Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Matokeo ya Uchaguzi Kenya 2022:Nyota walioibuka washindi na waliobwagwa katika uchaguzi wa Kenya
Huku matokeo ya uchaguzi wa Kenya uliofanyika siku ya Jumanne yakiendeea kutolewa katika maeneo mbali mbali ya nchi ,kuna kundi ambalo linaangaziwa pia wakati huu kujua walichuma vizuri na waliobwaga katika uchaguzi .
Kundi hilo ni la nyota tajika ,wanamuziki na watu mashuhuri hasa katika fani ya burudani ambao walijitosa katika siasa .
Mwanahabari Davidson Ngibuini, maarufu kama DNG, ameshinda kiti cha wadi ya Woodley, Kenyatta Golf Course
Aliwania chini ya chama cha UDA cha Naibu Rais William Ruto, alimshinda Mwangi Njihia wa Jubilee Party.
Huko huko Woodley, mmoja wa wanachama wa kundi la P-unit, Gabriel Kagundu, maarufu kama Gabu, alikuwa akitafuta nafasi hiyo hiyo na Alliance National Congress (ANC).
Alikubali kushindwa baada ya DNG kushinda kiti hicho
Msanii wa Kenya Kevin Kioko almaarufu Bahati, ambaye alikuwa akiwania ubunge kwa tikiti ya Jubilee, alipoteza azma yake ya kuwa mbunge wa Mathare.
Alikuwa akitafuta kurithi nafasi ya Anthony Oluoch.Hata hivyo hesabu zinaonyesha kwamba hatoweza kupata ushindi .
Aliyekuwa mtangazaji wa redio ya Kiss 100 na mchekeshaji Felix Odiwour kwa jina la usanii Jalang'o alimshinda mgombeaji Nixon Korir na kushinda kiti cha ubunge la Lang'ata kilicho katika kaunti ya Nairobi.
Mtangazaji maarufu wa redio na Mary Njambi Koikai alikuwa ameelekeza macho yake kwenye kiti cha ubunge cha Dagoretti Kusini.
Lakini ametuma ujumbe wa kukubali kushindwa .
Njambi, almaarufu Fyah Mummah, alikuwa akiwania kama mgombea huru lakini akakubali kushindwa.
Anita Sonia, mwanaharakati wa mazingira wa Kenya, pia amepoteza azma yake ya kuwa mbunge wa Kajiado Kaskazini.
"Jibu ni kusubiri. Wakati mwingine inaweza kuwa ndiyo. Nachukua nafasi hii kumpongeza mpinzani wangu na rafiki yangu Onesmus Nguro Ngogoyo wa UDA kwa kuwa mbunge mteule wa Kajiado Kaskazini," alisema.
Pia, mcheshi MC Jessy (Jasper Muthomi) amekubali kushindwa na kutoa ujumbe wa pongezi za dhati kwa mpinzani wake Shadrack Mwiti aliyekuwa akiongoza .
Nyota wa zamani wa soka wa timu ya taifa ya Harambee Stars Mcdonald Mariga pia amepoteza azma yake ya kuwa mbunge wa eneo bunge la Kibra kwa tiketi ya chama cha UDA.