Mzozo wa utekaji nyara Nigeria: Barua zilivyochukua nafasi ya simu

A man and a woman in Nigeria using mobile phones

Chanzo cha picha, Getty Images

Katika msururu wa barua kutoka kwa waandishi wa Afrika, Mannir Dan Ali, mhariri mkuu wa zamani wa gazeti la Daily Trust nchini Nigeria, anatathmini athari ya mbinu ya hivi karibuni ya kukabiliana na magenge hatari ya utekaji nyara - kukatiza mawasiliano ya simu na huduma za intaneti.

Short presentational grey line

Katika kipindi cha miaka kadhaa iliyopita maisha ya wakazi wa maeneo ya vijijini kaskazini -magharibi mwa jimbo la Zamfara yamekuwa ya madhila.

Magenge yaliyojihami kwa bunduki na yanayotumia piki piki kuendesha shughuli zao yanashikilia eneo la karibu kilo mita 39,761 mraba -eneo ambalo linaweza kulinganishwa na nchi kama Burundi, Lesotho na Rwanda kwa ukubwa - kutekeleza mauaji, ubakaji na utekaji nyara kwa lengo la kuitisha kikombozi.

Wanachama wa magenge hayo wameimarisha mipango yao, mara nyingi wanavalia sare za kijeshi kuwachanganya wanavijiji na baadaye kuwashambulia.

Hili tatizo limekuwepo kwa miaka kadhaa sasa, na imesambaa hadi karibu majimbo matano jirani.

Mikakati tofauti imezinduliwa katika eneo la Zamfara ili kukomesha msururu wa mashambulio ya kifaidi ikiwa ni pamoja na:

  • Msamaha kwa wanachama wa magenge ya uhalifu watakaojisalimisha.
  • Kuzuia ndege kupaa katika maeneo fulani - licha yamadai kwamba helikopta zilikuwa zikiwapelekea silaha majambazi.
  • Na marufuku ya shughuli za uchimbaji madini baada yadhahabu kudaiwa kutumiwa na watekaji nyara.

Lakini hatua hizi hazijaleta mabadiliko yaliyotarajiwa, sasa mamlaka katika jimbo la Zamfara zimepiga marufuku uuzaji wa mifugo pamoja na soka la kila wiki ambapo wakulima na wafanyabiashara wanaendesha shughuli zao. Kuiba mifuga ni moja ya njia kuu inayotumiwa na majambazi hao kujipatia kipao.

Hatua kali zaidi imekuwa ya kuzima minara yote 240 ya simu za rununu katika jimbo la Zamfara .

Lengo ni kuwanyima wahalifu njia za mawasiliano na watoa habari wao na kujadili ukombozi na familia za waliotekwa nyara.

Oparesheni ya kijeshi pia imeianzishwa katika eneo hilo.

Mannir Dan Ali
M Dan Ali
I personally chose to move my mother away from her home recently - and just a few days ago, three university students were abducted less than a kilometre from her house"
Mannir Dan Ali
Journalist
1px transparent line

Hatua ya kuzimwa kwa simu- ambayo pia imeathiri jamii kwenye mipaka ya Zamfara na majimbo mengine - inakuja kwa gharama kubwa kwa familia na wafanyabiashara.

Kitu kidogo ambacho kingelishughulikiwa kwa simu moja sasa inachukua safari ya siku nzima kukitekeleza.

Baadhi ya watu wameamua kuandika barua. Kwa kua hakuna mfumo wa posta unaoanya kazi, barua hizo zinawasilishwa kupitia mabasi yanayosafiri kati ya miji yajimbo hilo na maeneo mengine nchini.

Mzaliwa wa Zamfara- na mkazi wa Abuja, amenifahamisha jinsi alivyopata usumbufu wa akili kwa kuwa hajui kama jamaa zake wako salama .

Ni hivi majuzi tu mmoja wao alipowasili Abuja ndipo nilipata taarifa kuhusu hali zao.

Mwengine aliniambia kwamba ana wasiwasi, na kwamba atasafiri Zamfarahivi karibuni kujulia hali familia yake

Magenge 'yanaendeshwa kwengine'

Licha ya shida zinazosababishwa na kuzimwa kwa simu, majadiliano kwenye vipindi vya mazungumzo vya redio huko Abuja yanaunga mkono hatua hiyo.

Map of Nigeria

Mmoja wa wakazi wa jimbo hilo anayeishi katika mji mkuu alisema ni heri wavumilie kipindi kifupi cha tabu badala ya vurugu za kila siku ambazo zimegeuza Zamfara kuwa jangwa la watu wenye silaha wanatawala.

Kwa sasa hakuna anayejua oparesheni dhidi ya wahalifu katika jimbo la Zamfara inavyoendeshwa.

Hata wanahabari hawana njia ya kuthibitisha taarifa kuhusu hali ilivyo katika jimbo hilo.

Ripota mmoja aliniambia amekuwa akijaribu kushawishi mamlaka kumruhusu kujiunga na wanajeshi.

line