.

    Jaji wa Los Angeles aliridhia ombi la rappa huyo kubadilisha jina, afisa mawasiliano katika Mahakama Kuu ya Los Angeles alithibitisha.

    Nyota huyo wa miaka 44-aliwasilisha ombi hilo mwezi Agosti, akitoa "sababu za kibinafsi."

    Rapa huyo, anayejulikana sana kwa vibao kama vile Gold Digger na Stronger, alikua akitumia Ye kama jina la utani na mnamo 2018 alilitumia kama jina la albamu.

    Muda mfupi baada ya kutolewa kwa albamu hiyo, alitweet: "Kujulikana rasmi kama Kanye West. Mimi ni YE."

    Sasa amelifanya rasmi na jina lake la awali- Kanye Omari West - halitatumika tena.

    Ijapokua jina la Ye tayari lilikua likitumia kwenye Twitter, akaunti yake ya Instagram na wavuti yake bado inatumia jina lake la zamani kufikia Jumanne.

    "Ninaamini 'Ye' ni neno linalotumiwa sana katika Biblia, na katika Biblia linamaanisha wewe. Kwa hivyo mimi ni wewe, mimi ni nyinyi, yaani ni sisi," alisema katika mahojiano ya 2018 na mtangazaji wa redio Big Boy.

    Wasnii wengine waliobadilisha jina ni Prince, Snoop Dogg na Sean Love Combs, wengine wao mara kadhaa.

  10. Genge la majambazi wa Nigeria lakamatwa Afrika Kusini- ripoti

    Vyombo vya sheria vya Afrika Kusini na Markani vimewakamata wanachama sita wa genge la majambazi wa Black Axe huko Cape Town, tovuti ya habari ya TimesLive inaripoti.

    Kundi hilo , linaaminika kuhusika na mamia ya “Matapeli wa mapenzi”, liliripotiwa kukamatwa katika msako mapema Jumanne asubuhi.

    Black Axe pia inadaiwa kulaghai makampuni mamilioni ya pesa kupitia uhalifu wa kimtandao ikihusisha biashara ya barua pepe za ulaghai.

    Kundi hilo liliibuka miaka ya 1970 huko Nigeria ambapo lilifanya ubakaji, ukeketaji na mauaji ya kikatili. Wanachama wake waliendelea kujenga mtandao wenye nguvu wa kimataifa.

    Lina uwepo mkubwa nchini Italia. Wanachama wake kadhaa walikamatwa nchini humo mwezi Aprili na kufunguliwa mashtaka karibu 100 ikiwa ni pamoja na biashara ya dawa za kulevya na ulanguzi wa watu, ukahaba na ulaghai wa mtandao.

  11. Waziri Mkuu wa Sudan aunda jopo maalum kushughulikia mzozo wa kisiasa

    Abdalla Hamdok announced the committee during a special cabinet meeting on Monday

    Chanzo cha picha, AFP

    Waziri Mkuu wa Sudan Abdalla Hamdok amebuni "jopo maalum" kusuluhisha kile alichotaja kuwa mzozo "hatari zaidi" wa kisiasa nchini humo tangu mapinduzi ya kijeshi ya mwaka 2019, shirika la habari la serikali la Suna limeripoti.

    Bw. Hamdok ametangaza jopo, ambalo linajumuisha wanachama kutoka makundi pinzani ya kisiasa, wakati wa mkutano wa "dharura" wa baraza la mawaziri siku ya Jumatatu mjini Khartoum.

    Ametoa wito wa uvumilivu na kujadiliana kwa amani ili kukomesha wiki kadhaa za taharuki ya kisiasa ambayo imetishia kuvuruga utawala wa awamu ya mpito kuelekea uaongozi wa kidemokrasi.

    Kauli yake inajiri baada ya polisi kuwatawanya waandamano wanaounga mkono utawala wa kijeshi ambao wanashinikiza kuvunjwa kwa serikali ya mpito.

    Maandamano yalianza Oktoba 16 mbele ya Ikulu ya rais kutaka jeshi lichukue madaraka.

    • Kiongozi wa baraza la kijeshi la mpito nchini Sudan ameapa ''kuung'oa utawala
    • Omar al-Bashir: Namna kiongozi mwenye mamlaka makubwa ya kijeshi alivyodumu mamlakani
    • Mapinduzi Mali: Je mapinduzi ya kijeshi yanaongezeka Afrika?
  12. Tigray: Serikali ya Ethiopia yakiri kutekeleza shambulio la angani Mekelle

    Watu ndani ya jiji la Mekelle waliripoti mashambulizi ya angani Jumatatu

    Chanzo cha picha, Getty Images

    Maelezo ya picha, Watu ndani ya jiji la Mekelle waliripoti mashambulizi ya angani Jumatatu

    Ethiopia imekiru kuhusika na shambulio la angani dhidi ya mji mkuu wa eneo la Tigray linalokumbwa na mzozo - saa kadhaa baada ya kupinga kile kilichodaiwa na waasi kuwa shambulio hatari.

    Shirika la habari la serikali limesema mashambulio hayo yalilenga mashambulio mawasiliano na vifaa vya waasi.

    Lakini kituo ch ahabari kinachodhibitiwa na Tigray People's Liberation Front (TPLF) kilisema raia watatu waliuawa

    Kundi hilo la waasi limekuwa lipigana na serikali ya Ethiopia kwa karibu mwaka mmoja.

    Awali serikali ilikua imepinga madai kwamba imeshambulia mji mkuu wa he Tigray, Mekelle.

    "Kwa nini serikali ya Ethiopia ilishambulia mji wake? Mekelle ni mji wa Ethiopia," msemaji wa serikali Legesse Tulu aliuliza.

    Wizara ya Mambo ya Nje ya Ethiopia iliendelea kuishutumu TPLF kwa kuua raia wasiopungua 30 katika mashambulio ya hivi karibuni katika majimbo ya Amhara na Afar, ambayo yote yanapakana na Tigray.

    "Magaidi ndio wanaoshambulia miji na raia wasio na hatia wala sio serikali," Bw Legesse aliongeza.

  13. Wasomali "watishiwa kifo" kufuatia mauaji ya Mbunge wa Uingereza

    Maombolezo ya Mbunge wa Uingereza aliyeuawa Londona Ijumaa iliyopita

    Chanzo cha picha, Getty Images

    Shirika moja linalowasiadia Wasomali wanaoishi nchini Uingereza linasema kuwa wanachama wake wamekua wakitishiwa kifo tangu Mbunge wa Uingereza Sir David Amess kuuawa.

    Sir David alichomwa kisu mara kadhaa Ijumaa iliyopita alipokuwa akikutana na wakazi wa eneo bunge la Southend West.

    Ali Harbi Ali, 25, Muingereza mwenye asili ya Kisomali, anazuiliwa chini ya sheria ya Ugaidi kwa kushukiwa kuhusika na mauaji hayo.

    Baba yake, Harbi Ali Kullane, aliwahi kuwa mshauri wa Waziri Mkuu wa Somalia.

    Mwakilishi wa Baraza la Mashirika ya Wasomali (CSO) amemuambia mwandishi wa BBC Charlotte Gallagher kwamba Wasomali na watu wenye asili ya Kisomali wamekua wakipokea vitisho vya kuuawa tangu mauaji hayo.

    Baadhi ya klabu za vijana na vituo vya kijamii pia vimefungwa kwa sababu ya vitisho hivyo na watu wamekua wakiishi kwa uwoga, anasema Kahiye Alim.

    Bw Alim anasema kwamba hafahamu familia ya mshukiwa lakini anamjua baba yake kutokana na kazi aliyofanya zamani kama mshauri wa Waziri Mkuu wa Somalia.

    Amesema jamii ya Wasomali nchini Uingereza imegutushwa na mauaji hayo.

  14. Rais Buhari ahimiza utulivu baada ya shambulio lililowaua watu zaidi ya 40 Nigeria

    Ramani

    Rais wa Nigeria Muhammadu Buhari ametuma risala za rambi rambi kwa familia za watu waliouawa katika shambulio kwenye soko la kijiji katika jimbo la kaskazini magharibi la Sokoto.

    Serikali ya jimbo la Sokoto ilisema watu 43 walifariki katika shambulio la Jumapili jioni baada ya watu wenye silaha kuvamia soko la wazi katika mji wa Goronyo.

    Katika taarifa yake, Rais Buhari anatoa wito kwa Wanigeria "wasikate tamaa" lakini "waendelee kuwa na subira" kwani mamlaka "zimeazimia zaidi kuliko hapo awali kuwalinda Wanigeria".

    Serikali yake imekosolewa vikali kwa kushindwa kukabiliana na ukosefu wa usalama ulioenea nchini, na mauaji na utekaji nyara unaotekelezwa na vikundi vyenye silaha vinaongezeka.

    Mashambulio yameendelea licha ya kupelekwa kwa maelfu ya maafisa wa vikosi vya usalama na pia kuzuiwa kwa mtandao na huduma za simu za rununu katika sehemu nyingi za kaskazini magharibi mwa nchi hiyo.

  15. Mpiga mbizi apata upanga uliodumu miaka 900 katika pwani ya Israel

    Once cleaned, the blade will be put on public display

    Chanzo cha picha, Reuters

    Upanga unaoaminika kuwa wa mpiganaji wa zamani wa vita ya waasi takribani miaka 900 iliyopita umepatikana na mzama maji katika pwani iliyoko kaskazini mwa Israel.

    Upanga huo wenye futi 3.3 uligunduliwa na Shlomi Katzin na kukabidhiwa na mamlaka.

    Inadhaniwa kuwa upanga huo ambao ulikuwa baharini kwa muda mrefu umeonekana baada ya mchanga kuhama.

    Mamlaka ya masuala ya kale nchini Israel (IAA) imesema upanga huo utakaposafishwa na kufanyiwa uchunguzi wa kina utawekwa katika maonesho ya umma.

    "Upanga ambao umehifadhiwa katika hali nzuri , unavutia, ni uvumbuzi wa nadra na dhahiri kuwa ulikuwa wa shujaa wa vita," alisema afisa wa kitengo cha uchunguzi cha IAA.

    "Inafurahisha kukutana na kitu cha mtu kama hicho ambacho kinaturudisha miaka 900 iliyopita , wakati ambao silaha kubwa za kijeshi zilikuwa mapanga na visu”.

    Wapiganaji waliopigana vita za kidini walifahamika kama ‘vita vya msalaba’ na vilihusisha kanisa katoliki.

    Katika kampeni hizo, mashariki mwa bahari ya Mediterania wakilenga kugundua mji mtakatifu kutoka kwa utawala wa kiislamu.

  16. Karibu katika matangazo ya moja kwa moja leo Jumanne 19.10.2021.