Fahamu vyakula vitano vinavyoweza kukuokoa dhidi ya gharama za juu za maisha?

G

Chanzo cha picha, Getty Images

Karibu watu 690 million wanakabiliwa na njaa duniani, karibu asilimia 8.9% ya idadi ya watu wote duniani - ni sawa na watu 10 million kwa mwaka wanakabiliwa na njaaa , ambapo ni karibu watu 60 million kwa miaka 5,. Hii ni kwa mujibu wa Shirika la chakula duniani, FAO.

Licha ya malengo ya milenia ya Umoja wa Mataifa ya kuwa na ulimwengu usio na njaa ifikapo mwaka 2030, bado kuna wasiwasi kuhusu hatua za kukabiliana na janga hilo duniani. Zipo changamoto za mabadiliko ya tabia nchi, vita, hali ya uchumi, sera na majanga mengine yamekuwa vikwazo vyavinavcyotishia kufikiwa kwa lengo hilo.

FAO inasema, kunapaswa kuwa na mabadiliko makubwa ya kuhusu vyakula duniani na mfumo wa kilimo ili kuwaokoa watu milioni 690 wanaokabiliwa na njaa duniani na watu wengine bilioni 2 watakaokuwepo ifikapo mwaka 2050. Kuongeza uzalishaji kwenye kilimo na kuzalisha vyakula vinavyoweza kuhimili hali ya hewa, magonjwa, visivyolimwa kwa muda mrefu na kudumu kwa muda mrefu, ni suluhu inayopendekezwa na wataalamu.

Unaweza pia kusoma:

Kutokana na kupanda kwa gharama za maisha karibu katika maeneo mengi duniani kwa sasa kutokana na mtikisiko wa uchumi wa dunia katika miaka miwili iliyopita kutokana na janga la Corona na sasa athari za vita ya Ukraine na Urusi, vipo vyakula vinavyoweza kuwa kimbilio kwa watu wengi wakiwemo masikini katika kuokoa dunia na njaa. Vifuatavyo ni vyakula vitano vinavyoweza kutumika kupunguza gharama za juu za maisha.

Mihogo

G

Chanzo cha picha, Getty Images

Ni chakula pendwa kinachoweza kupikwa, kuchomwa, kukaangwa, kukaushwa, kusagwa ama kuliwa kilivyo. Kinatajwa kuwa cha kuhimili kwa hali zote kikiwa na uwezo wa kinachohifadhika na kudumu kwa muda mrefu. Kina asili ya Marekani Kusini. Nchi za Nigeria, Thailand, na Indonesia ni wazalishaji wakubwa wa zao la muhogo duniani.

Nchi hizi ni mara chache sana kusikia zikilalamika njaa ama mfumuko wa bei, kutokana na zao hili kutumika na wakazi wengi wakati wa shida na hali ngumu. Rais Yoweri Museveni wa Uganda hivi karibuni amewataka watu wake kugeukia mlo wa mihogo kama dawa ya kuporomoka kwa bei ya ngano wakati huu ambapo gharama ya maisha duniani kote imepanda.

"Kama hakuna mkate, kuleni muwogo [mihogo]," alisema.

Kuna aina ya mihogo inayoweza kuleta madhara kama haijapikwa, lakini mingi inayotumika sasa inaonekana kuwa salama kwa afya, ikiwa na virutubisho vya kutosha. Mihogo ina wanga wa kutosha inayosaidia nguvu. Gramu 100 ya muhogo ina Karoli 191, mingine ikiwa na vitamini, madini na kambamba muhimu kwa afya ya mlaji.

Viazi

g

Chanzo cha picha, Getty Images

Kama ilivyo kwa muhigo, viazi ni chakula kingine cha mizizi ambacho kinahimili hali zote ma kinaweza kutumika kupunguza gharama za juu za maisha. Vipo viazi zaidi ya aina 10 dunaini, lakini vilivyozoeleka ni viazi ulaya vya chipsi na viazi vitasmu vinavyotumika zaidi kwenye kifungua kinywa.

Zao hili pia huchukua muda mrefu kulimwa mpaka kuvunwa. Unaweza kukausha, kusaga, kukaangwa, kupikwa ama kuliwa vilivyo. Ni zao ambalo linaweza kutumika kupunguza gharama za maisha na hali ya njaa kwenye maeneo mengi duniani.

Mbaazi

a

Chanzo cha picha, Getty Images

Kwa mujibu wa Kituo cha Utafiti wa Kilimo, Ilonga mbaazi za muda mfupi hukomaa kati ya siku 120 hadi 125 kama miezi mitatu tu katika maeneo ya ukanda wa juu kwenye baridi, mbaazi za muda mfupi hukomaa kwa muda mrefu zaidi ya siku

Zipo mbaazi za kienyeji hukomaa kati ya siku 210 hadi 270. Mbaazi za muda mfupi hutoa mazao mengi zaidi ya zile za kienyeji iwapo zitalimwa kwa kuzingatia maelezo ya kitaalamu. Hili ni zao na chakula kinachoweza kusaidia kupatikana kwa chakula kwa muda mfupi.

Mtama

f

Chanzo cha picha, Getty Images

Mtama ni jamii ya nafaka, yenye mbegu ndogondogo. Ni moja ya zao ambalo likitumika vizuri husaidia kwa kiasi kikubwa kukabliana na mabadiliko ya hali ya nchi na pia katika vita ya kuzuia njaa. Mtama unaweza kusagwa na kutumika kama unga wa ugali,unaweza kupikiwa mikate, unaweza kuchemshwa na Kuliwa au unaweza kupikwa kama ubwabwa. Mtama aina ya SERENA na DOBBS zenye punje za kahawia hustawi kwenye eneo lenye mvua za wastani na hukomaa katika kipindi cha siku 110.

Uwele

Uwele siyo tu kwamba unastawi katika mazingiŕa magumu, lakini pia umeingia katika mioyo ya watu wengi wanaoishi katika maeneo kame. Uwele aina ya Gadam hulimwa sana katika maeneo kame ya Mashariki mwa Kenya. Kama ilivyo kwa mazao ya mtama, viazi, mihogo na mbaazi, Uwele pia ukitumika vyema, utaweza kusaidia kupunguza makali ya gharama za juu za maisha.