Sudan inawanyanyasa wanawake-HRW

Chanzo cha picha, Getty
Wanaharakati kutoka shirika la kutetea haki za binadamu la Human Rights Watch wamesema kuwa vikosi vya usalama nchini Sudan vinafanya ukatili wa kingono,vitisho na vitendo vingine vinavyokiuka haki za kibinadamu dhidi ya wanawake kwa lengo la kunyamazisha wanaharakati wanawake.

HRW linasema kuwa lina takriban mashahidi 12 wa vitendo vya ubakaji vilivyotekelezwa na maafisa wa usalama dhidi ya wanawake wanaopigania haki za kibinadamu.
Aidha HRW linasema kuwa maafisa wao hao wamewatishia wanaharakati wengine na ubakaji.

Chanzo cha picha, Getty Images
Wanaharakati wengine wanasema kuwa maafisa hao wa usalama pia wamewachafulia jina.
HRW inasema kuwa japo ukandamizaji na udhalilishwaji ni jambo la kawaida Sudan , wanawake wanakabiliwa na changamoto ya kipekee.

Chanzo cha picha, Getty
Maafisa wa serikali nchini Sudan wamekanusha madai ya kudhalilisha wanawake kingono au hata kwa ubakaji.








