Trump aahidi kuvunja mkataba wa nyuklia

Republican

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha, Trump ndiye anayeongoza miongoni mwa wagombea wa Republican

Mgombea Urais katika chama cha Republican nchini Marekani, Donald Trump, amesema kuwa akichaguliwa kuwa Rais hatua ya kwanza atakayochukua juu ya masuala ya kigeni ni kuvunjilia mbali mkataba wa nyuklia.

Mkataba huo ambao Trump anauzungumzia na kukerwa nao ni ule wa Marekani na Iran.

  • <link type="page"><caption> Ushindi wa Trump ni hatari kwa dunia</caption><url href="http://www.bbc.com/swahili/habari/2016/03/160317_trump_eiu_danger" platform="highweb"/></link>
  • <link type="page"><caption> Iran yaanza kutekeleza mkataba wa nyuklia</caption><url href="http://www.bbc.com/swahili/habari/2015/11/151102_iran_nuclear" platform="highweb"/></link>

Bw Trump, ambaye kwa sasa yuko mstari wa mbele katika kinyang'anyiro hicho katika chama chake aliliambia kundi lenye ushawishi mkubwa linalounga mkono Israel kuwa mapatano hayo ya Iran ni hatari kwa Marekani.

Amesema pamoja na madhara kwa Marekani lakini pia unaweza kuihatarisha Israel na Mashariki ya Kati.