Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Matunzo ya ngozi: Bidhaa za urembo zinazodaiwa kuzuia kuzeeka zina msingi gani kisayansi?
Historia imeonyesha kuwa watu wametumia mbinu mbalimbali kuifanya ngozi kuwa changa licha ya kwamba umri unaoongezeka. Kuanzia utumiaji wa maziwa ya punda, kama yale ya Malkia Cleopatra wa Misri, hadi kujipaka zebaki kwenye ngozi kama watu wa enzi ya Elizabethan.
Ingawa kuna matibabu mengi ya ajabu ya utunzaji wa ngozi katika enzi ya kisasa, kama vile matumizi ya kondo la nyuma au vitu vya ajabu kabisa usoni na matumizi ya kisasa zaidi yakiegemea zaidi sayansi.
Lakini katika nyakati za kisasa, peptidi, vitu vinavyozuia ongezeko la oksijeni yaani antioxidants, na asidi hutumiwa sana katika viambato vya tiba za hali ya juu ili kuweka ngozi mchanga.
Haya yote si rahisi kwa wale ambao hawajui mengi kuhusu biolojia na kemia.
Ni vigumu kwa watu kuelewa kwamba bidhaa za kuzuia kuzeeka wanazonunua kwa ajili ya ngozi hazina msingi halisi wa kisayansi au ikiwa ni namna ya biashara tu na inaweza kuwa na athari sokoni.
Basi hebu tujue kuhusu vitu vitatu maarufu zaidi vinavyotumiwa katika bidhaa za urembo za kuzuia kuzeeka, ni msingi gani wa kisayansi unaozifanya?
Vitamini C
Bidhaa za vitamini C mara nyingi zinadaiwa kung'arisha na kuongeza uzalishaji wa collagen kwenye ngozi.
Safu ya kati ya ngozi (inayoitwa dermis) ina kolagini na elastini, ambazo huendana na kufanya ngozi kuwa na ugumu unaostahili na kunyumbulika.
Lakini kadiri tunavyozeeka, kolagini na mnyambuliko hupungua kwenye ngozi yetu ambayo na badala yake kusababisha mikunjo.
Vitamini C ni vigumu kidogo kuingia moja kwa moja kwenye ngozi na kuchochea mabadiliko.
Hii ni kwa sababu safu ya nje ya ngozi (epidermis) huwa kama kizuizi dhidi ya maji.
Vitamini C humumunyifu katika maji. Kwa hivyo ni ngumu kutengeneza bidhaa ambazo zinaweza kutoa vitamini C kwenye ngozi.
Lakini utafiti fulani unaonyesha kuwa bidhaa hiyo inaweza kuwa na ufanisi kwenye ngozi ikiwa mkusanyiko wa vitamini C utawekwa kwa asilimia tano.
Kwa mfano, utafiti mmoja uligundua kwamba wanawake 10 wenye umri wa kati ya miaka 50 na 60 waliopaka krimu yenye asilimia tano ya vitamini C kwenye mikono yao kwa muda wa miezi sita walikuwa wameongeza viwango vya kolagini kwenye ngozi zao.
Utafiti zaidi umeonyesha kuwa upakaji wa kila siku wa Vitamin C kwenye ngozi unaweza kupunguza kwa kiasi kikubwa hatari ya kuungua na jua yaani (hyperpigmentation) kwenye ngozi.
Tafiti nyingi zimebaini kuwa krimu zenye vitamini C na zisizo na vitamini C zilipakwa sehemu mbalimbali za mwili na kubaini kuwa watu waliotumia krimu zenye vitamini C kwa siku 47 walionyesha mabadiliko makubwa ya rangi ya ngozi baada ya siku 12.
Lakini hakukuwa na mabadiliko makubwa katika rangi ya ngozi baada ya siku 12 za kwanza.
Hata hivyo, haikujulikana ni muda gani mabadiliko ya ngozi yaliendelea baada ya utafiti kukamilika.
Asidi ya Hyaluronic
Asidi ya Hyaluronic ni dutu ya asili inayotengenezwa ndani ya mwili wetu.
Inapatikana katika viambatisho vya maji na mifupa na tishu kwenye macho.
Bidhaa nyingi za Ngozi pia sasa hivi zinajumuisha asidi ya Hyaluronic, kwa madai kuwa hii ni 'moisturizer' yaani yenye unyevu nzuri kwa ngozi na husaidia kupunguza kuonekana kwa mikunjo kwenye ngozi.
Katika utafiti wa 2011, wanawake 76 kati ya umri wa miaka 30 na 60 walitumia krimu yenye 0.1% ya asidi ya hyaluronic mara mbili kwa siku kwa miezi miwili, ambayo huongeza unyevu na unyumbufu wa ngozi zao.
Lakini kuboreka kwa makunyanzi na muonekano mbaya wa ngozi kulionekana tu wakati chembe za aside ya hyaluronic katika krimu zilikuwa ndogo, kwani chembe kubwa za asidi ya hyaluronic haziingizii kwa urahisi kwenye ngozi.
Lakini baadhi ya creamu za ngozi zilizo na asidi ya hyaluronic hazielezei ikiwa ukubwa wa chembe za asidi ya hyaluronic katika bidhaa ni kubwa au ndogo, na hivyo ni vigumu kuamua wakati wa ununuzi.
Ni muhimu kujua aina ya asidi ya hyaluronic na kiwango chake kwenye krimu kwa kuangalia lebo wakati wa kununua bidhaa.
Hata hivyo tafiti nyingine nyingi zimeonyesha kuwa krimu au bidhaa za asidi ya hyaluronic ama bidhaa zinazoweza kudungwa kwenye ngozi husaidia kuongeza maji kwenye ngozi na kupunguza mikunjo.
Utafiti wa 2021 uligundua kuwa watu waliotumia krimu za asidi ya hyaluronic walikuwa wameboresha sana ngozi zao, kupunguza ukavu wa ngozi na kupunguza mikunjo ama makunyanzi.
Lakini pia ni muhimu kutambua kwamba utafiti huu ulitumia bidhaa za biashara zenye mchanganyiko wa niacinamide, keramidi na asidi ya hyaluronic na ilitumiwa mara mbili, ikiwa ni pamoja na mtu kupigwa na jua kila siku.
Hii inafanya iwe vigumu kuhitimisha kwamba matokeo hayo yalitokana na asidi ya hyaluronic pekee.
Retinol
Bidhaa za retinol pia zinajulikana siku hizi na zinadaiwa kupunguza uharibifu wa muda mrefu wa ngozi kutokana na jua (inayoitwa photoaging) ikiwa ni pamoja na 'hyperpigmentation' yaani sehemu ya Ngozi kuwa nyeusi sana kwa sababu ya kuongezeka kwa melanini na makunyanzi.
Retinol inatokana na Vitamini-A.
Baada ya kufyonzwa ndani ya ngozi, inabadilishwa kuwa asidi ya retinoic.
Mara baada ya kufyonzwa ndani ya ngozi, inakuza uundaji wa kolagini na kuharakisha uundaji wa seli za ngozi.
Haya yote husaidia kupunguza kutokea kwa makunyanzi na sehemu zenye weusi kwenye ngozi.
Tafiti mbalimbali kwenye seli za binadamu, sampuli za ngozi na binadamu zimeonyesha kuwa bidhaa zenye retinol hubadilisha mwonekano wa ngozi.
Kwa mfano, utafiti wa wanadamu ulionyesha kuwa kutumia retinol 0.4% mara tatu kwa wiki kwa miezi sita ilipunguza kuonekana kwa makunyanzi.
Utafiti wa awali uligundua kuwa kutumia bidhaa zenye 0.04% za retinol kwa hadi wiki 12 kunaweza kuwa na athari kwenye ngozi.
Hata hivyo, hii sio athari sawa na bidhaa za retinol. Bidhaa zilizo na angalau 0.04% za retinol zinaweza kuwa na athari za kupunguza kuonekana kwa mikunjo kwenye ngozi baada ya miezi kadhaa ya matumizi, hasa wakati zinatumiwa pamoja na bidhaa nyingine za kujikinga dhidi ya jua.
Je unapaswa kuchukua bidhaa gani za ngozi?
Ikiwa unafikiria kununua bidhaa za utunzaji wa ngozi za kuzuia kuzeeka, kumbuka mambo haya.
Kwanza, angalia ikiwa una mzio wa viungo vyovyote katika bidhaa na ikiwa inafanana na aina ya ngozi yako.
Kwa mfano, ikiwa ngozi yako ni kavu, retinol inaweza isiwe sawa kwako kwani inaweza kuongeza madhara katika ngozi yako kwasababu ya jua na kukusababishia usumbufu zaidi.
Zingatia viungo vinavyofanya kazi katika bidhaa na ufuate maagizo ya mtengenezaji kwa matumizi.
Lebo ina maelezo haya yote.
Ndio, unapaswa kukumbuka kuwa bidhaa unayonunua haiwezi kuwa tiba ya kila kitu.
Pamoja na hayo maisha ya kawaida yenye kuendeleza afya njem ni muhimu.
Kunapaswa kuwa na lishe bora na mapumziko ya kutosha ambayo yatakuwa na athari chanya kwenye ngozi yako.