Je, washirika wa karibu wa Trump kote duniani ni akina nani?

Kama ilivyo desturi ya kidiplomasia, pongezi zilimiminika kwa Donald Trump kutoka duniani kote baada ya kutangazwa kuwa mshindi wa uchaguzi. Lakini je, ni akina nani marafiki na washirika wake kote duniani?

Muhtasari

Moja kwa moja

Na Asha Juma, Yusuf Jumah & Dinah Gahamanyi

  1. Na mpaka hapo ndio tunafikia mwisho wa matangazo haya ya mubashara, tukutane tena hapo kesho majaaliwa.

  2. 'Tunatumai kuwa Marekani itaimarika zaidi'- Zelensky

    g

    Chanzo cha picha, EPA

    Rais wa Ukraine amesema uhusiano kati ya Marekani na bara la Ulaya "lazima uthaminiwe na hauwezi kupotea" baada ya ushindi wa Donald Trump katika uchaguzi wa Marekani.

    Akizungumza katika mkutano wa kilele wa viongozi wa Ulaya mjini Budapest, Volodymyr Zelensky amesema: "Tunatumai kuwa Marekani itaimarika zaidi."

    "Hii ndiyo aina ya Amerika ambayo Ulaya inahitaji," amesema. "Na Ulaya yenye nguvu ndiyo ambayo Amerika inahitaji - huu ni uhusiano kati ya washirika ambao lazima uthaminiwe na hauwezi kupotea."

    Kulingana na shirika la habari la AFP, Zelensky pia ameuambia mkutano huo kuwa "haitakubalika kwa Ukraine" ikiwa kiongozi wa Urusi Vladimir Putin atapewa makubaliano yoyote.

    Vita vya Ukraine: Mengi zaidi

  3. Raia wa Ghana walalamika baada ya rais kuzindua sanamu yake mwenyewe

    g

    Chanzo cha picha, Citi Newsroom

    Maelezo ya picha, Picha za sanamu hiyo zimesambaa nchini Ghana

    Rais wa Ghana anayemaliza muda wake Nana Akufo-Addo anakabiliwa na mzozo kwenye mitandao ya kijamii baada ya kuzindua sanamu yake alipokuwa katika ziara ya Ukanda wa Magharibi mwa nchi hiyo.

    Sanamu hiyo imesimikwa kwa heshima ya mipango ya maendeleo ambayo Rais amesimamia akiwa madarakani, Waziri Kwabena Okyere Darko-Mensah alisema.

    Lakini Waghana wengi wamekuwa wakidhihaki usimikwaji wake nje ya hospitali katika jiji la Sekondi – wanaiona kama njia ya "kujitukuza".

    "Watu wa Ukanda wa Magharibi wanastahili jambo bora zaidi ya maonyesho ya kujionyesha ," Mbunge wa upinzani Emmanuel Armah Kofi-Buah alichapisha kwenye X.

    Akufo-Addo, ambaye atang'atuka madarakani Januari baada ya mihula miwili madarakani, amejigamba kuwa ametimiza asilimia 80 ya ahadi zake kwa Waghana.

    Alizindua sanamu hiyo iliowekwa mbele ya hospitali ya Effia-Nkwanta ya jimbo la Sekondi , Jumatano wakati wa ziara yake ambayo imepewa jina la "safari ya shukrani".

    Katika hafla hiyo, Darko-Mensah, ambaye anasimamia Kanda ya Magharibi, aliangazia miradi kadhaa muhimu iliyoanzishwa chini ya rais.

    Lakini sanamu hiyo imezua wimbi la ukosoaji, huku baadhi ya Waghana wakihoji umuhimu wake wakati miradi kadhaa muhimu haijakamilika.

  4. Hawa ndio washirika wa karibu wa Trump kote duniani

    g

    Chanzo cha picha, Reuters

    Kama ilivyo desturi ya kidiplomasia, pongezi zilimiminika kwa Donald Trump kutoka duniani kote baada ya kutangazwa kuwa mshindi wa uchaguzi. Hebu tuangalie baadhi ya marafiki wa karibu wa Trump na washirika wake:

    Benjamin Netanyahu, Waziri Mkuu wa Israel: "Kurejea kwa historia kubwa"

    • Trump alisemekana kusikitika wakati Netanyahu alipopongeza ushindi wa Biden mwaka 2020, lakini anasisitiza kuwa wana "uhusiano mzuri sana"

    Viktor Orbán, Waziri Mkuu wa Hungary: "Ushindi unaohitajika sana kwa ulimwengu!"

    -kama "mmoja wa watu wanaoheshimika zaidi" duniani.

    • Mapema mwezi huu, Orbán alisema: "Tutafungua chupa kadhaa za champagne ikiwa Trump atarudi". Trump awali alimuelezea Orbán -ambaye anatuhumiwa kuwa kiongozi wa kimabavu na

    Giorgia Meloni, Waziri Mkuu wa Italia: "Kazi nzuri, Mheshimiwa Rais"

    • Meloni alimpigia simu Trump Jumatano usiku kumpongeza na kuthibitisha "urafiki wao wa kina na wa kihistoria", aliandika kwenye mtandao wa X

    Javier Milei, Rais wa Argentina: "Unaweza kuitegemea Argentina kuifanya Marekani kuwa kubwa tena"

    • Akizungumzia kumhusu Milei katika mkutano wa hadhara mwezi Machi, Trump alisema: "Ni mtu mkubwa kwa Trump. Anampenda Trump, nampenda, kwa sababu anampenda Trump."

    Unaweza pia kusoma:

  5. Je, nani anaweza kuwa katika baraza la mawaziri la Trump?

    g

    Chanzo cha picha, Getty Images

    Maelezo ya picha, Trump na mmoja wa wasimamizi wake wawili wa kampeni, Susie Wiles, wakitazama mchezo wa soka wa New York Jets dhidi ya Pittsburgh Steelers tarehe 20 Oktoba.

    Wakati wa kampeni yake, Donald Trump alitoa ahadi chache – baadhi kuu kuliko nyingine - kuhusu nani anataka kumuona katika utawala wake. Je ni nani anayeweza kumteua amsaidie katika muhula wake wa pili:

    Susie Wiles: Ameonekana kuwa na mchango mkubwa katika kinyang'anyiro cha urais wa Trump, na anaweza kuwa mkuu wake wa majeshi . Aliyekuwa mshauri wa sera za ndani Brooke Rollins pia anachukuliwa kuwa mtu anayeweza kutekeleza jukumu hilo.

    Robert F Kennedy Jr: Trump alisema - ikiwa atachaguliwa - mgombea binafsi wa zamani na mtu anayetilia shaka chanjo anaweza kumteua . Lakini haijahakikishiwa kuwa Seneti ingemthibitisha Kennedy katika wadhifa wa baraza la mawaziri.

    Mike Pompeo: Mkurugenzi wa zamani wa CIA na waziri wa mambo ya nje katika urais wa wa awali wa Trump anatajwa kuwa miongoni mwa wale wanaowania kuwa waziri wa ulinzi .

    Ric Grenell: Aliwahi kuwa balozi wa Marekani nchini Ujerumani na kaimu mkurugenzi wa ujasusi wa kitaifa katika utawala wa mwisho wa Trump. Anachukuliwa kuwa mtu anayewania kuwa katibu wa serikali au mshauri wa usalama wa kitaifa .

    Elon Musk: Tumeona na kusikia mengi ya Elon Musk - mtu tajiri zaidi duniani alihusiaka sana katika uchaguzi huu. Trump alidokeza kumpa Musk jukumu lisilo la Baraza la Mawaziri katika utawala wake kusaidia kuondoa taka za serikali katika kile bilionea huyo aliita " Idara ya Ufanisi wa Serikali.’’

    Soma zaidi:

  6. Mataifa sita kushiriki katika mashindano ya kimataifa ya chess nchini Tanzania,

    g

    Wachezaji wa Chess kutoka nchi sita, yakiwemo Tanzania, Poland, Ujerumani, India, Nigeria na Msumbiji, wanatarajiwa kuchuana katika shindano la kupanda viwango la Shirikisho la Kimataifa des Echecs (FIDE).

    Mashindano hayo yanayofanyika Desemba 14 na 15, ni mashindano ya mara ya nne ya kufanyika katika Chuo Kikuu cha Jordan mjini Morogoro mashariki mwa Tanzania.

    Waandaaji wanajivunia uwepo wa timu hizo za kimataifa katika mashindano hayo, huku wakionyesha umuhimu wake katika kuinua hadhi ya Tanzania katika mchezo wa chess.

    "Tunafuraha kuwa mwenyeji wa mashindano ya mwaka huu ambapo tayari tuna mataifa sita yamedhibitisha kushiriki," alisema Dkt Konrad Czernichowski, mmoja wa waandaaji na pia ni mhadhiri katika Chuo Kikuu cha Jordan cha Morogoro.

    Dkt Konrad aliongeza kuwa, “Pamoja na washiriki kutoka mataifa sita, ni fursa ya kipekee kuinua Tanzania kwenye jukwaa la dunia la mchezo wa chess. Viwango vya Chess sio nambari tu ni onyesho la ustadi, kujitolea, na huwa na hadhi ya kimataifa.”

    Kabla ya kuanza kwa michuano hiyo, mchezaji wa mchezo wa chess kutoka Tanzania, Shedrack Mwakajila, ambaye hivi karibuni aliiwakilisha nchi yake kwenye Olympiad ya Chess mjini Budapest, alitembelea Klabu ya Jordan Chess na kucheza mchezo huo na wachezaji mbalimbali

    Katika ziara yake, nyota huyo alikabiliana na wachezaji wengi mara moja dhidi yake na baadaye kucheza dhidi ya mchezaji mmoja mmoja. Wapinzani wawili tu ndio waliibuka washindi; mwanafunzi wa chuo hiko Inocent Agustino Herman na Dkt Konrad.

    Dkt Konrad alimsifu Mwakajila kama mfano mzuri wa kuigwa na wachezaji chipukizi nchini Tanzania.

    Kwa mujibu wa Dkt Konrad pamoja na washiriki wa kimataifa na fursa ya kupata viwango vya FIDE, mashindano ya Desemba yanatarajiwa kukuza wasifu wa chess wa Tanzania, kuwapa wachezaji wa ndani jukwaa la kimataifa na kuhamasisha vijana zaidi kujihusisha na mchezo huo.

    Chess ni mchezo wa aina gani?

    h

    Wataalamu wa elimu wametaja mchezo wa Chess kuwa wenye umuhimu mkubwa katika kukuza vipaji, uwezo wa kufikiria kwa undani na kusuluhisha matatizo yanayokumba jamii, na ubunifu.

  7. Matokeo ya uchaguzi Marekani 2024: Waendesha mashtaka waanza kutupilia mbali mashtaka ya Trump

    d

    Chanzo cha picha, Getty Images

    Wizara ya sheria na mwendesha mashtaka maalum wa Marekani Jack Smith, wako katika majadiliano kuhusu jinsi ya kumaliza mashtaka dhidi ya Donald Trump, shirika la habari washirika na BBC la CBS linaripoti.

    Vyanzo vinataja sera ya muda mrefu ya kutomshtaki rais aliyeko madarakani.

    Smith kwa sasa anaongoza kesi nyingi dhidi ya Trump, ambaye atakuwa rais wa kwanza kuchukua madaraka wakati akikabiliwa na kesi kadhaa.

    Hii ni pamoja na kesi ya madai ya matumizi mabaya ya nyaraka za siri, na ile inayohusu juhudi zake za kubatilisha kushindwa kwake kwa uchaguzi wa 2020 ambapo Joe Biden alishinda.

    f

    Chanzo cha picha, Getty Images

    Unaweza pia kusoma:

  8. Droni za Shahid zaupiga mji mkuu wa Ukraine usiku kucha Kyiv wakati wa shambulio la drone usiku kucha

    g

    Chanzo cha picha, Reuters

    Maelezo ya picha, Droni za Shahid zaupiga mji mkuu wa Ukraine usiku kucha Kyiv wakati wa shambulio la drone usiku wa Novemba 7

    Urusi imefanya mashambulizi ya ndege zisizokuwa na rubani aina ya shahed usiku kuanzia saa sita katika mji mkuu Kyiv. Tahadhari ya mashambulizi ya anga ilidumu kwa muda wa saa nane ambapo onyo lilitangazwa usiku wa manane, na kurushwa - saa nane asubuhi.

    Wanajeshi wa Urusi walishambulia mji mkuu huo kwa kutumia ndege zisizo na rubani. Mabaki ya ndege hizo zinazojulikana kama UAVs yalianguka kwenye nyumba za kibinafsi, karakana, vituo vya biashara, vituo vya matibabu, na Barabara.

    Watu kadhaa walijeruhiwa na kupelekwa hospitali kufuatia mashambulizi hayo.

    Ni wilaya gani za Kyiv zilizoathiriwa

    g

    Chanzo cha picha, State Emergency Service

    Maelezo ya picha, Moto ulizuka Kyiv kutokana na shambulio la ndege zisizo na rubani usiku

    Ripoti za kwanza za meya wa Kyiv kuhusu mashambulizi ya droni hizo zilizoanguka zilionekana saa mbili asubuhi.

    Kutokana na shambulio la usiku kucha mjini Kyiv, wilaya tano ziliharibiwa, na kuna majeruhi.

    Gereji iliungua moto katika wilaya ya Holosiivskyi, wimbi la shambulio hilo liliharibu vyumba kadhaa katika jengo la makazi. Moto ulizuka katika kituo cha huduma karibu, gazeti la Vitaliy Klitschko liliripoti.

    Makombora ya Ukraine

    Kwa jumla, wakati wa usiku huo, jeshi la anga la Ukraine lilipiga ndege 36 zisizo na rubani za Urusi za UAVs katika mikoa ya Odesa, Mykolaiv, Kyiv, Sumy, Kirovohrad, Zhytomyr, Cherkasy, Chernihiv na Zaporizhia.

    Miundombinu ya reli pia iliharibiwa, haswa vipengele vya usambazaji wa umeme na nyimbo.

    Vita vya Ukraine: Mengi zaidi

  9. Australia inapanga kupiga marufuku kuingia kwenye mitandao ya kijamii kwa watoto chini ya miaka 16

    .

    Chanzo cha picha, Getty Images

    Serikali ya Australia inasema itaanzisha sheria ya kupiga marufuku watoto walio chini ya umri wa miaka 16 kuingia kwenye mitandao ya kijamii ambayo "itakuwa mfano wa kuigwa duniani"

    Waziri Mkuu Anthony Albanese alisema sheria zinazopendekezwa, zitakazowasilishwa bungeni wiki ijayo, zinalenga kupunguza "athari" za mitandao ya kijamii ambayo yanawapata watoto nchini Australia.

    "Hii ni ya akina mama na akina baba... Wao, kama mimi, wana wasiwasi kuhusu usalama wa watoto wetu mtandaoni. Nataka familia za Australia zijue kwamba serikali inawaunga mkono," alisema.

    Ingawa maelezo mengi bado hayajajadiliwa, serikali ilisema marufuku hiyo haitatumika kwa vijana ambao tayari wako kwenye mitandao ya kijamii.

    Soma zaidi:

  10. Je, mchakato wa kipindi cha mpito wa kukabidhiana madaraka ukoje?

    .

    Chanzo cha picha, Getty Images

    Rais mteule Donald Trump ataapishwa kuwa rais tarehe 20 Januari 2025.

    Ni wakati huu ambapo kisheria atachukua mamlaka na majukumu ya urais.

    Kabla ya Januari, mchakato wa kuhesabiwa kwa kura za wawakilishi maalum ndio unaoendelea.

    Kila jimbo kwa ujumla hutoa kura za wawakilishi kwa yeyote atakayeshinda wingi wa maarufu. Hii itathibitishwa tarehe 17 Desemba.

    Bunge jipya la Marekani kisha litakutana tarehe 6 Januari kuhesabu kura za wawakilishi na kuthibitisha matokeo, hivyo kuthibitisha rasmi rais ajaye.

    Ilikuwa ni sehemu hii ya mchakato ambao wafuasi wa Trump walijaribu kusitisha walipovamia Ikulu ya Marekani mnamo 2021 baada ya kukataa kukubali kushindwa na Joe Biden.

    .

    Soma zaidi:

  11. Trump ameshinda - lakini hatakuwa katika Ikulu ya White House kwa siku 74

    TH

    Chanzo cha picha, Reuters

    Wakati Donald Trump amepata ushindi unaomrejesha Ikulu ya White House, bado si rais rasmi - na itachukua zaidi ya miezi miwili kabla ya kurejea katika Ofisi ya Oval.

    Makabidhiano ya madaraka ya Marekani ni tofauti sana na jinsi mambo yanavyofanyika nchini Uingereza. Mnamo Julai, Sir Keir Starmer aliapishwa kama waziri mkuu ndani ya saa chache baada ya uchaguzi kumalizika na kabla ya Rishi Sunak hata kubeba vitu vyake.

    Trump ataapishwa Januari 20 na Joe Biden atasalia madarakani hadi wakati huo - ingawa atakuwa na kikomo cha kisiasa katika kile anachoweza kufanya.

    Soma zaidi:

  12. Trump anapaswa kuiruhusu Ukraine kushambulia maeneo lengwa Urusi - balozi wa zamani

    .

    Chanzo cha picha, EPA

    Balozi wa zamani wa Donald Trump wa Nato anasema anatumai "ataruhusu Ukraine kushambulia vikosi vya [Urusi] upande wa pili wa mpaka" ili kumaliza mkwamo wa vita.

    Akizungumza na BBC, Kay Bailey Hutchinson alisema serikali ya Kyiv inapaswa kulenga "kupata makubaliano ambayo yatawapendelea" baada ya mazungumzo na Trump.

    Siku za nyuma, Trump alikosoa kiasi cha matumizi ya misaada ambayo Marekani imejitolea kwa Ukraine chini ya Joe Biden, na inaonekana kwa kiasi kikubwa kutounga mkono juhudi za vita za Ukraine.

    Hutchinson pia anasema Trump atatafuta kuhakikisha "biashara huria na ya haki" na China, au kurudisha viwanda nchini Marekani ili kubuni fursa za ajira nyumbani.

    Pia unaweza kusoma:

  13. Je, Harris atakuwa na kazi baada ya kushindwa uchaguzi?

    .

    Chanzo cha picha, Reuters

    Kamala Harris ataendelea kutumikia kipindi chake kilichosalia kama makamu wa rais pamoja na Rais Joe Biden, hadi wakati wa makabidhiano ya madaraka kwa Donald Trump na JD Vance tarehe 20 Januari.

    Lakini baada ya Rais-Mteule Trump na Makamu wa Rais-Mteule JD Vance kuapishwa, wote wawili Biden na Harris hawatakuwa na nafasi yoyote ya kisiasa katika serikali ya Marekani.

    Tofauti na siasa za Uingereza, hakuna nafasi sawa ya "kiongozi wa upinzani" - Harris atakuwa hana kazi. Na si kwamba hawezi kupata fursa zingine.

    Soma zaidi:

  14. Trump amesema atafanya nini mara moja?

    th

    Chanzo cha picha, Reuters

    Donald Trump ataapishwa kama rais tarehe 20 Januari . Baadhi ya ahadi zake zinaangazia kile anachonuia kutimiza katika siku yake ya kwanza ofisini, au hata kabla - haya hapa ni baadhi ya yale anayosema kuwa amepanga kuyafanya mara moja:

    Kumaliza vita nchini Ukraine: "Hivyo ni vita ambavyo vinakaribia kutatuliwa. Nitaipata suluhu kabla hata sijawa rais. Nikishinda, nikiwa rais mteule, na nitakachofanya ni kusema na mmoja kisha nitazungumza na mwingine, nitawaleta pamoja,” Trump alisema wakati wa mjadala wake na Harris wakati wa kampeni.

    Mnamo 2023, aliiambia CNN: "Ikiwa nitakuwa rais, vita hivyo vitatatuliwa kwa siku moja, masaa 24."

    Mabadiliko ya uhamiaji: Trump amesema kwamba siku ya kwanza atatia saini amri ya rais kuhakikisha "watoto wahamiaji haramu hawatapata uraia wa Marekani moja kwa moja".

    Alipoulizwa mwaka wa 2023 na Fox News atatumia vibaya mamlaka yake au kuwalenga wapinzani wa kisiasa, Trump alijibu: "Hapana, hapana, hapana, kando na siku ya kwanza. Tunafunga mpaka, na baada ya hapo mimi sitakuwa dikteta."

    Pia amesema "atazindua mpango mkubwa zaidi wa kuwafukuza wahalifu katika historia ya Marekani" siku ya kwanza.

    Maliza kesi ya jinai ya Januari 6: Wakili maalum Jack Smith alifungua mashtaka ya jinai dhidi ya Trump mwaka jana kutokana na juhudi zake za kubatilisha matokeo ya uchaguzi wa 2020. Kesi hiyo imekuwa katika mkanganyiko wa kisheria tangu Mahakama ya Juu ilipotoa uamuzi kwamba Trump alikuwa na kiasi fulani cha kinga dhidi ya kushtakiwa kwa makosa ya jinai kutokana na hatua alizochukua akiwa ofsini rasmi akiwa madarakani.

    Smith alidai kuwa majaribio ya Trump kubadilisha matokeo ya uchaguzi hayakuhusiana na majukumu yake rasmi. Trump anasema anaamini uamuzi wa Mahakama ya Juu umempa kinga, lakini pia amesema haya kumhusu Smith- "nitamfukuza ndani ya sekunde mbili."

    .

    Soma zaidi:

  15. Obama: 'Mimi na Michelle twajivunia Harris na Walz'

    th

    Chanzo cha picha, Getty Images

    Rais wa zamani wa Marekani Barack Obama na mke wake Michelle Obama, wametoa pongezi zao kwa rais mteule Donald Trump na mgombea mwenza wake, JD Vance, kwa ushindi wao.

    "Kwa hakika haya si matokeo tuliyotarajia, kutokana na kutoelewana kwetu na tiketi ya Republican katika masuala mengi," walisema wawili hao, lakini wakaongeza: "Kuishi katika demokrasia ni kutambua kwamba maoni yetu siku zote hayatashinda, na kuwa tayari kukubali makabidhiano madaraka kwa amani."

    Aidha, Obama na mkewe wanasema wanafahari sana na wanajivunia juhudi za Kamala Harris na mgombea mwenza wake Tim Walz - "watumishi wawili wa ajabu wa umma ambao waliendesha kampeni ya kipekee".

    Obama anasema maswala kama janga la Corona na kupanda kwa bei za bidhaa vilileta changamoto kwa tawala za kidemokrasia kote ulimwenguni," na Marekani haikusazwa katika hilo.

    Anasema matatizo haya yanaweza kusuluhishwa, "lakini tu ikiwa tutasikilizana, na ikiwa tu tutazingatia kanuni za msingi za kikatiba na kanuni za kidemokrasia zilizoifanya nchi hii kuwa yenye nguvu".

    th

    Chanzo cha picha, Getty Images

    Soma zaidi:

  16. Trump ajiandaa kuteua baraza la mawaziri katika siku zijazo

    .

    Chanzo cha picha, Get

    Rais Mteule Donald Trump ataanza kuteua baraza lake la mawaziri katika "siku na wiki zijazo", timu inayoongoza kipindi chake cha mpito kuelekea Ikulu imesema.

    Katika taarifa, wenyeviti wenza Linda McMahon na Howard Lutnick wanasema watamkabidhi Trump "wataalam kadhaa ambao anaweza kuchagua kwa ajili ya timu yake".

    Wanasema atachagua wafanyakazi ambao watatunga sera ambazo "zinafanya maisha ya Wamarekani kuwa nafuu na salama".

    Soma zaidi:

  17. Bilionea aliyeathiriwa pakubwa na shambulio la 9/11 anayemsaidia Trump kujenga timu yake ya maafisa wakuu

    TH
    Maelezo ya picha, Picha hii inaonyesha baadhi ya washauri waliokuwa jukwaani na Donald Trump kwenye hotuba yake ya ushindi.

    Huku Donald Trump akiibuka mshindi, macho sasa yatageukia mchakato wake wa kuingia Ikulu ya White House.

    Howard Lutnick, mmoja wa watu wanaoongoza timu ya mpito, alikuwa jukwaani na Trump jana usiku.

    Bilionea huyo anayoongoza kampuni ya kifedha ya Cantor Fitzgerald tayari amekuwa akiomba nyaraka za wasifu huku akitarajia kujaza maelfu ya nafasi za kazi za kisiasa katika utawala mpya.

    Lutnick ana uzoefu mkubwa wa kuajiri wafanyikazi haraka. Mashambulizi ya Septemba 11 kwenye jengo la World Trade Centre yaliua kila mfanyakazi wa Cantor Fitzgerald ofisini siku hiyo - zaidi ya watu 650, akiwemo kaka yake Lutnick.

    Licha ya uhusiano wake wa Wall Street, Lutnick amesema amejitolea kwa ajenda ya Trump ya ‘Make America Great Again’

    "Timu yake ya mpito itahakikisha utekelezaji wa ajenda ya Rais Trump kuanzia Siku ya 1," Lutnick na mwenyekiti mwenza Linda McMahon walisema katika taarifa Jumatano.

    Soma zaidi:

  18. Harris awaambia wafuasi wake 'wasikate tamaa' na kuahidi kumsaidia Trump katika makabidhiano ya madaraka

    .

    Chanzo cha picha, Getty Images

    Makamu wa rais wa Marekani Kamala Harris amekutana na wafuasi wake waliomkaribisha kwa shangwe huku wimbo wa Beyoncé wa Freedom ukiwa unacheza, ambao ulikuwa wimbo wa kampeni yake.

    'Nuru ya Marekani itang’aa kila wakati'

    "Moyo wangu unafuraha leo," Harris alisema, wakati akianza hotuba yake.

    "Nimejawa na shukrani kwa imani uliyoweka kwangu, iliyojaa upendo kwa nchi yetu na maazimio."

    Aliendelea kusema matokeo ya uchaguzi huu si yale aliyotarajia au kuyapigania.

    "Nuru ya Marekani itang’aa kila wakati mradi tu tusikate tamaa na pia tuendelee kupigana," aliongeza.

    Harris ashukuru familia yake

    Harris aliendelea kushukuru familia yake, ikiwa ni pamoja na mumewe ambaye alimwita " mpenzi wangu Doug", pamoja na Jill na Joe Biden, na mgombea mwenza wake Tim Walz na familia yake.

    Wamarekani wana mengi zaidi ya kuwapatanisha kuliko ya kuwatenganisha - Harris

    Kamala Harris aliwaambia wafuasi wake kwamba kampeni yake ilikuwa ya makusudi kuhusu "kujenga jumuiya na miungano", na kwa hilo anajivunia kile ambacho yeye na timu yake waliweza kufanya.

    Makamu wa rais alisema timu yake imeungana katika upendo wake kwa Marekani, shauku na furaha katika kupigania mustakabali wa nchi hiyo.

    Aliendelea kuongeza kuwa kampeni yake iliendeshwa na dhamira kwamba Wamarekani wana mengi zaidi ya kuwaweka pamoja kuliko ya kuwatenganisha.

    'Lazima tukubali matokeo ya uchaguzi huu'

    "Ninajua watu wanahisi na wanakabiliana na mihemko mbalimbali kwa sasa," Harris alisema. "Ninaelewa.

    " Lakini akaongeza, "lazima tukubali matokeo ya uchaguzi huu", na kuthibitisha kuwa amezungumza na Trump na kumpongeza kwa ushindi wake.

    Pia alisema alimwambia atashiriki katika "uhamishaji wa madaraka kwa amani" na atasaidia katika mchakato huo.

    "Kanuni ya msingi ya demokrasia" ni kukubali matokeo, aliongeza. Hii inatofautisha demokrasia na udhalimu, Harris alisema.

    .

    Soma zaidi:

  19. Hujambo na karibu katika matangazo yetu ya moja kwa moja ikiwa ni tarehe 07/11/2023